Kuhusu Ayubu (Sehemu 2)

07/09/2019

Urazini wa Ayubu

Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye urazini zaidi alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake. Machaguo kama hayo ya kirazini yasingeweza kutenganishwa na shughuli zake za kila siku na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa amejua kwenye maisha yake ya siku baada ya siku. Uaminifu wa Ayubu ulimfanya kuweza kusadiki kwamba mkono wa Yehova unatawala mambo yote; imani yake ilimruhusu kujua ukweli wa ukuu wa Yehova Mungu juu ya vitu vyote; maarifa yake yalimfanya kuwa radhi na kuwa na uwezo wa kutii ukuu na mipangilio ya Yehova Mungu juu ya vitu vyote; utiifu wake ulimwezesha kuwa mkweli na mkweli zaidi katika kumcha kwake kwa Yehova Mungu; kumcha kwake kulimfanya kuwa halisi zaidi na zaidi katika kujiepusha kwake na maovu; hatimaye, Ayubu alikuwa mtimilifu kwa sababu alimcha Mungu na kujiepusha na maovu; na ukamilifu kwake kulimfanya kuwa na hekima zaidi na kukampa urazini wa kipekee.

Tunafaa kulielewa vipi neno hili, “urazini”? Ufasiri wa moja kwa moja unamaanisha kwamba kuwa mwenye hisia nzuri, kuwa mwenye mantiki na wa kueleweka katika kufikiria kwako, kuwa na maneno ya kueleweka, vitendo na hukumu ya kueleweka, na kumiliki viwango visivyo na makosa na maadili ya mara kwa mara. Lakini urazini wa Ayubu hauelezwi sana kwa urahisi. Inaposemekana hapa kwamba Ayubu alimiliki urazini wa kipekee, inahusiana na ubinadamu wake na mwenendo wake mbele ya Mungu. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwaminifu, aliweza kuusadiki na kuutii ukuu wa Mungu, uliompa maarifa ambayo yasingeweza kupatikana na wengine na maarifa haya yalimfanya kuweza kutambua, kuhukumu, na kufafanua kwa usahihi zaidi yale yaliyompata, na yaliyomwezesha kuchagua ni nini cha kufanya na ni nini cha kushikilia kwa usahihi na wepesi zaidi wa kukata ushauri. Hivi ni kusema kwamba maneno, tabia, na kanuni zake ziliandamana na hatua zake, na msimbo ambao aliufanyia kazi, ulikuwa wa mara kwa mara, ulio wazi, na mahususi na haukukosa mwelekeo, wenye uamuzi wa haraka au wa kihisia. Alijua namna ya kushughulikia chochote kile kilichompata yeye, alijua namna ya kusawazisha na kushughulikia mahusiano kati ya matukio magumu, alijua namna ya kushikilia mambo kwa njia ambayo mambo hayo yalifaa kushikiliwa, na, vilevile, alijua namna ya kushughulikia ule utoaji na uchukuaji wa Yehova Mungu. Huu ndio uliokuwa urazini wenyewe wa Ayubu. Ilikuwa hasa kwa sababu Ayubu alijihami na urazini kama huu ndiposa akasema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake wa kiume na kike.

Wakati Ayubu alipokabiliwa na maumivu makali ya mwili, na malalamiko ya watu wa ukoo na marafiki zake, na wakati alipokabiliwa na kifo, mwenendo wake halisi kwa mara nyingine tena ulionyesha kimo chake kwa mambo yote.

Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu

Asili Halisi ya Ayubu: Mkweli, Aliyetakaswa, na Asiye na Uongo

Hebu tusome Ayubu 2:7-8: “Hivyo Shetani akatoka mbele za uwepo wa Yehova, na akamgonga Ayubu kwa majipu ya kuuma kutoka kwenye wayo wa mguu wake hadi utosini mwa kichwa chake. Na akachukua kigae kwa ajili ya kujikuna nacho; naye akakaa chini kwenye majivu.” Huu ni ufafanuzi wa mwenendo wa Ayubu wakati ambapo majipu yawashayo yalipoota kwenye mwili wake. Wakati huu, Ayubu aliketi kwenye majivu huku akiyavumilia. Hakuna aliyemtibu yeye, na hakuna aliyemsaidia kupunguza maumivu kwenye mwili wake; badala yake, alitumia kigaye cha chungu kukwaruza sehemu ya juu ya majipu yake yenye maumivu. Juu juu, hii ilikuwa awamu tu ya mateso ya Ayubu na haina uhusiano wowote na ubinadamu wake na kumcha Mungu kwake, kwani Ayubu hakuongea maneno yoyote kuonyesha hali na maoni yake wakati huo. Lakini matendo na mwenendo wake Ayubu bado ni onyesho la kweli la ubinadamu wake. Kwenye rekodi za sura ya awali tunasoma kwamba Ayubu alikuwa ndiye mkuu zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki. Kifungu hiki cha sura ya pili, nacho, kinatuonyesha kwamba binadamu huyu mkuu wa mashariki hakika alichukua kigae cha chungu na kujikwaruza nacho huku akiwa ameketi kwenye jivu. Je, hakuna ulinganuzi wowote wa wazi kati ya fafanuzi hizi mbili? Ni ulinganuzi unaotuonyesha nafsi ya kweli ya Ayubu: Licha ya nafasi na hadhi yake ya kifahari, hakuwahi kuzipenda wala kuzitilia maanani yoyote; hakujali namna wengine walivyoangalia nafasi yake wala kuhusu kama hatua au mwenendo wake ungekuwa na athari mbaya kwa nafasi yake; hakujihusisha katika utajiri wa hali, wala hakufurahia utukufu uliokuja pamoja na hadhi na nafasi yake katika jamii. Alijali tu kuhusu thamani yake na umuhimu wa kuishi kwake mbele ya macho ya Yehova Mungu. Nafsi ya kweli ya Ayubu ilikuwa kiini chake: Hakupenda umaarufu na utajiri, na wala hakuishi kwa ajili ya umaarufu na utajiri; alikuwa mkweli, na aliyetakaswa, na aliye bila ya uongo wowote.

Kuhusu Ayubu (Sehemu 2)

Utenganisho wa Ayubu kati ya Upendo na Chuki

Upande mwingine wa ubinadamu wa Ayubu unaonyeshwa katika mazungumzo yake na mke wake: “Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe. Lakini yeye akasema kwake, Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:9-10). Kuona mateso aliyokuwa akipitia, mke wa Ayubu alijaribu kumshauri Ayubu ili amsaidie kutoroka mateso yake—lakini zile “nia nzuri” hazikupata idhini ya Ayubu; badala yake, ziliamsha ndani yake hasira, kwani alikataa imani yake katika na utiifu wake kwa Yehova Mungu na pia akakataa uwepo wa Yehova Mungu. Hali hii isingeweza kuvumilika kwa Ayubu, kwani hakuwahi kujiruhusu kufanya chochote ambacho kingepinga au kingemdhuru Mungu, bila kusema chochote kuhusu wengine. Angewezaje kubakia vilevile bila kujali chochote wakati alipowaona wengine wakiongea maneno yaliyomkufuru na kumtukana Mungu? Hivyo basi akamuita mke wake “mwanamke mjinga.” Mwelekeo wa Ayubu kwa mke wake ulikuwa ule wa hasira na chuki, pamoja na ule wa kushutumu na kukemea. Haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kiasili ya ubinadamu wa Ayubu ambayo yalitofautisha kati ya upendo na chuki na yalikuwa uwakilishi wa kweli wa ubinadamu wake uliokuwa na unyofu. Ayubu alimiliki hali fulani ya haki—hali ambayo ilimfanya kuchukia upepo na mawimbi ya maovu, na kumfanya kuchukia, kushutumu, na kukataa uzushi wa ajabu, mabishano ya kijinga na madai yasiyokuwa na msingi, na ikamruhusu kushikilia kanuni zake sahihi, za kweli kwake yeye mwenyewe na msimamo ule aliochukua wakati alipokuwa amekataliwa na wengi na kuachwa na wale walio kuwa karibu na yeye.

Ukarimu na Uaminifu wa Ayubu

Kwa sababu, kutoka katika mwenendo wa Ayubu, tunaweza kuona maonyesho ya vipengele mbalimbali vya ubinadamu wake, tunauona ubinadamu wa Ayubu upi anapokifunua kinywa chake kuilaani siku aliyozaliwa? Hii ndiyo mada tutakayozungumzia hapa chini.

Hapo juu, Nimezungumzia asili ya laana la Ayubu ya siku ya kuzaliwa kwake. Mnaona nini katika haya? Kama Ayubu asingekuwa mkarimu na asiye na upendo, kama angekuwa mnyama na asiye na hisia, na mpungufu wa ubinadamu, angejali kuhusu tamanio la moyoni mwa Mungu? Na je angedharau siku ya kuzaliwa kwake kutokana na kuutunza moyo wa Mungu? Kwa maneno mengine kama Ayubu alikuwa hana ukarimu na aliyepungukiwa na ubinadamu, angedhikishwa na maumivu ya Mungu? Angeilaani siku yake ya kuzaliwa kwa sababu Mungu alikuwa amedhulumiwa na yeye? Jibu ni, bila shaka la! Kwa sababu alikuwa mkarimu, Ayubu aliutunza moyo wa Mungu; kwa sababu aliutunza moyo wa Mungu, Ayubu alihisi maumivu ya Mungu; kwa sababu alikuwa mkarimu, alipata maumivu makali zaidi kutokana na kuyahisi maumivu ya Mungu; kwa sababu aliyahisi maumivu ya Mungu, alianza kuichukia siku ya kuzaliwa kwake, na hivyo akailaani siku yake ya kuzaliwa. Kwa watu wa nje, mwenendo wote wa Ayubu wakati wa majaribio yake ni wa kupigiwa mifano. Kulaani kwake tu kwa siku ya kuzaliwa ndiko kunakoweka picha ya kiulizo juu ya utimilifu na unyofu wake, au kutoa utathmini tofauti. Kwa hakika, haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kweli zaidi ya kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Kiini cha ubinadamu wake hakikufichwa au kubadilishwa, au kudurusiwa na mtu mwingine. Alipoilaani siku yake ya kuzaliwa, alionyesha ukarimu na uaminifu uliokuwa ndani ya moyo wake; alikuwa kama chemichemi ya maji ambayo maji yake yalikuwa safi sana na angavu kiasi cha kufichua sehemu ya chini kabisa ya chemichemi hio.

Baada ya kujifunza haya yote kuhusu Ayubu, watu wengi zaidi bila shaka watakuwa na utathmini sahihi kwa kiasi fulani na usiopendelea kuhusu kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Wanafaa pia kuwa na uelewa na kina kikuu cha kimatendo, na uliopevuka zaidi wa utimilifu na unyofu wa Ayubu kama ulivyozungumzwa na Mungu. Ni tumaini langu kwamba, uelewa na kina hiki kitawasaidia watu kuanza kushughulikia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Iliyotangulia: Kuhusu Ayubu (Sehemu 1)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Ayubu (Sehemu 1)

Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp