Ayubu Amshinda Shetani na Kuwa Binadamu Wa Kweli Machoni pa Mungu

07/09/2019

Ayubu Amshinda Shetani na Kuwa Binadamu Wa Kweli Machoni pa Mungu

Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. Alikuwa ameshinda majaribio ya Shetani, na alikuwa ameshinda rasilimali zake zote za dunia na watoto wake, na majaribio ya kupoteza mali yake ya dunia, hivi ni kusema kwamba aliweza kutii Mungu kuchukua na kutwaa kutoka kwake na akatoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa sababu ya hayo. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Shetani, na huo ndio uliokuwa ushuhuda wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Mungu. Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu. Wakati wa majaribio haya, Ayubu alitumia mwenendo wake halisi kumtangazia Shetani kwamba maumivu ya mwili wake yasingebadilisha imani yake na utiifu wake kwa Mungu au kuchukua ule upendo wake kwa Mungu na kumcha Mungu; asingemuacha Mungu au kutupilia mbali utimilifu wake binafsi na unyofu kwa sababu alikuwa amekabiliwa na kifo. Bidii ya Ayubu ilimfanya Shetani mwoga, imani yake ilimuacha Shetani akiwa na dukuduku na kutetemeka, nguvu za vita vya maisha yake na kifo chake na Shetani viliweza kuzua chuki na dharau nyingi kwa Shetani, utimilifu na unyofu wake ulimuacha Shetani akiwa hana chochote zaidi cha kumfanya kiasi cha kwamba Shetani aliyaacha mashambulizi yake kwake na kukata tamaa na mashtaka yake dhidi ya Ayubu mbele ya Yehova Mungu. Hii ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa ameushinda ulimwengu, alikuwa ameushinda mwili wake, alikuwa amemshinda Shetani, na alikuwa ameshinda kifo; alikuwa kwa kweli na hakika binadamu aliyemilikiwa na Mungu. Wakati wa majaribio haya mawili, Ayubu alisimama imara katika ushuhuda wake, na kwa hakika aliishi kwa kudhihirisha utimilifu wake na unyofu, na akapanua upana wa kanuni zake za kuishi za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Baada ya kupitia majaribio haya mawili, ndani ya Ayubu kulizaliwa uzoefu mwingi, na uzoefu huu ulimfanya yeye kuwa mwenye kimo na uzoefu zaidi, ilimfanya kuwa mwenye nguvu zaidi, na imani kubwa zaidi, na ilimfanya yeye kuwa na ujasiri zaidi kuhusu haki na ustahili wa uadilifu ambao yeye alishikilia kwa dhati. Majaribio ya Yehova Mungu kwa Ayubu yalimpa uelewa wa kina na hisia za wasiwasi wa Mungu kwa binadamu, na kumruhusu yeye kuhisi thamani ya upendo wa Mungu, ambapo vyote vinaelekezwa katika utiliaji maanani kwa na kuhusu upendo wa Mungu na vyote viliweza kuongezwa katika kumcha Mungu. Majaribio ya Yehova Mungu kumwondoa tu Ayubu kutoka Kwake, lakini pia yaliuleta moyo wake karibu na Mungu. Wakati maumivu yale ya mwili yaliyovumiliwa na Ayubu yalifikia kilele, wasiwasi aliouhisi kutoka kwa Yehova Mungu haukumpa chaguo lolote ila kuilaani siku yake ya kuzaliwa. Mwenendo kama huo haukuwa umepangiliwa mapema lakini ulikuwa ni ufunuo wa kiasili wa kutilia maanani na kumpenda Mungu kutoka ndani ya moyo wake, ulikuwa ni ufunuo wa kiasili uliotoka kwenye kutilia maanani na kumpenda Mungu kwake. Hivi ni kusema, kwa sababu alijichukia, na hakuwa na radhi na hakuweza kuvumilia kuona Mungu Akiteswa, hivyo kutilia maanani na upendo wake vilifika hali ya kutojijali. Wakati huu, Ayubu aliimarisha kuabudu kwake kwa muda mrefu na kutamani kwake kwa Mungu na upendo kwa Mungu hadi katika kiwango cha utiliaji maanani na upendo. Wakati huohuo, aliweza kupandisha imani na utiifu wake kwa Mungu na kumcha Mungu kwake hadi katika kiwango cha kutilia maanani na upendo. Hakujiruhusu kufanya chochote ambacho kingesababisha madhara kwa Mungu, hakujiruhusu mwenendo ambao ungemuumiza Mungu, na hakujiruhusu kuleta masikitiko, huzuni au hata kutokuwa na furaha kokote kwake Mungu kwa sababu zake mwenyewe. Katika Macho ya Mungu, ingawaje Ayubu alikuwa bado Ayubu wa hapo awali, imani, utiifu na kumcha Mungu kwake kulikuwa kumemletea Mungu utoshelezi kamilifu. Wakati huu, Mungu alitarajia Ayubu kuweza kutimiza, alikuwa amegeuka kuwa mtu aliyestahili kuitwa “mtimilifu na mnyofu” mbele ya macho ya Mungu. Vitendo vyake vya haki vilimruhusu yeye kumshinda Shetani na kuwa makini katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mtimilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuimarishwa, kuzidishwa zaidi kuliko awali, na kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishinda na kumlemea Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuendelea mbele, Ayubu akawa binadamu wa kwanza ambaye hangewahi tena kukabidhiwa Shetani, kwa kweli alikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na akaishi kwenye nuru, katika baraka za Mungu bila ya kupelelezwa au kuangamizwa na Shetani.… Alikuwa amekuwa binadamu wa kweli katika macho ya Mungu; alikuwa ameachiliwa huru. …

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Ayubu (Sehemu 1)

Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe,...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp