Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu

07/09/2019

Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya malaika waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za vitendo vyake vya kila siku, na mwelekeo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli. Kama Ayubu hangekuwa amejaribiwa, kama Mungu Asingekuwa Amemletea Ayubu majaribio, wakati Ayubu aliposema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” ungesema kwamba Ayubu alikuwa mnafiki; Mungu alikuwa amempa rasilimali nyingi, hivyo bila shaka alilibariki jina la Yehova. Kama, kabla ya kupitia majaribio, Ayubu angekuwa amesema, “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Ungesema kwamba Ayubu alikuwa akipiga chuku, na kwamba hangeliacha jina la Mungu kwa sababu mara nyingi alibarikiwa kwa mkono wa Mungu. Kama Mungu Angekuwa Amemletea janga, basi kwa kweli angeliacha jina la Mungu. Lakini wakati Ayubu alipojipata katika hali hizi ambazo hakuna yeyote angetaka kujipata ndani au kutaka kuona, au kutaka zimpate, ambazo watu wangeogopa kupata, hali ambazo hata Mungu mwenyewe Hakuweza kuvumilia kuzitazama, bado Ayubu aliweza kushikilia uadilifu wake: “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” na “tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Kama wangekumbwa na mwenendo wa Ayubu wakati huu, wale wanaopenda kuzungumzia maneno ya kuonyesha umuhimu na kuvutia, na wale wanaopenda kuongea barua na mafundisho ya dini, wote wanaachwa wanyamavu. Wale wanaotukuza jina la Mungu kwa matamshi pekee, ilhali hawajawahi kukubali majaribio ya Mungu, wanashutumiwa na uadilifu ambao Ayubu alishikilia kwa dhati, na wale ambao hawajawahi kusadiki kwamba binadamu anaweza kushikilia kwa dhati njia ya Mungu wanahukumiwa na ushuhuda wa Ayubu. Wakiwa wamekabiliwa na mwenendo wa Ayubu wakati wa majaribio haya na maneno aliyoyaongea, baadhi ya watu watahisi wakiwa wamechanganyikiwa, baadhi watamwonea wivu, baadhi wahisi shaka, baadhi wataonekana hata wasio na haja ya kufuatilia mambo haya, huku wakiukataa ushuhuda wa Ayubu kwa sababu hawayaoni tu mateso yaliyompata Ayubu wakati wa majaribio, na kusoma maneno yaliyozungumzwa na Ayubu, lakini pia ule “unyonge” wa binadamu uliofichuliwa na Ayubu wakati majaribio yalipomsibu. “Unyonge” huu wanaoamini kuwa ile hali ya kudaiwa ya kutokuwa mtimilifu katika utimilifu wa Ayubu, doa katika binadamu ambaye katika macho ya Mungu alikuwa mtimilifu. Hivi ni kusema kwamba, inasadikiwa kwamba wale walio watimilifu hawana doa wala toa, hawana dosari wala hila, kwamba hawana unyonge wowote, hawana habari yoyote kuhusu maumivu, kwamba hawahisi katu wakiwa wamehuzunika au wamekataliwa, na hawana chuki au tabia yoyote ya nje isiyofaa; kutokana na haya, watu wengi hawasadiki kwamba Ayubu alikuwa kwa kweli mtimilifu. Watu hawaidhinishi mambo mengi kuhusu tabia yake wakati wa majaribio yake. Kwa mfano, wakati Ayubu alipopoteza mali yake na watoto wake, hakuweza, kama vile watu wanavyofikiria, kuanza kulia. “Utovu wake wa adabu” unawafanya watu kufikiria alikuwa jiwe, kwani hakuwa na machozi wala upendo kwa familia yake. Hii ndiyo picha mbaya ya kwanza ambayo Ayubu anawaonyesha watu. Wanafikiri tabia yake baada ya hapo kuwa ya kushangaza zaidi: “akalipasua joho lake” ni kauli iliyotafsiriwa na watu kuonyesha utovu wake wa heshima kwa Mungu, na “kunyoa kichwa chake” kunasadikiwa visivyo kumaanisha kukufuru kwa Ayubu na upinzani wake kwa Mungu. Mbali na maneno ya Ayubu kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” watu hawatambui uhaki wowote ndani ya Ayubu uliosifiwa na Mungu, na hivyo ukadiriaji kuhusu Ayubu uliofanywa na wengi wao si chochote zaidi ya kutofahamu, kutoelewa, shaka, lawama, na idhinisho kwa nadharia tu. Hakuna kati yao anayeweza kuelewa na kushukuru kwa kweli maneno ya Yehova Mungu kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Kutokana na picha yao kuhusu Ayubu hapo juu, watu wana shaka zaidi kuhusiana na uhaki wake, kwani vitendo na mwenendo wa Ayubu uliorekodiwa kwenye maandiko haukuwa wenye mguso wa kina kama vile watu wangefikiria. Hakutekeleza tendo lolote kubwa tu, lakini pia alikichukua kigae ili ajikwaruze akiwa ameketi kwenye jivu. Kitendo hiki kinawashangaza pia watu na kuwafanya kutilia shaka—na hata kukataa—uhaki wa Ayubu, kwani wakati akijikwaruza Ayubu hakumwomba Mungu, au kutoa ahadi kwa Mungu; wala, zaidi ya hayo, hakuonekana akilia machozi ya maumivu. Wakati huu, watu wanauona tu unyonge wa Ayubu na wala sio chochote kingine, na hivyo hata wanapomsikia Ayubu akisema “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” hawaguswi kamwe, au vinginevyo hawaonekani kuamua chochote, na bado hawawezi kutambua uhaki wa Ayubu kutoka kwa maneno haya. Picha ya kimsingi ambayo Ayubu anapatia watu wakati wa mateso ya majaribio yake ni kwamba alikuwa si mnyenyekevu wala mwenye kiburi. Watu hawaioni hadithi inayotokana na tabia yake iliyojitokeza katika kina cha moyo wake, wala hawaioni ile hali yake ya kumcha Mungu ndani ya moyo wake au kutii kwa kanuni ya njia ya kujiepusha na maovu. Utulivu wake unawafanya watu kufikiria kuwa utimilifu na unyofu wake vyote vilikuwa ni maneno matupu tu, kwamba kumcha kwake Mungu kulikuwa tu uvumi; ule “unyonge” alioufichua kwa nje, wakati huo, unawaachia picha ya kina, ukiwapatia “mtazamo mpya” kuhusu, na hata “uelewa mpya” kuhusu binadamu yule ambaye Mungu anafafanua kuwa mtimilifu na mnyofu. “Mtazamo mpya” na “uelewa mpya” kama huo vyote vinathibitishwa wakati Ayubu alipokifungua kichwa chake na kulaani siku aliyozaliwa.

Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu

Ingawaje kiwango cha mateso aliyoyapitia hakifikiriki wala kufahamika kwa binadamu yeyote, hakuzungumza maneno yoyote ya uvumi, lakini alipunguza tu maumivu ya mwili wake kwa njia zake mwenyewe. Kama ilivyorekodiwa kwenye maandiko, alisema: “Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba” (Ayubu 3:3). Pengine, hakuna yeyote aliyewahi kutilia maanani maneno haya na kuona kwamba ni muhimu, na pengine kunao watu ambao wameyatilia maanani. Kwa maoni yenu, yanamaanisha kwamba Ayubu alimpinga Mungu? Je, ni malalamiko dhidi ya Mungu? Najua kwamba wengi wenu mnayo mawazo fulani kuhusu maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu na mnasadiki kwamba kama Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, hakufaa kuonyesha unyonge wowote au huzuni yoyote, na badala yake alifaa kukabiliana vilivyo na shambulizi lolote kutoka kwa Shetani kwa njia nzuri, na hata kutabasamu wakati alikumbwa na majaribio ya Shetani. Hakufaa kuwa na mwitikio hata mdogo kuhusiana na mateso aliyoyapata kwenye mwili wake kutokana na Shetani, wala hakufaa kuonyesha hisia zozote ndani ya moyo wake. Alifaa hata kuuliza kwamba Mungu Ayafanye majaribio haya kuwa mabaya zaidi. Haya ndiyo yanayofaa kuonyeshwa na kumilikiwa na mtu ambaye hatikisiki na ambaye anamcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na maovu. Katikati ya mateso haya makuu, Ayubu hakufanya chochote ila kulaani siku aliyozaliwa. Hakulalamika kuhusu Mungu, hakuwa na nia yoyote ya kumpinga Mungu. Hali hii ni rahisi zaidi ikisemwa kuliko kutendwa, kwani tangu enzi za zamani hadi wa leo, hakuna yeyote ambaye amewahi kupitia majaribio kama hayo au kuteseka kama vile Ayubu alivyoteseka. Na kwa nini hakuna yeyote ambaye amepitia aina hiyo ya majaribio ya Ayubu? Kwa sababu, kama vile Mungu Anavyoona, hakuna yeyote anayeweza kuvumilia wajibu au agizo kama hilo, hakuna anayeweza kufanya kama Ayubu alivyofanya, na, zaidi, hakuna yule ambaye bado, mbali na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake, anaweza kutoliacha jina la Mungu na kuendelea kubariki jina la Yehova Mungu, kama vile Ayubu alivyofanya wakati mateso kama hayo yalimpata. Je, mtu yeyote angeweza kufanya hivi? Tunaposema haya kumhusu Ayubu, tunapongeza tabia yake? Alikuwa binadamu mwenye haki, na aliyeweza kuwa na ushuhuda kama huo kwa Mungu, aliyeweza kumfanya Shetani kutoroka kwa haraka sana, ili asiwahi kuja mbele ya Mungu tena na kumshtaki yeye—kwa hivyo nini mbaya na kumpongeza? Inaweza kuwa kwamba mnavyo viwango vya juu zaidi kuliko Mungu? Inaweza kuwa kwamba mngechukua hatua hata bora zaidi kuliko Ayubu wakati majaribio yatakapowasibu? Ayubu alisifiwa na Mungu—ni upinzani upi mnaoweza kuwa nao?

Ayubu Anailaani Siku Ya Kuzaliwa Kwake Kwa Sababu Hamtaki Mungu Kupata Maumivu Kwa Sababu Yake

Mara nyingi mimi husema kwamba Mungu huangalia ndani ya mioyo ya watu, na watu huangalia namna watu walivyo kwa nje. Kwa sababu Mungu anaangalia ndani ya mioyo ya watu, Anaelewa kiini chao, huku nao watu wanafafanua kiini cha watu wengine kutokana na wanavyoonekana kwa nje. Wakati Ayubu alipoufunua mdomo wake na kulaani siku ya kuzaliwa kwake, kitendo hiki kilishangaza wahusika wote wa kiroho, wakiwemo wale marafiki watatu wa Ayubu. Binadamu alitoka kwa Mungu, na anafaa kuwa mwenye shukrani kwa maisha na mwili, pamoja na siku yake ya kuzaliwa, aliopewa na Mwenyezi Mungu, na wala hafai kuilaani. Hali hii inaeleweka na kufahamika na watu wengi. Kwa yeyote yule anayemfuata Mungu, uelewa huu ni takatifu na dhabiti, ni ukweli usioweza kubadilika. Ayubu, kwa mkono mwingine, alizivunja sheria: Aliilaani siku ya kuzaliwa kwake. Hiki ni kitendo ambacho watu wa kawaida huchukulia kuwa kinajumuisha kuvuka hadi kwenye eneo haramu. Yeye hastahili tu uelewa na huruma ya watu, lakini pia hastahili msamaha wa Mungu. Wakati huohuo, hata watu wengi zaidi wanatilia shaka uhaki wa Ayubu, kwani inaonekana kana kwamba kibali cha Mungu kwake yeye kilimfanya Ayubu kujifikiria yeye mwenyewe, kilimfanya kuwa jasiri sana na asiyejali kiasi cha kwamba hakuweza tu kutoshukuru Mungu kwa kumbariki yeye na kumtunza yeye wakati wa maisha yake, lakini pia aliilaani siku ya kuzaliwa kwake na kuomba ingeangamizwa. Hii ni nini, kama si kumpinga Mungu? Mambo ya juujuu kama hayo yanawapa watu ithibati ya kushutumu kitendo hiki cha Ayubu, lakini ni nani anayejua kile Ayubu alichokuwa akifikiria kwa kweli wakati huo? Na ni nani anayeweza kujua sababu ya Ayubu kufanya hivyo? Mungu pekee na Ayubu mwenyewe ndio wanaojua hadithi ya ndani na sababu husika hapa.

Wakati Shetani alipounyosha mbele mkono wake ili kudhuru mifupa ya Ayubu, Ayubu aliangukia mashiko yake, bila ya mbinu za kutoroka au nguvu za kumpinga. Mwili na nafsi yake iliteseka na kupata maumivu makali, na maumivu haya yalimfanya kufahamu kwa kina kuhusu kutokuwa na umuhimu, unyonge, na hali ya kutokuwa na mamlaka iliyokuwemo ndani ya mwili. Wakati huohuo, alipata shukrani na uelewa mkubwa wa kwa nini Mungu Anatilia maanani kujali na kutunza wanadamu. Akiwa ameangukia mashiko ya Shetani, Ayubu alitambua kwamba binadamu, aliye katika mwili na damu, kwa hakika hana nguvu kamwe. Wakati aliposujudu na kumwomba Mungu, alihisi ni kana kwamba Mungu Alikuwa akiufunika uso Wake na kujificha, kwani Mungu Alikuwa Amemweka kabisa katika mikono ya Shetani. Wakati huohuo, Mungu Alimlilia yeye, na, zaidi, Alimsikitikia yeye; Mungu Aliumizwa na maumivu yake na Aliumia kwa maumivu yake.… Ayubu alihisi maumivu ya Mungu, pamoja na namna ambavyo haikuweza kuvumilika kwa Mungu.… Ayubu hakutaka kuleta huzuni wowote zaidi kwa Mungu, wala hakutaka Mungu kulia kwa ajili yake yeye, isitoshe hakutaka kumwona Mungu akiwa katika maumivu kwa sababu yake yeye. Wakati huu, Ayubu alitaka tu kujiondoa mwenyewe kwenye mwili wake, kuacha kuvumilia tena maumivu yaliyoletewa kwake kupitia kwa mwili wake, kwani kufanya hivi kungekomesha Mungu kuteseka kwa maumivu yake—lakini hakuweza kufanya hivyo, na alifaa kuvumilia tu maumivu ya mwili, na pia mateso ya kutotaka kumfanya Mungu kuwa na wasiwasi. Maumivu haya mawili—moja kutoka kwa mwili, na mengine kutoka kwa roho—yalileta maumivu makali ya moyoni, yakusokotesha tumbo kwake Ayubu, na kumfanya yeye kuhisi namna ambavyo mipaka ya binadamu aliye na mwili na damu inavyoweza kumfanya mtu kuhisi akiwa amedhalilishwa na asiye na njia ya kusaidika. Katika hali hizi, tamanio lake la Mungu lilizidi kukua, na chuki yake kwa Shetani ikazidi kuwa nyingi. Wakati huu, Ayubu angependelea kutowahi kuzaliwa kwenye ulimwengu huu wa binadamu, afadhali asingekuwepo badala ya kumuona Mungu Akilia au Akihisi maumivu kwa sababu yake. Alianza kuchukia kwa kina mwili wake, kuwa mgonjwa na mchovu ndani yake mwenyewe, siku yake ya kuzaliwa, na hata ya hayo yote ambayo yalikuwa yameunganishwa kwake. Hakutaka kuwepo na kutajwa kokote zaidi kuhusu siku yake ya kuzaliwa au chochote kilichohusu siku hiyo, na hivyo aliufunua mdomo wake na kuilaani siku yake ya kuzaliwa: “Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba. Siku ile iwe na kiza; Mungu na asiitazame kutoka juu, wala nuru iiangazie” (Ayubu 3:3-4). Maneno ya Ayubu yanaonyesha kuchukia kwake kwa nafsi yake mwenyewe, “Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba,” pamoja na yeye kujilaumu mwenyewe na kuwa katika hali ya kuhisi kwamba yuko katika hatia kwa kumsababishia Mungu maumivu, “Siku ile iwe na kiza; Mungu na asiitazame kutoka juu, wala nuru iiangazie.” Vifungu hivi viwili ni maonyesho ya namna Ayubu alivyohisi wakati huo, na vinaonyesha kikamilifu utimilifu wake na unyofu wake kwa wote. Wakati huohuo, kama vile tu Ayubu alivyokuwa ametaka, imani na utiifu wake kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, vyote viliinuliwa. Bila shaka, kuinuliwa huku kwa hakika ni athari ambayo Mungu Alikuwa Ametarajia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Ayubu (Sehemu 2)

Urazini wa Ayubu Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp