Onyo na Nuru Iliyotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu
Huku wakielewa mchakato ambao Mungu anampata kabisa mtu, watu wataweza pia kuelewa nia na umuhimu wa Mungu kumpeleka Ayubu kwa Shetani. Watu hawasumbuliwi tena na maumivu makali ya Ayubu, na wanatambua upya umuhimu wake. Hawawi na wasiwasi tena kuhusu kama wao wenyewe watapitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, na hawapingi tena au kukataa tena ujio wa majaribio ya Mungu. Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watakapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Ushuhuda wa Ayubu Wamliwaza Mungu
Nikiwaambia sasa kwamba Ayubu ni mtu mzuri, huenda msiweze kutambua maana iliyo katika maneno haya, na huenda msiweze kung’amua mawazo yaliyofanya Nizungumze maneno haya yote; lakini subirini mpaka siku ile mtakapokuwa mmepitia majaribu sawa na au yale yanayofanana na yale ambayo Ayubu alipitia, wakati mtakapokuwa mmepitia magumu, wakati mtakapokuwa mmepitia majaribu yaliyopangiliwa kwa ajili yenu na Mungu mwenyewe, wakati utakapojitolea kila kitu ulicho nacho, na kuvumilia udhalilishaji na ugumu ili uweze kumshinda Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu katikati ya vishawishi hivi vyote—basi utaweza kutambua maana ya maneno haya Ninayoyaongea. Wakati huo, utahisi kwamba wewe ni duni kuliko Ayubu, utahisi namna Ayubu alivyo mzuri na kwamba anastahili kuigwa; wakati huo utakapowadia, utatambua namna ambavyo maneno yale yaliyo bora yaliyozungumzwa na Ayubu yalivyo muhimu kwa yule aliyepotoka na anayeishi katika nyakati hizi, na utatambua namna ilivyo vigumu kwa watu wa leo kuweza kutimiza kile ambacho Ayubu alitimiza. Unapohisi kuwa ni vigumu, utatambua na kuona namna ambavyo moyo wa Mungu una dukuduku na wasiwasi, utatambua namna gharama aliyolipa Mungu kuwapata watu kama hao ilivyo ya juu, na jinsi kile ambacho Mungu hufanya na kutumia kwa ajili ya mwanadamu kilivyo cha thamani. Kwa sababu sasa mmeyasikia maneno haya, je, mnao ufahamu sahihi na ukadiriaji wa kweli kuhusu Ayubu? Machoni penu, je, Ayubu alikuwa kweli mtu mtimilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu? Nasadiki kwamba watu wengi bila shaka watasema ndiyo. Kwani ukweli kuhusu kile ambacho Ayubu alitenda na kufichua hakiwezi kupingwa na binadamu yeyote au Shetani. Hivyo ndivyo thibitisho la nguvu zaidi kuhusu ushindi wa Ayubu dhidi ya Shetani. Thibitisho hili lilitolewa katika Ayubu, na ndio ushuhuda wa kwanza uliopokelewa na Mungu. Hivyo, Ayubu aliposhinda vishawishi vya Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, Mungu aliona tumaini kwake Ayubu, na moyo wake uliliwazwa na Ayubu. Tangu wakati wa uumbaji mpaka wakati wa Ayubu, huu ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Mungu kwa kweli alipitia na kujua kuliwazwa kulikuwa nini, na kuliwazwa na mwanadamu kulimaanisha nini. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Alikuwa ameona, na kupata ushuhuda wa kweli uliotokana na Yeye.
Ninaamini kwamba, baada ya kuusikia ushuhuda wa Ayubu na simulizi za vipengele mbalimbali vya Ayubu, watu wengi watakuwa na mipango ya njia iliyo mbele yao. Hivyo, pia, Ninaamini kwamba watu wengi zaidi walio na wasiwasi na woga wataanza kwa utaratibu kuwa watulivu katika mwili na akili zao, na wataanza kuhisi tulizo, hatua kwa hatua …
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?