Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)

07/09/2019

a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu

Ayubu 2:3 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu.

Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani

Ayubu 2:4-5 Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.

c. Namna Ayubu Anavyoshughulikia Majaribio

Ayubu 2:9-10 Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe. Lakini yeye akasema kwake, Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya? Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake.

Ayubu 3:3 Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba.

Upendo wa Ayubu wa Njia ya Mungu Unazidi Yote Mengine

Maandiko yanarekodi maneno haya yaliyozungumzwa kati ya Mungu na Shetani: “Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu” (Ayubu 2:3). Katika maneno haya Mungu Anarudia swali moja kwa Shetani. Ni swali linalotuonyesha ukadiriaji wa uthibitisho wa Yehova Mungu kuhusu kile kilichoonyeshwa na kuishi na kudhihirishwa na Ayubu kwenye jaribio lake la kwanza, na ule ambao si tofauti na ukadiriaji wa Mungu wa Ayubu kabla ya kupitia jaribio lile la Shetani. Hivi ni kusema, kabla jaribio halijamfika, katika macho ya Mungu Ayubu alikuwa mtimilifu, na hivyo basi Mungu Alimlinda yeye na familia yake, na Akambariki, alistahili kubarikiwa kwa macho ya Mungu. Baada ya jaribio, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake kwa sababu alikuwa amepoteza mali yake na watoto wake, lakini aliendelea kulisifu jina la Yehova. Mwenendo wake halisi ulimfanya Mungu kumpongeza, na kumpa alama zote. Kwani machoni mwa Ayubu, watoto wake au rasilimali zake hazikutosha kumfanya yeye kumkataa Mungu. Nafasi ya Mungu katika moyo wake, kwa maneno mengine, isingeweza kusawazishwa na watoto wake au kipande chochote cha mali yake. Kwenye jaribio la kwanza la Ayubu, alimwonyesha Mungu kwamba upendo wake kwake na upendo wake wa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ulizidi kila kitu kingine. Ni kwa sababu tu jaribio hili lilimpa Ayubu uzoefu wa kupokea tuzo kutoka kwa Yehova Mungu na kufanya mali yake na watoto wake kuchukuliwa na Yeye.

Kwa Ayubu, hali hii aliyoipitia ilikuwa ya kweli na ambayo ilisafisha nafsi yake ikawa safi; ulikuwa ni ubatizo wa maisha uliotimiza uwepo wake, na, isitoshe, ilikuwa ni karamu ya kutosha iliyojaribu utiifu wake kwa, na yeye kumcha Mungu. Jaribio hili lilibadilisha hadhi ya Ayubu kutoka ule wa bwana tajiri hadi kwa mtu ambaye hakuwa na chochote, na pia likamruhusu kupitia dhuluma za shetani kwa wanadamu. Ufukara wake haukumfanya kuchukia Shetani; badala yake, kwenye vitendo vibovu vya Shetani aliuona ubaya na hali ya kudharau ya Shetani pamoja na uadui wa Shetani na uasi wake kwa Mungu, na hali hii ilimhimiza vizuri zaidi kushikilia daima njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Aliapa kwamba asingewahi kumwacha Mungu na kugeuka njia ya Mungu kwa sababu ya mambo ya nje kama vile mali, watoto au urithi, wala hangewahi kuwa mtumwa wa Shetani, mali, au mtu yeyote; mbali na Yehova Mungu, hakuna mtu ambaye angekuwa Bwana wake, au Mungu wake. Hayo ndiyo yaliyokuwa maazimio ya Ayubu. Kwa upande mwingine wa jaribio, Ayubu alikuwa pia amepata jambo jingine: Alikuwa amepata utajiri mkubwa katikati ya majaribio hayo aliyoyapitia kutoka kwa Mungu.

Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova na kupata baraka za Yehova Mungu kwake yeye. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, ndani ya moyo wake mara nyingi aliomba, akitumai angeweza kumlipa Mungu, akitumai kwamba angekuwa na fursa ya Kuwa na ushuhuda wa matendo na ukubwa wa Mungu, na kutumai kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vyote vingepata idhini ya Mungu. Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili vivi hivi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingetimia. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu wake na kumcha Mungu vyote vingeweza kutiwa kwenye majaribu, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu. Wakati wa jaribio, imani kama hiyo na kufuatilia huko kulimruhusu yeye kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimwaga sifa kubwa zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukubwa, na utakatifu wa Mungu. Wakati huu, ingawaje Ayubu alikuwa bado yuleyule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu kwenye macho ya Mungu, kuhusiana na yale aliyopitia, imani na maarifa ya Ayubu vyote vilikuwa vimeimarika pakubwa: Imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umeimarika pakubwa, na hali yake ya kumcha Mungu ilikuwa ya kina zaidi. Ingawaje jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakufanya maendeleo yake ya kwenda mbele kwenda polepole. Wakati huo, akiwa anapiga hesabu kile alichokuwa amepata kutoka kwenye jaribio hilo, na akitilia maanani upungufu wake binafsi, aliomba kimyakimya, akisubiri jaribio linalofuata ambalo lingemsibu yeye, kwa sababu alitamani sana, imani, utiifu, na kumcha Mungu kwake kuweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.

Mungu Anaziangalia fikira za ndani zaidi za binadamu na yale yote ambayo binadamu anasema na kufanya. Fikira za Ayubu zilifikia masikio ya Yehova Mungu, na Mungu alisikiliza maombi yake na kwa njia hii jaribio la Mungu kwa Ayubu lililofuata liliwasili kama lilivyotarajiwa.

Katikati ya Mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa kweli Utunzaji wa Mungu wa Wanadamu

Kufuatia maswali ya Yehova Mungu kwa Shetani, Shetani alifurahi kisirisiri. Kwa sababu Shetani alijua kwamba angeweza kwa mara nyingine kuruhusiwa kumshambulia mtu aliyekuwa mtimilifu katika macho ya Mungu—jambo ambalo kwa Shetani lilikuwa fursa ya nadra. Shetani alitaka kutumia fursa hii kudhalilisha kabisa kujitolea kwa Ayubu kumfanya kupoteza imani yake kwa Mungu na hivyo basi kutomcha Mungu tena au kubariki jina la Yehova. Hali hii ingempa Shetani fursa: Haijalishi ni wapi au ni muda gani, angeweza kumfanya Ayubu kuwa kikaragosi cha kufuata amri zake. Shetani alificha njama zake za maovu bila kuacha alama, lakini hakuweza kudhibiti asili yake ya maovu. Ukweli huu unaashiriwa kuhusu kupitia kwa majibu yake kwa maneno ya Yehova Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko. “Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako” (Ayubu 2:4-5). Haiwezekani kutopata maarifa makuu na hali ya kuonea kijicho ya Shetani kutokana na mabadilishano haya kati ya Mungu na Shetani. Baada ya kusikia uongo huu wa Shetani, wale wote wanaoupenda ukweli na kuchukia uovu bila shaka watakuwa na chuki kubwa zaidi kwa utwezo na kutokuwa na aibu kwa Shetani, watahisi wakiwa wametishika na kusinyika kutokana na uongo wa Shetani, na, wakati huohuo, watatoa maombi yao ya kina na heri zao za dhati kwa Ayubu, wakiomba kwamba binadamu huyu mwenye unyofu ataweza kutimiza utimilifu wake, wakitamani kwamba binadamu huyu anayemcha Mungu na kujiepusha na maovu aweze kushinda milele majaribio ya Shetani, na kuishi kwa mwangaza, na kuishi katikati ya mwongozo na baraka za Mungu, hivyo, pia ndivyo watakavyotaka matendo ya haki ya Ayubu yaweze milele kuenea na kuhimiza wale wanaofuatilia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Ingawaje nia ya kijicho ya Shetani inaweza kuonekana kupitia kwa tangazo hili, Mungu alikubali kwa urahisi “ombi” la Shetani—lakini alikuwa pia na sharti moja: “Yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake” (Ayubu 2:6). Kwa sababu, wakati huu, Shetani aliomba kunyosha mbele mkono wake ili kudhuru mwili na mifupa ya Ayubu, Mungu Alisema, “lakini okoa maisha yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba alimpa Shetani mwili wa Ayubu, lakini Akabakiza maisha yake. Shetani asingeweza kuyachukua maisha ya Ayubu, lakini isipokuwa haya angeweza kutumia njia au mbinu zozote dhidi ya Ayubu.

Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mungu, Shetani alimkimbilia Ayubu na kunyosha mbele mkono wake ili kuathiri ngozi yake na akamsababishia majipu mabaya yaliyoupiga mwili wake wote, naye Ayubu akahisi maumivu kwenye ngozi yake. Ayubu aliyasifu maajabu na utakatifu wa Yehova Mungu, jambo ambalo lilimfanya Shetani hata kuwa wazi zaidi katika ufidhuli wake. Kwa sababu alikuwa amehisi furaha ya kumwumiza binadamu, Shetani aliunyosha mkono wake na akakwaruza nyama ya Ayubu, na kusababisha majipu yake mabaya kutunga usaha. Mara moja Ayubu alihisi maumivu na mateso kwenye mwili wake ambayo hayakuwa na kifani, na asingeweza kujisaidia kwa vyovyote vile isipokuwa kujikanda yeye mwenyewe kutoka kwenye kichwa hadi miguu akitumia mikono yake, ni kana kwamba kufanya hivi kungetuliza balaa ile iliyofanyikia roho yake kutokana na maumivu haya ya nyama za mwili wake. Alitambua kwamba Mungu Alikuwa kando yake akimwangalia, na akajaribu kwa njia bora zaidi kujituliza. Kwa mara nyingine alipiga magoti kwenye ardhi, na kusema: Unaangalia ndani ya binadamu, unauona umaskini wake; kwa nini unyonge wake unakuhusu wewe? Jina la Yehova Mungu lisifiwe. Shetani aliyaona yale maumivu yasiyovumilika ya Ayubu, lakini hakumwona Ayubu akiliacha neno la Yehova Mungu. Hivyo aliunyoosha mkono wake haraka mbele ili kudhuru mifupa ya Ayubu, akiwa na tamaa ya kudhuru kila kiungo cha mwili wake. Mara, Ayubu akahisi mateso asiyoyatarajia; ni kana kwamba mwili wake ulikuwa umepasuliwa katikati kutoka kwenye mifupa, na kana kwamba mifupa yake ilikuwa ikipasuliwa kipande hadi kipande. Mateso haya ya kuumiza yalimfanya akafikiria afadhali basi afe.… uwezo wake wa kuvumilia ulikuwa umefikia kilele.… Alitaka kulia kwa sauti, alitaka kuirarua ngozi kwenye mwili wake ili kupunguza maumivu—lakini alishikilia mayowe yake, na hakuirarua ngozi yake kutoka kwenye mwili wake, kwani hakutaka Shetani auone udhaifu wake. Na hivyo alipiga magoti chini kwa mara nyingine, lakini wakati huu hakuhisi uwepo wa Yehova Mungu. Alijua kwamba mara nyingi alikuwa mbele yake, na nyuma yake, na upande wake. Lakini kwenye maumivu haya, Mungu alikuwa hajawahi kuyatazama; Aliufunika uso wake na Akawa Amefichwa, kwa maana uumbaji wake wa binadamu haukuwa wa kumletea mateso binadamu. Wakati huu, Ayubu alikuwa akilia, na akijaribu kwa njia bora zaidi kuvumilia maumivu yake ya kimwili, lakini asingeweza kujizuia tena dhidi ya kutoa shukrani kwa Mungu: Binadamu aanguka kwa mpigo wa kwanza, yeye ni myonge na asiye na nguvu, yeye ni mchanga na asiyejua—kwa nini ukataka kumtunza na kuwa mzuri kwake yeye? Unanipiga, ilhali inakuumiza kufanya hivyo. Ni nini cha binadamu kinastahili utunzaji na kujali Kwako? Maombi ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu, na ya Mungu Alikuwa kimya, Akitazama tu bila kutoa sauti.… Akiwa amejaribu kila ujanja kwenye kitabu bila mafanikio, Shetani aliondoka kimyakimya, lakini haya hayakufikisha hadi tamati majaribio ya Ayubu kutoka kwa Mungu. Kwa sababu nguvu za Mungu zilizokuwa zimefichuliwa ndani ya Ayubu zilikuwa hazijajulikana kwa umma, hadithi ya Ayubu haikuishia pale ambapo Shetani alijiondoa. Huku wahusika wengine wakiingia katika tukio hilo, matukio mengine ya ajabu zaidi yalikuwa yaje.

Maonyesho Mengine ya Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kutukuza Kwake Jina la Mungu Katika Mambo Yote

Ayubu alikuwa ameteseka kutokana na maudhi ya Shetani, lakini bado hakuliacha jina la Yehova Mungu. Mke wake ndiye aliyekuwa wa kwanza kujiondoa na kuendeleza wajibu wa Shetani unaoweza kuonekana kwa kumshambulia Ayubu. Maandishi asilia yanafafanua hali hii hivyo basi: “Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe” (Ayubu2:9). Haya yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Shetani akisingizia kuwa binadamu. Yalikuwa ni shambulizi, na shtaka, pamoja na kichocheo, jaribio, na matusi. Baada ya kushindwa kushambulia mwili wa Ayubu, Shetani sasa alishambulia moja kwa moja uadilifu wa Ayubu, akitaka kutumia jambo hili kumfanya Ayubu kutupilia mbali uadilifu wake, kumwacha Mungu, na asiendelee kuishi tena. Hivyo, pia, ndivyo Shetani alivyotaka kutumia maneno kama hayo kumjaribu Ayubu: Kama Ayubu angeacha jina la Yehova, kisha asingelazimika kuvumilia mateso kama hayo; yeye angejiondolea mateso ya mwili. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu alimkosoa kwa kusema, “Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:10). Ayubu alikuwa amejua kwa muda mrefu maneno haya, lakini wakati huu ukweli wa maarifa ya Ayubu kuhusu maneno haya ulikuwa umethibitishwa.

Wakati mke wake alimshauri kulaani Mungu na kufa, maana yake ilikuwa: “Mungu wako anakushughulikia hivi, kwa hivyo kwa nini usimlaani yeye? Kama ungali hai unafanya nini? Mungu wako hakufanyii haki, na ilhali ungali unasema ‘libarikiwe jina la Yehova’. Angekuleteaje janga hili huku unabariki jina Lake? Harakisha na uliache jina la Mungu, na usimfuate yeye tena. Kisha, matatizo yako yataisha.” Kwa wakati huu, ushuhuda ulitolewa ambao Mungu alitaka kuuona kwa Ayubu. Hakuna mtu yeyote wa kawaida ambaye angeweza kuwa na ushuhuda huu, wala hatuusomi katika mojawapo ya hadithi za Biblia—lakini Mungu Alikuwa ameuona kabla hata Ayubu kuongea maneno haya. Mungu Alitaka tu kutumia fursa hii kumruhusu Ayubu kuthibitisha kwa wote kwamba Mungu alikuwa sahihi. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu hakutupilia tu mbali uadilifu wake au kumuacha Mungu, bali pia alimwambia mke wake: “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Je, maneno haya yanao uzito mkuu? Hapa, kunayo ukweli mmoja tu unaoweza kuthibitisha uzito wa maneno haya. Uzito wa maneno haya ni kwamba yameidhinishwa na Mungu ndani ya moyo Wake, ndiyo yale yaliyotamaniwa na Mungu, ndiyo yale Mungu Alitaka kusikia, na ndiyo matokeo ambayo Mungu Alitamani kuona; maneno haya ndiyo pia kiini cha ushuhuda wa Ayubu. Katika haya, utimilifu, unyofu, kumcha Mungu, kujiepusha na maovu kwa Ayubu kulithibitishwa. Thamani ya Ayubu ilikuwa namna ambavyo, alipojaribiwa, na hata wakati mwili wake mzima ulikuwa umefunikwa na majipu mabaya, alipovumilia mateso ya kiwango cha juu zaidi, na wakati mke na watu wake wa ukoo walipomshauri, bado aliyatamka maneno hayo. Ili niweze kuiweka kwa njia nyingine, ndani ya moyo wake alisadiki kwamba, haijalishi ni kiasi kipi cha majaribio, au ni vipi ambavyo masaibu au mateso yalivyokuwa, hata kama kifo kingemjia, hangemuacha Mungu au kugeuka na kuacha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Unaona, basi, kwamba Mungu Alishikilia sehemu muhimu sana ndani ya moyo wake, na kwamba kulikuwa tu na Mungu moyoni mwake. Ni kwa sababu ya haya ndipo tunasoma ufafanuzi kama huo kuhusu yeye katika maandiko kama: Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi na midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp