Shetani Anamjaribu Ayubu kwa Mara ya Kwanza (Mifugo Yake Yaibiwa na Janga Lawapata Watoto Wake)

07/09/2019

a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu

Ayubu 1:8 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?

Ayubu 1:12 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, vyote ambavyo anavyo vimo uwezoni mwako; lakini juu yake mwenyewe wewe usinyoshe mkono wako. Hivyo basi Shetani akaondoka mbele za uwepo wa Yehova.

b. Jibu la Shetani

Ayubu 1:9-11 Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.

Mungu Amruhusu Shetani Kumjaribu Ayubu ili Imani ya Ayubu iweze Kufanywa Kuwa Timilifu

Ayubu 1:8 ndiyo rekodi ya kwanza tunayoiona kwenye Biblia kuhusu mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Na ni nini alichosema Mungu? Maandishi asilia yanatupatia simulizi ifuatayo: “Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?” Huu ulikuwa ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu kwa Shetani; Mungu alisema kwamba alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kabla ya maneno haya kati ya Mungu na Shetani, Mungu alikuwa ameamua kwamba Angemtumia Shetani kujaribu Ayubu—kwamba Angemkabidhi Ayubu kwa Shetani. Kwa mkondo mmoja, hali hii ingethibitisha kwamba uangalizi na utathmini wa Mungu kwa Ayubu ulikuwa sahihi na bila kosa, na ungesababisha Shetani kuaibishwa kupitia kwa ushuhuda wa Ayubu, kwa mkondo mwingine, ingefanya imani ya Ayubu kwa Mungu na kumcha Mungu kuwa timilifu. Hivyo, wakati Shetani alipokuja mbele ya Mungu, Mungu hakutatiza maneno. Alienda moja kwa moja kwenye hoja na kumuuliza Shetani: “Je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?” Katika swali la Mungu kunayo maana ifuatayo: Mungu alijua kwamba Shetani alizunguka kila pahali, na mara nyingi alikuwa amemnyemelea Ayubu, aliyekuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa mara nyingi amemjaribu na kumshambulia, akijaribu kupata njia ya kumwangamiza Ayubu ili kuthibitisha kwamba imani ya Ayubu katika Mungu na kumcha Mungu kwake kusingeweza kubadilika. Shetani pia alitafuta kwa haraka sana fursa za kumhangaisha Ayubu, ili Ayubu aweze kumkataa Mungu, na kwamba aweze kumpokonya kutoka katika mikono ya Mungu. Lakini Mungu aliuangalia moyo wa Ayubu na kuona kwamba alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alitumia swali moja kumwambia Shetani kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwamba Ayubu asingeweza kumwacha Mungu na kufuata Shetani. Baada ya kusikia utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu, ndani ya Shetani kukatokea hasira kali iliyotokana na udhalilishaji, na akawa mwenye hasira zaidi, na aliyekosa subira ya kumpokonya Ayubu kutoka kwa Mungu, kwani Shetani alikuwa hajawahi kusadiki kwamba mtu angeweza kuwa mtimilifu na mnyofu, au kwamba angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Wakati huohuo, Shetani pia alichukizwa na utimilifu na unyofu kwa binadamu, na aliwachukia watu ambao wangeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Na hivyo imeandikwa katika Ayubu 1:9-11 kwamba “Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.” Mungu alikuwa amezoea kwa undani asili ya kijicho ya Shetani, na Alijua vizuri kabisa kwamba Shetani alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kumwangamiza Ayubu, na hivyo kwa haya Mungu alitaka, kwa kumwambia Shetani kwa mara nyingine kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimwogopa Mungu na kujiepusha na maovu, kumrudisha Shetani pale anapofaa, kumfanya Shetani kufichua uso wake wa kweli na kumshambulia na kumjaribu Ayubu. Kwa maneno mengine, Mungu alitilia mkazo makusudi kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kwa njia hii alimfanya Shetani kumshambulia Ayubu kwa sababu ya chuki na hasira za Shetani kutokana na vile ambavyo Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kutokana na haya, Mungu angemletea Shetani aibu kupitia kwa ukweli kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, na Shetani angeachwa akiwa amedhalilishwa kabisa na kushindwa. Baada ya hapo, Shetani asingekuwa tena na shaka au asingetoa mashtaka kuhusu utimilifu, unyofu, ucha Mungu au hali ya kujiepusha na maovu ya Ayubu. Kwa njia hii, majaribio ya Mungu na yale ya Shetani yalikuwa karibu yasiyoepukika. Yule tu aliye na uwezo wa kustahimili majaribio ya Mungu na yale ya Shetani alikuwa ni Ayubu. Kufuatia mabadilishano haya, Shetani alipewa ruhusa kumjaribu Ayubu. Na hivyo raundi ya kwanza ya mashambulizi ya Shetani ikaanza. Kilengwa cha mashambulizi haya kilikuwa mali ya Ayubu, kwani Shetani alikuwa ametoa mashtaka yafuatayo dhidi ya Ayubu: “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? … Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini.” Kutokana na haya, Mungu alimruhusu Shetani kuchukua kila kitu ambacho Ayubu alikuwa nacho—ambalo ndilo lilikuwa kusudio lenyewe la Mungu kuzungumza na Shetani. Hata hivyo, Mungu alitoa sharti moja kwa Shetani: “Vyote ambavyo anavyo vimo uwezoni mwako; lakini juu yake mwenyewe wewe usinyoshe mkono wako” (Ayubu 1:12). Hili ndilo sharti ambalo Mungu alitoa baada ya kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu na akamweka Ayubu kwenye mikono ya Shetani, na hiyo ndiyo mipaka aliyomwekea Shetani: Alimwamuru Shetani kutodhuru Ayubu. Kwa sababu Mungu alijua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba Alikuwa na imani kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu kwake Yeye ulikuwa zaidi ya kutiliwa shaka, na kwamba angeweza kustahimili majaribio; hivyo, Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, lakini akaweka hapo kizuizi kwa Shetani: Shetani aliruhusiwa kuchukua mali ya Ayubu yote, lakini asimguse hata kwa kidole. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba Mungu hakumkabidhi Ayubu kabisa kwa Shetani wakati huo. Shetani angeweza kumjaribu Ayubu kwa mbinu zozote zile ambazo alitaka, lakini hakuweza kumdhuru Ayubu mwenyewe, hata unywele mmoja wa kichwa chake, kwa sababu kila kitu cha binadamu kinathibitiwa na Mungu, iwapo binadamu anaishi ama anakufa inaamuliwa na Mungu na Shetani hana leseni yoyote ya kuthibiti haya. Baada ya Mungu kumwambia Shetani maneno haya, Shetani asingeweza kusubiri kuanza. Alitumia kila mbinu kumjaribu Ayubu, na baada ya muda usiyokuwa mrefu Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng’ombe na mali yote aliyokuwa amepewa na Mungu…. Na hivyo majaribio ya Mungu yakamjia yeye.

Ingawa Biblia inatuambia asili ya jaribio la Ayubu, je Ayubu mwenyewe, ambaye alipatwa na majaribio haya, alijua kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea? Ayubu alikuwa tu binadamu wa kawaida; bila shaka hakujua chochote kuhusu hadithi ile iliyokuwa ikiendelea nyuma yake. Hata hivyo, kumcha Mungu kwake na utimilifu pamoja na unyofu wake, ulimfanya kutambua kwamba majaribio ya Mungu yalikuwa yamemjia. Hakujua ni nini kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme wa kiroho, wala nia alizokuwa nazo Mungu katika majaribio hayo. Lakini alijua kwamba haijalishi ni nini ambacho kingemfanyikia yeye, alifaa kuendelea kushikilia ukweli wa utimilifu na unyofu wake, na kwamba alifaa kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mwelekeo na mwitikio wa Ayubu katika masuala haya uliweza kutazamwa waziwazi na Mungu. Naye Mungu aliona nini? Aliuona moyo wa Ayubu uliyomcha Mungu, kwa sababu kutoka mwanzo hadi wakati ambapo Ayubu alijaribiwa, moyo wa Ayubu ulibakia wazi kwa Mungu, uliwekwa mbele ya Mungu, naye Ayubu hakuwacha utimilifu wala unyofu wake, wala hakutupilia mbali au kugeuka katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—na hakuna kingine chochote kilichokuwa cha kumtosheleza na kumfurahisha Mungu kama haya. Kisha, tutaangalia ni majaribio yapi aliyoyapitia Ayubu na ni vipi ambavyo aliyashughulikia majaribio haya. Hebu tuyasome maandiko.

Shetani Anamjaribu Ayubu kwa Mara ya Kwanza (Mifugo Yake Yaibiwa na Janga Lawapata Watoto Wake)

c. Mwitikio wa Ayubu

Ayubu 1:20-21 Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Naye akasema, Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi; Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.

Kwamba Ayubu Anajiwajibikia Yeye Mwenyewe Kurudisha Vyote Anavyomiliki Kunatokana na Kumcha Kwake Mungu

Baada ya Mungu kumwambia Shetani, “Vyote ambavyo anavyo vimo uwezoni mwako; lakini juu yake mwenyewe wewe usinyoshe mkono wako.” Shetani aliondoka, muda mfupi baadaye Ayubu alipata mashambulizi ya ghafla na makali: Kwanza, ng’ombe na punda wake waliibwa na watumishi wake kuuwawa; kisha, kondoo na watumishi wake waliteketezwa hadi kiwango cha kuangamia; baada ya hapo ngamia wake walichukuliwa na watumishi wake wakauliwa; hatimaye watoto wake wa kiume na wa kike waliaga dunia. Msururu huu wa mashambulizi ulikuwa ni mateso ambayo alipitia Ayubu kwenye jaribio hili la kwanza. Kama alivyoamrishwa na Mungu, kwenye kipindi hiki cha mashambulizi, Shetani alilenga tu mali ya Ayubu na watoto wake, na hakumdhuru Ayubu mwenyewe. Hata hivyo, Ayubu alibadilishwa papo hapo kutoka kuwa mtu tajiri aliyemiliki utajiri mwingi hadi kuwa mtu asiye na chochote wala lolote. Hakuna yeyote ambaye angestahimili mshangao huu mkubwa au ambaye angeitikia vizuri, ilhali Ayubu aliuonyesha upande wake usio wa kawaida. Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” Huu ndio uliokuwa mwitikio wa kwanza wa Ayubu baada ya kusikia kwamba watoto wake walikuwa wameaga dunia na alikuwa amepoteza mali yake yote. Zaidi ya yote, hakuonekana ni kana kwamba ameshangazwa, au amepigwa na butwaa chakari, isitoshe hakuonyesha hasira au chuki. Unaona, basi, kwamba moyoni mwake alikuwa tayari ametambua kuwa majanga haya hayakuwa ajali, au yalitokana na mkono wa binadamu, na wala hayakuwa kuwasili kwa kuadhibiwa au adhabu. Badala yake, majaribio ya Yehova yalikuwa yamemjia yeye; alikuwa ni Yehova ambaye alitaka kuchukua mali na watoto wake. Ayubu alikuwa mtulivu na mwenye kuelewa haraka wakati huo. Ubinadamu wake wa utimilifu na unyofu ulimwezesha yeye kuweza kufanya uamuzi na uamuzi kwa usahihi kwa njia ya kiasili na kirazini hasa, kuhusu majanga yaliyokuwa yamemsibu, na matokeo yake ni kuwa, alijiendeleza kwa utulivu usio wa kawaida. “Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” “Akalipasua joho lake” inamaanisha kwamba alikuwa hana nguo, na hakumiliki chochote; “akanyoa kichwa chake” inamaanishwa kwamba alikuwa amerudi mbele ya Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa; “akaanguka chini, na kuabudu” inamaanisha alikuwa amekuja ulimwenguni akiwa uchi, na bado hakuwa na chochote leo, alirudishwa kwa Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa. Mwelekeo wa Ayubu kwa yote yaliyompata usingeweza kutimizwa na kiumbe yeyote wa Mungu. Imani yake kwa Yehova ilizidi ile ufalme wa imani; huku kulikuwa ni kumcha Mungu kwake, kuwa mtiifu kwa Mungu, na hakuweza tu kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa yeye lakini pia kuchukua kutoka kwake. Na zaidi ya hayo, aliweza kujiwajibikia yeye mwenyewe ili kurudisha yale yote aliyomiliki, pamoja na maisha yake.

Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa wanadamu, na utimilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawaje hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu, na kutokana na kumcha Mungu kwake, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu uhuru wa kuchukua chochote alichokuwa nacho, ilhali hakulalamika, na akaanguka chini mbele ya Mungu na kumwambia kwamba kwa wakati huohuo, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake timilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na upole wake, Ayubu hakutikisika katika utambuzi wake na uzoefu wa uwepo wa Mungu na juu ya msingi huu aliweza kujitolea madai yeye mwenyewe na kuwastanisha kufikiria kwake, tabia, mwenendo, na kanuni za vitendo mbele ya Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake yeye na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa ameviona miongoni mwa mambo mengine yote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia. Ayubu aliumiliki ubinadamu wa uaminifu, usio na hatia, na wa upole, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kushuhudia katikati ya mashambulizi mabaya kama yale yaliyomsibu kutoka kwa Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kutosheleza kwake Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia. Ingawaje mwenendo wa Ayubu kwenye jaribio la kwanza ulikuwa wa moja kwa moja, vizazi vya baadaye havikuwa na uhakika wa kutimiza hali hiyo ya moja kwa moja hata baada ya kutia bidii maisha yao yote, wala hawangemiliki kwa vyovyote vile mwenendo wa Ayubu uliofafanuliwa hapo juu. Leo, wakikabiliwa na mwenendo wa moja kwa moja wa Ayubu, na katika kuulinganisha na kilio na bidii ya “utiifu wenye hakika na uaminifu hadi kifo” ulioonyeshwa kwa Mungu na wale wanaodai kusadiki Mungu na kufuata Mungu, je mnahisi aibu kwa kina au la?

Wakati unasoma maandiko kuhusu yale mateso yote aliyopitia Ayubu na familia yake, mwitikio wako ni upi? Unapotea kwenye fikira zako? Unashangazwa? Je, majaribio haya yaliyomsibu Ayubu yanaweza kufafanuliwa kama ya “kusikitisha”? Kwa maneno mengine, inatisha vya kutosha kuyasoma majaribio ya Ayubu kama yalivyofafanuliwa kwenye maandiko, kutosema chochote kuhusu vile yangekuwa katika uhalisia. Unaona, basi, kwamba kile kilichomsibu Ayubu hakikuwa “mazoezi,” lakini “vita,” halisi vikiwa na “bunduki” na “risasi” za kweli. Lakini nani alisababisha yeye kuweza kupitia majaribio haya? Yaliweza, bila shaka, kutekelezwa na Shetani, yalitekelezwa na Shetani mwenyewe—lakini yaliidhinishwa na Mungu. Je, Mungu alimwambia Shetani kumjaribu Ayubu kwa njia gani? Hakumwambia. Mungu alimpa Shetani sharti moja tu, na baadaye jaribio hilo likamjia Ayubu. Wakati jaribio lilimjia Ayubu, liliwapatia watu hisia ya maovu na ubaya wa Shetani, ya uoneaji kijicho wake, na uchukivu wake kwa binadamu, na uadui wake kwa Mungu. Katika haya tunaona kwamba maneno yasingeweza kufafanua namna tu ambavyo jaribio hili lilikuwa la kikatili. Inaweza kusemekana kwamba asili ya kijicho ambayo Shetani alimnyanyasa binadamu, na uso wake mbaya, vyote vilichuliwa kabisa kwa wakati huu. Shetani alitumia fursa hii, fursa iliyotolewa kupitia kwa ruhusa ya Mungu, kumnyanyasa Ayubu kwa njia mbaya na ya kusikitisha, mbinu na kiwango cha ukatili ambao haufikiriki na hauvumiliki kabisa na watu wa leo. Badala ya kusema kwamba Ayubu alijaribiwa na Shetani, na kwamba alisimama imara katika ushuhuda wake wakati wa jaribio hili, ni bora zaidi kusema kwamba katika majaribio hayo yaliyokuwa mbele yake kutoka kwa Mungu, Ayubu alianza kuwa katika mapambano na Shetani ili kuulinda utimilifu na unyofu wake, kutetea njia yake ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika shindano hili, Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng’ombe, alipoteza mali yake yote na watoto wake wa kike na kiume—lakini hakuacha utimilifu, unyofu, au hali yake ya kumcha Mungu. Kwa maneno mengine, katika pigano hili na Shetani alipendelea kunyang’anywa mali na watoto kuliko kupoteza utimilifu, unyofu na hali yake ya kumcha Mungu. Alipendelea kushikilia mzizi wa maana ya kuwa binadamu. Maandiko yanatoa simulizi halisi kuhusu mchakato wote ambao Ayubu alipoteza rasilimali zake, na pia ukasimulia mwenendo na mwelekeo wa Ayubu. Simulizi hizi za mkato, na wazi zinatoa hisia kwamba Ayubu alikuwa karibu anao utulivu wakati akipitia jaribio hili, lakini kama kile kilichofanyika kwa hakika kingeundwa upya, na kuongeza asili yale ya kijicho ya Shetani—basi mambo yasingekuwa rahisi au mepesi kama yalivyofafanuliwa kwenye sentensi hizi. Uhalisia ulikuwa wenye ukatili zaidi. Hicho ndicho kiwango cha uharibifu na chuki ambacho Shetani hushughulikia wanadamu na wale wote wanaoidhinishwa na Mungu. Kama Mungu asingekuwa amemwomba Shetani kutodhuru Ayubu, Shetani bila shaka angekuwa amemwua bila ya shaka. Shetani hataki mtu yeyote kumwabudu Mungu, wala hataki wale wenye haki mbele ya macho ya Mungu na wale walio timilifu na wanyofu kuweza kuendelea kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa watu kumcha Mungu na kujiepusha maovu kunamaanisha kwamba wanajiepusha na kumwacha Shetani, na hivyo Shetani alitumia ruhusa ya Mungu kumlimbikizia hasira yake na chuki kwake Ayubu bila huruma. Unaona, basi, mateso aliyoyapitia Ayubu yalikuwa mengi sana, haya yalikuwa mengi kiasi gani ambayo Ayubu alipitia, kuanzia kwenye akili hadi kwenye mwili, kutoka nje hadi ndani. Leo, hatuoni namna ambavyo kwa wakati huu na tunaweza tu kupata kutoka kwenye simulizi za Biblia, mtazamo mfupi wa hisia za Ayubu wakati alipokuwa akipitia yale mateso wakati huo.

Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, Aliweza kujuta ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, La, Asingefanya hivyo. Kwani Yeye alisadiki kwa dhati kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani tu fursa ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua maovu yake Shetani na hali ya kudharauliwa kwake binafsi. Ilikuwa, zaidi ya hapo, fursa ya Ayubu kutolea ushuhuda utakatifu wake na kumcha Mungu kwake na kujiepusha na maovu mbele ya watu wa ulimwengu, Shetani, na hata wale wanaomfuata Mungu. Je, matokeo ya mwisho yalithibitisha kwamba ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu ulikuwa sahihi na bila makosa? Je, Ayubu alimshinda kweli Shetani? Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.” Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.” Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. Yalikuwa maneno haya ya kawaida yaliyomfanya Shetani kuogopa, yaliyoleta aibu kwake na kumsababisha kutoroka kwa wasiwasi, na, vilevile, yaliyomfunga pingu Shetani na kumuacha bila rasilimali zozote. Hivyo, pia, ndivyo maneno haya yalivyomfanya Shetani kuhisi matendo ya kustaajabisha na yenye nguvu ya Yehova Mungu, na kumruhusu kuelewa haiba kubwa na isiyo ya kawaida ya yule ambaye moyo wake ulitawaliwa na njia ya Mungu. Zaidi, yalionyesha Shetani nguvu za kipekee zilizoonyeshwa na mtu mdogo asiyekuwa na umuhimu wowote katika kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu Shetani hivyo basi alishindwa kwenye shindano la kwanza. Licha ya utambuzi wake “uliopatikana kwa hali ngumu,” Shetani hakuwa na nia ya kumwachilia Ayubu, wala hakukuwa na badiliko lolote katika asili yake ya unafiki. Shetani alijaribu kuendelea kumshambulia Ayubu, na kwa mara nyingine tena akamjia Mungu …

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp