Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ayubu Abariki Jina la Mungu na Hafikirii Baraka au Janga

2

Kunao ukweli ambao haurejelewi katu kwenye hadithi za maandiko kuhusu Ayubu, ambayo ndio itakayokuwa zingatio letu leo. Ingawaje Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Na mwelekeo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “jina la Yehova libarikiwe.” Baraka yake kwa jina la Mungu haikuwa ya masharti, wala isiyofuzu, na bila ya sababu. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, na kuuruhusu kudhibitiwa na Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopangilia katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kuzuia Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kuuliza Mungu kumfanyia chochote au kumpa chochote yeye, na wala hakuwa na matamanio yasiyo ya kawaida ambayo angepata chochote kutoka kwa kumwabudu Mungu. Ayubu hakuzungumzia biashara na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Hali yake ya kusifia jina la Mungu ilikuwa kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala mambo yote, na haikutegemea kama alipata baraka au alipigwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au analeta janga kwao, mamlaka na nguvu vyote havitabadilika, na hivyo, haikujalisha hali za mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na wakati janga lilipompata binadamu, hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu cha binadamu; matukio yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu, na licha ya maoni yake mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu alipitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu vyote vilifikia masikio ya Mungu na vikawasili mbele ya Mungu, na vikaonekana kuwa muhimu na Mungu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akathamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na pahali pote, na haijalishi ni muda au mahali gani palipokaribisha chochote kile kilichomsibu. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake kilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu alisadiki hili kuwa wajibu wake, na ndio hasa kile ambacho Mungu Alitaka. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu wala kumsikiliza Akiongea mambo yoyote, akitoa amri zozote, akiyatoa mafundisho yoyote, au kuelekeza yeye kuhusu chochote. Kwa maneno ya leo, kwake yeye kuweza kumiliki mwelekeo kama huo kwa Mungu, wakati Mungu alikuwa hajampa nuru, mwongozo, au toleo kuhusiana na ukweli—hili lilikuwa lenye thamani sana, na kwake yeye kuonyesha mambo kama hayo kulitosha kwa Mungu, na ushuhuda wake ulipongezwa na Mungu, na kutunzwa na Mungu. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake yeye, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele ya Mungu waliweza tu kuongea kuhusu nadharia kuu, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwani moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Binadamu kama huyu pekee aliyemiliki moyo kama huo na ubinadamu ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Binadamu kama huyo angeona ukuu wa Mungu, angeona mamlaka na nguvu Yake, na angeweza kutimiza utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio. Binadamu tu kama huyo ndiye angeweza kusifu jina la Mungu kwa kweli. Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki yeye au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya ujinga, kutojua, na kutoweza kufikiria vyema, kuwa na shaka katika ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, na ya kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Hivyo basi, Ayubu alikuwa na maarifa makubwa ya kinadharia kumhusu Mungu kuliko ninyi? Kwa sababu kazi na matamko ya Mungu wakati huo yalikuwa machache, halikuwa jambo rahisi kutimiza maarifa ya Mungu. Mafanikio kama hayo ya Ayubu hayakukuwa jambo dogo. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala kuwahi kusikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mwelekeo kama huo kwa Mungu yalikuwa ni hasa matokeo yaliyoonyesha ubinadamu wake na ufuatiliaji wake wa kibinafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao haujamilikiwa na watu leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “hakuna mtu ambaye yuko kama yeye ulimwenguni, mtu aliye kamili na mwaminifu.” Katika enzi hiyo, Mungu alikuwa tayari amefanya ukadiriaji wake Ayubu, na alikuwa amefikia hitimisho fulani. Ungekuwa ukweli zaidi kwa kiasi kipi hii leo?

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Maudhui Yanayohusiana