Kumjua Mungu ni nini hasa? Kuwa kwa ufahamu wa Biblia na nadharia ya teolojia unaweza kuchukuliwa kama kumjua Mungu?

23/09/2018

Maneno Husika ya Mungu:

Kumjua Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha kwamba mwanadamu anajua shangwe, hasira, huzuni na furaha ya Mungu; huku ndiko kumjua Mungu. Unasema kwamba umemwona Mungu, ilhali huelewi shangwe, hasira, huzuni, na furaha ya Mungu, huelewi tabia Yake, wala huelewi haki Yake. Huna ufahamu wa rehema Zake, na hujui Anachokipenda ama Anachokichukia. Huu si ufahamu wa Mungu. Kwa hivyo, watu wengine wanaweza kumfuata Mungu, lakini sio lazima kwamba wanaweza kumwamini kwa ari: hii ndiyo tofauti. Ikiwa unamjua, unamwelewa, na unaweza kuelewa mapenzi Yake kiasi, basi unaweza kumwamini kwa kweli, kumtii kwa kweli, kumpenda kwa kweli, na kumwabudu Yeye kwa kweli. Ikiwa huelewi mambo haya, basi unafuata tu, mtu fulani anayefuata tu na kufuata umati. Hiyo haiwezi kuitwa kutii kwa kweli au ibada ya kweli. Je! Ibada ya kweli inafanyika vipi? Hakuna wowote wanaomjua Mungu na kumwona Mungu kwa kweli ambao hawamwabudu Yeye, ambao hawamheshimu. Wote lazima wasujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, kadri watu wanavyokuwa na ufahamu wa tabia ya Mungu mwenye mwili na wa kile Alicho nacho na kile Alicho, ndivyo wanavyovithamini zaidi na kumcha Yeye. Kwa kawaida, ufahamu mdogo unamaanisha kutokuwa makini zaidi, na kwamba Mungu anachukuliwa kama mwanadamu. Ikiwa watu wanamjua Mungu na kumwona kweli, watatetemeka kwa hofu. Kwa nini Yohana alisema, “Yeye anayekuja baada ya mimi ni mwenye nguvu kuniliko, ambaye mimi si wa kufaa kubeba viatu vyake”? Ijapokuwa ufahamu wa ndani ya moyo wake haukuwa wa kina kirefu sana, lakini alijua kwamba Mungu ni wa ajabu. Ni watu wangapi wanaoweza kumcha Mungu sasa? Bila kuijua tabia Yake, mtu anawezaje kumheshimu? Ikiwa watu hawajui kiini cha Kristo na hawaelewi tabia ya Mungu, hawawezi hata kumwabudu Mungu wa vitendo kwa kweli. Ikiwa watu wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo na hawajui asili Yake, ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona kuwa sahihi na kuchukulia neno Lake kama yasiyo na maana, wahodhi mawazo kumhusu Mungu, na kumshutumu na kumkufuru. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini cha Kristo, uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile waumini wote wanaoamini katika Mungu wa utendaji wanapaswa kuingia na kufanikisha.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ukitaka kumjua Mungu wa vitendo, lazima kimsingi ujue jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi katika ubinadamu na katika uungu; hili, wakati ule ule, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote hujihusisha nayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. … Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kuyajua matendo ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote—haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya yana uhusiano wa moja kwa moja na iwapo watu wanaweza kuingia kwa uhalisi wa ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba yule Mungu unayemwamini si Mungu Mwenyewe wa kweli kabisa, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini ni Mungu wa fikira tu, si Mungu wa kweli. Hii ni kwa sababu Mungu wa kweli ni Yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote.

Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaongoza binadamu wote kwa njia ya utawala Wake wa vitu vyote, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa Anayejumuisha yote na mwenye wingi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na utele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyoshawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Yeye Mwenyewe Aeleze na kumfungulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? Kuleta mambo ya zamani leo kunayafanya yawe historia, haijalishi yana ukweli kiasi gani, bado ni historia—na historia haiwezi kushughulikia masuala ya leo. Maana Mungu haangalii historia! Na hivyo, kama unaelewa tu Biblia, na huelewi chochote kuhusu kazi ambayo Mungu anakusudia kufanya leo, na kama unamwamini Mungu, na hutafuti kazi ya Roho Mtakatifu, basi hujui inamaanisha nini kumtafuta Mungu. Ikiwa unasoma Biblia kwa lengo la kujifunza historia ya Israeli, kutafiti historia ya uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia, basi humwamini Mungu. Lakini leo, kwa kuwa unamwamini Mungu, na kutafuta uzima, kwa kuwa unatafuta maarifa juu ya Mungu, na hutafuti nyaraka na mafundisho mfu, au ufahamu wa historia, unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu ya leo, na unapaswa kutafuta uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama ungekuwa mwanaakiolojia ungeweza kusoma Biblia—lakini wewe sio mwanaakiolojia, wewe ni mmoja wa wale wanaomwamini Mungu, na utakuwa bora zaidi ukitafuta mapenzi ya Mungu ya leo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (4)

Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi? Mimi huishi miongoni mwa wanadamu, ilhali bado wanadamu hawajui kuhusu kuwepo Kwangu. Ninapoangaza mwanga Wangu juu ya wanadamu, bado yeye hana ufahamu kuhusu kuwepo Kwangu. Wakati Ninatoa ghadhabu Yangu juu ya wanadamu, wao hukanusha kuwepo Kwangu kwa nguvu kubwa zaidi. Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp