Ni vipi Mungu amewaongoza na kuwaruzuku wanadamu hadi leo?

23/09/2018

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Ni kazi gani ambayo Mungu amefanya kuzigawanya mbari? Kwanza, aliandaa mazingira makubwa ya kijiografia, Akiwapa watu maeneo tofautitofauti, na kisha kizazi baada ya kizazi kinaendelea kuishi pale. Hii imeamuliwa—mawanda ya kuendelea kuishi kwao yameamuliwa. Na maisha yao, kile wanachokula, kile wanachokunywa, riziki zao—Mungu aliamua hayo yote zamani sana. Na Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, Alifanya maandalizi tofautitofauti kwa ajili ya aina tofauti za watu: Kuna vijenzi tofautitofauti vya udongo, hali ya hewa tofauti, mimea tofauti, na mazingira tofauti ya kijiografia. Maeneo tofautitofauti yana hata ndege na wanyama tofauti, maji tofauti yana aina tofauti za samaki wao spesheli na bidhaa za majini. Hata aina ya wadudu inaamuliwa na Mungu. … Tofauti katika vipengele hivi tofautitofauti zinaweza zisionekane au kufahamika kwa watu, lakini Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, alivionyesha kinaganaga na aliandaa mazingira tofauti ya kijiografia, mandhari tofauti, na viumbe hai tofauti kwa ajili ya mbari mbalimbali. Hiyo ni kwa sababu Mungu aliumba aina tofautitofauti za watu, na Anajua kile ambacho kila mmoja anahitaji na mitindo yao ya maisha ni nini.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Hii ni sawa na kusema, ikiwa wawindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, basi wasingekuwa tena na riziki yao. Hivyo ikiwa watu ambao wanategemea uwindaji wangepoteza milima ya misitu na wasiwe tena na ndege na wanyama, wasingekuwa tena na chanzo cha riziki yao, basi mwelekeo wa aina hiyo ya mbari ungechukua na mahali watu wa aina hii wangeelekea ni kiwango kisichojulikana, na wangeweza pia tu kutoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao hutegemea nini? Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo yao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi—uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng’ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama hawangekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Yaani, kama kuna tatizo na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi, na zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, kama hawangeweza kupanda vitu, na kupata vyakula vyao kutoka kwa mimea mbalimbali, matokeo yake yangekuwa nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali. Mungu ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira—ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.

Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Yehova aliwaumba wanadamu, ambayo ni kusema kwamba Yeye aliumba babu za wanadamu: Hawa na Adamu. Lakini hakuwapa akili zaidi au hekima. Ingawa walikuwa tayari wanaishi duniani, hawakuelewa takriban chochote. Na kwa hiyo, kazi ya Yehova ya kuwaumba wanadamu ilikuwa imekamilishwa nusu tu. Haikuwa imekamilika hata kidogo. Alikuwa ameumba tu mfano wa mwanadamu kutoka kwa udongo na kumpa pumzi Yake, lakini Hakuwa amempa mwanadamu radhi ya kutosha kumcha Yeye. Hapo mwanzo, mwanadamu hakuwa na akili ya kumcha Yeye, au kumwogopa Yeye. Mwanadamu alijua tu jinsi ya kuyasikiliza maneno Yake lakini hakujua ujuzi wa msingi wa maisha duniani na sheria za kufaa za maisha. Na kwa hiyo, ingawa Yehova aliumba mwanamume na mwanamke na kumaliza siku saba za shughuli, Hakukamilisha uumbaji wa mwanadamu hata kidogo, kwa maana mwanadamu alikuwa ganda tu, na hakuwa na uhalisi wa kuwa mwanadamu. Mwanadamu alijua tu kwamba ni Yehova aliyeumba wanadamu, lakini mwanadamu hakuwa na fununu ya jinsi ya kutii maneno na sheria za Yehova. Na kwa hiyo, baada ya kuumbwa kwa wanadamu, kazi ya Yehova ilikuwa mbali sana kumalizika. Pia alitakiwa kuwaongoza wanadamu kabisa mbele Yake ili wanadamu waweze kuishi pamoja duniani na kumcha Yeye, na ili wanadamu waweze kwa mwongozo Wake kuingia katika njia sahihi ya maisha ya kawaida ya binadamu duniani baada ya kuongozwa na Yeye. Kwa njia hii tu ndiyo kazi ambayo ilikuwa imeendeshwa kwa kiasi kikubwa kupitia jina la Yehova ilimalizika kabisa; yaani, kwa njia hii tu ndiyo kazi ya Yehova ya kuumba ulimwengu ilihitimishwa kabisa. Na kwa hiyo, kwa vile Alimuumba mwanadamu, Alipaswa kuongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu kadhaa, ili wanadamu waweze kutii amri na sheria Zake, na kushiriki katika shughuli zote za maisha ya kufaa ya binadamu duniani. Wakati huo tu ndio kazi ya Yehova ilikamilika kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili—kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini—na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. … Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.

…………

Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale ambayo bado hayajaonekana na yeyote: Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa “kuufurahia.” Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua? … Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza “utukufu” na “mapenzi” ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa ukweli wa kuwa mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza … ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha nafsi Yake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza binadamu wote na kiini Chake, na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huificha nafsi Yake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho binadamu wamekuwa wakigusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe. Je, hayo si kweli? Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawakaribisha watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Mungu Anapoanza kufanya kazi kwa mtu, wakati amemchagua mtu, Haambii yeyote, wala Hamwambii Shetani, wala hata kufanya maonyesho makubwa. Anafanya tu kwa ukimya, kwa asili kile ambacho kinahitajika. Kwanza, Anakuchagulia familia; usuli ambao hiyo familia inao, wazazi wako ni nani, mababu zako ni nani—haya yote tayari yaliamuliwa na Mungu. Kwa maneno mengine, haya hayakuwa uamuzi wa mvuto wa ghafla yaliyofanywa na Yeye, lakini badala yake hii ilikuwa kazi iliyoanza kitambo. Baada ya Mungu kukuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Kwa sasa, Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Kwanza unachukua hatua moja na kisha unachukua nyingine … sasa unaweza kukimbia, sasa unaweza kuruka, sasa unaweza kuongea, sasa unaweza kuonyesha hisia zako. Mwanadamu anavyokuwa, macho ya Shetani yamewekwa kwa kila mmoja wao, kama chui mkubwa mwenye milia anavyomwangalia nyara wake. Lakini kwa kufanya kazi Yake, Mungu hajawahi kuteseka mapungufu yoyote ya watu, matukio ama mambo, ya nafasi ama wakati; Anafanya kile anachopaswa kufanya na Anafanya kile Anacholazimika kufanya. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na bahati zako ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Mungu anakupa hakikisho halisi litakalodumu maisha yako yote, kwani Yeye yuko kando yako, anakulinda na kukutunza. Bila kujua haya, unakua. Unaanza kukutana na mambo mapya na unaanza kujua dunia hii na wanadamu hawa. Kila kitu ni kipya kwako. Unapenda kufanya kile unachopenda. Unaishi katika ubinadamu wako mwenyewe, unaishi katika nafasi yako ya kuishi na huna hata kiasi kidogo cha mtazamo kuhusu kuwepo kwa Mungu. Lakini Mungu anakulinda katika kila hatua ya njia unapokua, na Anakutazama unapoweka kila hatua mbele. Hata unapojifunza maarifa, ama kusoma sayansi, Mungu hajawahi toka upande wako kwa hatua hata moja. Wewe ni sawa na watu wengine kwamba, katika harakati za kuja kujua na kukutana na dunia, umeanzisha mawazo yako mwenyewe, una mambo yako mwenyewe ya kupitisha muda, mambo unayopenda mwenyewe, na pia unayo matamanio ya juu. Wakati mwingi unafikiria siku zako za baadaye, wakati mwingi ukichora muhtasari wa jinsi siku zako za baadaye zinapaswa kuwa. Lakini haijalishi kitakachofanyika njiani, Mungu anaona vyote na macho wazi. Labda wewe mwenyewe umesahau siku zako za nyuma, lakini kwa Mungu, hakuna anayeweza kukuelewa bora kuliko Yeye. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka. … Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakupi maelezo moja baada ya nyingine ya kila kitu Amefanya. Mungu hakukuruhusu kujua, na Hakukwambia). Hata hivyo, kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Yaani, kutoka alipozaliwa mwanadamu hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wao. Baada ya kusikia maneno haya, mnaweza kuhisi kana kwamba hamwelewi kikamilifu, kusema “usalama huu ni muhimu sana?” Kwa hivyo ni nini maana halisi ya “usalama”? Labda mnauelewa kumaanisha amani ama pengine mnauelewa kumaanisha kutopitia maafa ama msiba wowote, kuishi vyema, kuishi maisha ya kawaida. Lakini katika mioyo yenu lazima mjue kwamba si rahisi hivyo. Kwa hivyo ni nini hasa kitu hiki ambacho Nimekuwa nikizungumzia, ambacho Mungu anapaswa kufanya? Usalama unamaanisha nini kwa Mungu? Kuna hakikisho lolote la usalama wenu? La. Kwa hivyo ni nini hiki ambacho Mungu anafanya? Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu huacha nafsi kama hiyo na huacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu kiasi, silo? Kwa hivyo mbona hamwezi kujibu? Inaonekana kwamba hamwezi kuhisi wema mkubwa wa Mungu!

Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa kutayarisha kumchagua mtu na kumwokoa. Kwanza, una tabia gani, utazaliwa kwa familia ya aina gani, wazazi wako ni nani, una kaka na dada wangapi, na hali, hadhi ya kiuchumi na tabia za familia ambayo unazaliwa ndani ni gani—haya yote yanapangiwa wewe kwa uangalifu na Mungu. … Kwa nje, inaonekana kwamba Mungu hajafanya chochote kikuu kwa mwanadamu; Anafanya kila kitu kwa siri tu, kwa unyenyekevu na kwa kimya. Lakini kwa hakika, vyote ambavyo Mungu anafanya vinafanywa kuweka msingi wa wokovu wako, kuandaa njia mbeleni na kuandaa hali zote muhimu za wokovu wako. Mara moja wakati maalum wa kila mtu, Mungu anawarudisha mbele Yake—wakati unapofika kwako kusikia sauti ya Mungu, huo ndio wakati unapokuja mbele Yake. Wakati hili linafanyika, watu wengine wamekuwa wazazi tayari wenyewe, ilhali wengine ni watoto wa mtu tu. Kwa maneno mengine, watu wengine wameoa na kupata watoto ilhali wengine bado hawajaoa, na hawajaanza bado familia zao. Lakini licha ya hali za watu, Mungu tayari ameweka nyakati utakapochaguliwa na injili na maneno Yake yatakapokufikia. Mungu ameweka hali, ameamulia mtu fulani ama muktadha fulani ambamo injili itapitishwa kwako, ili uweze kusikia maneno ya Mungu. Mungu tayari amekuandalia hali zote muhimu ili, bila kujua, unakuja mbele Yake na unarudishwa kwa familia ya Mungu. Pia, bila kujua, unafuata Mungu na kuingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua, kuingia katika njia ya Mungu ya kazi ambayo, hatua kwa hatua amekuandalia. … Kuna sababu tofauti na njia tofauti za imani, lakini licha ya sababu inakuleta kumwamini Yeye, yote hakika yamepangwa na kuongozwa na Mungu. Kwanza, Mungu hutumia njia kadhaa ili kukuchagua na kukuleta katika familia Yake. Hii ndiyo neema Mungu anayompa kila mwanadamu.

Sasa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Hampi tena mwanadamu neema na baraka tu kama Alivyofanya mwanzoni, wala halazimishi watu kwenda mbele. Wakati wa hatua hii ya kazi, ni nini mwanadamu ameona kutoka kwa vipengele hivi vyote vya kazi ya Mungu ambavyo wamepitia? Wameona upendo wa Mungu, na hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa wakati huu, Mungu zaidi ya hayo, anamtegemeza, tia nuru, na kumwongoza mwanadamu, ili aje kujua nia Zake polepole, kujua maneno Anayozungumza na ukweli Anaompa mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati amevunjika roho, wakati hana popote pa kugeukia, Mungu atatumia maneno Yake kufariji, kushauri na kuwatia moyo, ili mwanadamu wa kimo kidogo aweze kupata nguvu polepole, kuinuka kwa wema na kuwa radhi kushirikiana na Mungu. Lakini wakati wanadamu hawamtii Mungu ama wanampinga Yeye, ama wanapofichua upotovu wao, Mungu hataonyesha huruma kuwarudi na kuwafundisha nidhamu. Kwa ujinga, kutojua, unyonge, na uchanga wa mwanadamu, hata hivyo, Mungu ataonyesha uvumilivu na ustahimilivu. Kwa njia hii, kupitia kazi yote Mungu anamfanyia mwanadamu, mwanadamu anapevuka, anakua na anakuja kujua nia za Mungu polepole, kujua baadhi ya ukweli, kujua ni nini mambo mema na ni nini mambo hasi, kujua uovu ni nini na kujua giza ni nini. Mungu hamrudi na kumfundisha nidhamu mwanadamu siku zote wala Haonyeshi uvumilivu na ustahimilivu siku zote. Badala yake anampa kila mtu kwa njia tofauti, katika hatua zao tofauti na kulingana na kimo na ubora wa tabia yao tofauti. Anamfanyia mwanadamu mambo mengi na kwa gharama kubwa; mwanadamu hafahamu lolote la gharama hii ama mambo haya Mungu anafanya, ilhali yote ambayo anafanya kwa kweli inafanywa kwa kila mtu. Upendo wa Mungu ni wa kweli: Kupitia neema ya Mungu mwanadamu anaepuka janga moja baada ya jingine, ilhali kwa unyonge wa mwanadamu, Mungu anaonyesha ustahimili wake muda baada ya muda. Hukumu na kuadibu kwa Mungu yanaruhusu watu kuja kujua polepole upotovu wa wanadamu na kiini chao cha kishetani. Kile ambacho Mungu anapeana, kutia nuru Kwake kwa mwanadamu na uongozi Wake yote yanawaruhusu wanadamu kujua zaidi na zaidi kiini cha ukweli, na kujua zaidi kile ambacho watu wanahitaji, njia wanayopaswa kuchukua, kile wanachoishia, thamani na maana ya maisha yao, na jinsi ya kutembea njia iliyo mbele. Haya mambo yote ambayo Mungu anafanya hayatengwi na lengo Lake la awali. Ni nini, basi lengo hili? Mbona Mungu anatumia njia hizi kufanya kazi Yake kwa mwanadamu? Anataka kutimiza matokeo gani? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho anataka kuona kwa mwanadamu na kupata kutoka kwake? Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumwacha mtu kujua alipotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ya kuwacha mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kuabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na wazo nyuma ya kazi Yake kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya uasherati, tabia potovu, lakini badala yake kutaka kufuatilia ukweli kwa kuridhishwa kwa Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki katika kazi ya Mungu na katika maneno Yake kwa njia njema kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata uchaji wa Mungu na uepukaji wa uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa Ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawaje mwanadamu, anayeishi miongoni mwa viumbe vyote amepotoka na kudanganywa na Shetani, angali hawezi kupuuza maji yaliyoumbwa na Mungu, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu angali bado anaishi na kuzaana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu zingali hazijabadilika. Binadamu angali anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na viganja vyake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali toleo la Mungu limebakia hivyo bila kubadilishwa, welekevu ambao binadamu alitumia kushirikiana na Mungu bado haujabadilika, welekevu wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili zake halijabadilika, hamu ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi katika mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawaje mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena kutoka mwanzo wa uumbaji, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira na kadhalika, na amejaa tabia ya kishetani iliyopotoka, kwenye macho ya Mungu, mwanadamu yungali bado mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu angali anatawaliwa na kupangiwa na Mungu, na angali anaishi ndani ya mkondo uliowekwa wazi na Mungu, na kwa hivyo kwenye macho ya Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya kujikokota kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na mwenye umri ulioongezeka kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu ananuia kuokoa. Mwanadamu huyu anahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama wima na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona umbo la Muumba naye hatakuwa msikivu wa kila kitu kingine, ataacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wakati moyo wa mwanadamu unapoelewa maneno hayo ya moyoni kutoka kwa Muumba, mwanadamu atakataa Shetani na atakuja upande wake Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine toleo na ukuzaji kutoka kwa Muumba, basi kumbukumbu la mwanadamu litarejeshwa, na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp