Mtu anawezaje kujua asili na tabia ya Mungu?

23/09/2018

Maneno Husika ya Mungu:

Raha ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa wanadamu; raha Yake ni raha ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi, ishara ya fadhili. Hasira ya Mungu inatokana na uharibifu ambao kuwepo na kuingilia kwa dhuluma kunaleta kwa wanadamu Wake, kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na chema. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule mwanadamu mzuri lakini mwenye upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu hupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kutoka wakati huu kuendelea, na ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wa mwangaza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Mungu ndicho kile Alicho na Anacho kile anacho. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukifichua ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Kila alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, tulizo kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye ambaye hawezi kukosewa(wala Hatavumilia kukosewa)[b] na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanao uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. … Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia, Ninawasubiri; Niko kando yenu….

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Kumjua Mungu kunapaswa kufanywa kupitia kwa kusoma na kulielewa neno la Mungu. Wengine husema: “Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo ningewezaje kumjua Mungu?” Kwa kweli, neno la Mungu ni maonyesho ya tabia ya Mungu. Kutoka kwa neno la Mungu unaweza kuuona upendo na wokovu wa Mungu kwa wanadamu, na mbinu Yake ya kuwaokoa…. Hii ni kwa sababu neno la Mungu linaonyeshwa na Mungu Mwenyewe ikilinganishwa na kumtumia mwanadamu kuliandika. Linaonyeshwa na Mungu binafsi. Anaeleza maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. Kwa nini inasemekana kwamba ni maneno ya dhati? Kwa sababu hayo hutolewa kutoka ndani kabisa, Akionyesha tabia Yake, mapenzi Yake, mawazo Yake, upendo Wake kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na matarajio Yake ya wanadamu…. Miongoni mwa maneno ya Mungu kuna maneno makali, maneno ya upole na yenye kuzingatia, na kuna maneno mengine ya ufunuo ambayo hayalingani na matakwa ya binadamu. Ikiwa unayaangalia tu maneno ya ufunuo, utahisi kwamba Mungu ni mkali kabisa. Ikiwa unaangalia maneno ya upole tu, utahisi kuwa Mungu hana mamlaka mengi. Kwa hiyo hupaswi kuelewa hili nje ya muktadha, lakini uliangalie kutoka kila pembe. Wakati mwingine Mungu huzungumza kwa mtazamo mpole na wenye huruma, na watu wanauona upendo wa Mungu kwa wanadamu; wakati mwingine Yeye huzungumza kwa mtazamo mkali, na watu wanaona tabia ya Mungu ambayo haitavumilia kosa lolote. Mwanadamu ni mchafu kwa njia ya kusikitisha na hastahili kuuona uso wa Mungu au kuja mbele za Mungu. Kuwa watu wanaweza sasa kuja mbele za Mungu ni neema ya Mungu tu. Hekima ya Mungu inaweza kuonekana kutokana na jinsi Yeye anavyofanya kazi na maana ya kazi Yake. Watu bado wanaweza kuona mambo haya katika neno la Mungu hata bila kuwasiliana na Yeye moja kwa moja.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vyenyewe ni ukweli; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kukionyesha waziwazi; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu anapenda, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, ni watu wapi Anaowadharau na ni watu wapi Anaowafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Mbali na kujua kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kimatendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu huo umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kuna tofauti na vile ambavyo Mungu alivyo kwa kweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Miliki na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyatekeleza mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chemichemi na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu matokeo yaliotarajiwa ya maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia ya Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii mamlaka ya Mungu na mipango. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na katika wakati huu atakuwa pia amepata viwango tofauti vya ufahamu kumhusu Yeye. Kuelewa huku na maarifa havitoki katika kitu ambacho mwanadamu amefikiria ama kutengeneza, ila kutoka kwa kile ambacho anafahamu, anapitia, anahisi, na anashuhudia ndani yake mwenyewe. Ni baada tu ya kufahamu, kupitia, kuhisi, na kushuhudia vitu hivi ndipo ufahamu wa mwanadamu kumhusu Mungu utapata ujazo, ni maarifa anayopata katika wakati huu pekee ndio ulio halisi, wa kweli na sahihi, na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, uzoefu, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa dhati na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa dhati na kujua miliki na uwepo wa Mungu, anakuja na kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhakika wa kweli kuhusu, na ufafanuzi sahihi wa, ukweli wa mamlaka ya Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mkondo kamili kwa na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu anabadilika, hatua kwa hatua, mawazo yake kuhusu Mungu, bila kumwaza pasi na msingi, ama kuipa nafasi tashwishi yake kumhusu Yeye, ama kutomwelewa, ama kumshutumu, ama kupitisha hukumu Kwake, ama kuwa na shaka Naye. Kwa sababu hii, mwanadamu atakuwa na mijadala michache na Mungu, atakuwa na uhasama kiasi kidogo na Mungu, na kutakuwa na matukio machache ambapo atamuasi Mungu. Kwa upande mwingine, kujali kwa mwanadamu na utii kwa Mungu kutakua kwa kiasi kikubwa, na uchaji wake Mungu utakuwa wa kweli zaidi na pia mkubwa zaidi. Katika ya aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kupewa ukweli pekee na ubatizo wa uzima, bali wakati uo huo pia atapata maarifa ya kweli ya Mungu. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kubadilishwa kwa tabia yake na kupata wokovu pekee, bali pia kwa wakati huo atafikia uchaji na ibada ya kweli ya kiumbe aliyeumbwa kwa Mungu. Baada ya kuwa na aina hii ya ushirika, imani ya mwanadamu katika Mungu haitakuwa tena ukurasa tupu wa karatasi, ama ahadi ya maneno matupu, ama harakati na tamanio lisilo na lengo na kuabudu kama mungu; katika aina hii ya ushirika pekee ndio maisha ya mwanadamu yatakua kuelekea ukomavu siku baada ya siku, na ni wakati huu ndio tabia yake itabadilika polepole, na imani yake kwa Mungu, hatua kwa hatua, itatoka kwenye imani ya wasiwasi na kutoeleweka na imani isiyo ya hakika mpaka katika utii wa kweli na kujali, na kuwa katika uchaji Mungu wa kweli, na mwanadamu pia, katika mchakato wa kumfuata Mungu, ataendelea polepole kutoka kuwa mtazamaji na kuwa na hali ya utendaji, kutoka yule anayeshughulikwa na kuwa anayechukua nafasi ya kutenda; kwa aina hii ya ushirika pekee ndipo mwanadamu atafikia kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu, kwa ufahamu wa kweli wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji

Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho binafsi wa Mungu, na hali halisi ya Mungu haviwezi kutimizwa kwa kutegemea kufikiria kwako. Kwa vile huwezi kutegemea kufikiria ili kujua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kutimiza maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na hali halisi ya kujua kwa utaratibu na uthibitishaji wa mamlaka ya Mungu na hivyo basi utafaidi kuelewa kwa utaratibu na maarifa yaliyoongezeka. Hii ndiyo njia tu ya kutimiza maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuuliza kutofikiria si sawa na kukufanya uketi kimyakimya ukisubiri maangamizo, au kukusitisha dhidi ya kufanya kitu. Kutotumia akili zako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki ya kujijazia, kutotumia maarifa kuchambua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufurahia, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye Mungu Mwenyewe ni wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza nia hii, lakini unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Nakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua kwa uangalifu na bila kusita na kuhakikisha kile Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analolielezea na Analolifanya. Hii ndiyo njia pekee ya kujua Mungu. Kwani kile Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si cha wazi na tupu—lakini cha kweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yanasema “ni ishara ya kutoweza.”

b. Maandishi asilia yanasema “na vilevile ishara ya kutoweza kukosewa kuwa (na kutovumilia kukosewa).”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp