Ni katika vipengele vipi ambapo uweza na hekima ya Mwenyezi Mungu hufichuliwa hasa?

23/09/2018

Njia ambazo kwazo uweza na hekima ya Mwenyezi Mungu hufichuliwa hasa

Maneno Husika ya Mungu:

Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kiumbe kipya Alichokiumba, na maneno na kufanikiwa Kwake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu yoyote ndogo na bila ya kuchelewa kokote kudogo. Kujitokeza na kuzaliwa kwa viumbe hivi vyote vipya kulikuwa ithibati ya mamlaka na nguvu za Muumba: Yeye ni mzuri sawa tu na neno Lake, na neno Lake litakamilika, na kile kinachokamilika kinadumu milele. Hoja hii haijawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa kale, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa daima dawamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kufaidi kila kitu Alichoweka wazi ili kufaidi, na kutimiza kila kitu Alichoweka wazi ili kutimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa ameumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa ameumba kulingana na mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa cha mfumo na cha kawaida. Viumbe vyote viliishi na kufa pia kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kiumbe kilichoachwa!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Bwana Yesu alipomleta Lazaro kutoka kwa wafu, Alitumia mstari mmoja: “Lazaro, kuja nje.” Hakusema kitu kingine mbali na hiki—maneno haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha hoja kwamba Mungu anaweza kukamilisha chochote kupitia maongezi, kukiwemo kumfufua mtu aliyekufa. Mungu alipoumba viumbe vyote, Alipouumba ulimwengu, Alifanya hivyo kwa maneno—amri za kutamkwa, maneno yaliyotamkwa kwa mamlaka, na hivyo tu viumbe vyote viliumbwa. Yalikamilishwa hivyo. Mstari huu mmoja uliozungumzwa na Bwana Yesu ulikuwa sawa na maneno yaliyotamkwa na Mungu alipoziumba mbingu na dunia na viumbe vyote; mstari huo pia uliweza kushikilia mamlaka ya Mungu, uwezo wa Muumba. Viumbe vyote viliumbwa na vikasimama kwa sababu ya matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu, na vivyo hivyo, Lazaro alitembea kutoka katika kaburi lake kwa sababu ya matamshi kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu. Haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ya Mungu, yaliyoonyeshwa na kutambuliwa katika mwili Wake. Aina hii ya mamlaka na uwezo vilimilikiwa na Muumba, na kwa Mwana wa Adamu ambaye kwake Muumba alitambuliwa. Huu ndio ufahamu uliofunzwa kwa mwanadamu kwa Mungu kumleta Lazaro kutoka kwa wafu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kile Nilichosema lazima kihesabiwe, kile kilichohesabiwa lazima kikamilishwe, na hili haliwezi kubadilishwa na yeyote; hili ni thabiti. Kama ni kile Nilichosema katika wakati uliopita au Nitakachosema katika siku za usoni, yote yatatimia, na wanadamu wote wataliona hili. Hii ni kanuni inayoelekeza kazi ya maneno Yangu. … Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu? Chochote Nisemacho hufanyika, na miongoni mwa wanadamu, ni nani aliyepo anayeweza kuyabadilisha mawazo Yangu? Yaweza kuwa agano Nililofanya juu ya dunia? Hakuna chochote kinachoweza kuuzuia mpango Wangu; Mimi huwepo wakati wote katika kazi Yangu na vilevile katika mpango wa usimamizi Wangu. Ni mwanadamu gani anaweza kuingilia? Je, sio Mimi binafsi Niliyetengeneza mipango hii? Kuingia katika hali hii leo, bado haipotei kutoka kwa mpango Wangu au Nilichoona mbele; yote iliamuliwa Nami zamani sana. Ni nani miongoni mwenu anaweza kufahamu mpango Wangu wa hatua hii? Watu Wangu wataisikiliza sauti Yangu, na kila mmoja wa wale wanaonipenda kwa kweli atarudi mbele ya kiti Changu cha enzi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1

Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Wakati mapepo yalikemewa kutoka kwa mwanadamu na alikombolewa, hii ilimaanisha tu kwamba alipokonywa kutoka kwa mikono ya Shetani na kurudishwa kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. … Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu Yake kwa neno. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali hukumu kwa neno unaweza kuwakilisha bora mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Mnapaswa kuona mapenzi ya Mungu na kuona kwamba kazi ya Mungu si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Wakati wa hatua hii ya kazi Yake, Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa binadamu iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni mwa binadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo ambalo Alikuwa ameliamua kimakusudi kabla; mtu anaweza kusema kwamba hili halikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya hili ndiyo Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali: “Hekima Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayewapotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema. Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kitii mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu duniani kipumzike chini ya kigonda Chake, na pia Huwafanya wale watenda maovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu wajipate katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa binadamu, kwani Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya dunia, au kwenye ulimwengu kwa ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti, Aliwaumba binadamu kwenye dunia, na ilikuwa ni kwa sababu ya binadamu ndiyo Alianza rasmi vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na duniani huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule ukweli wa ndani katika kila hatua ya kazi, kuona hasa ni vipi mnaweza kuelezea uweza wa Mungu na hasa ni vipi mnavyoweza kuelezea uhalisia wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Katika mpango Wangu, Shetani amewahi kushindana na kila hatua, na, kama foili[a] ya hekima Yangu, amejaribu siku zote kutafuta njia na namna za kuvuruga mpango Wangu wa awali. Lakini Ningeweza kushindwa na njama zake danganyifu? Vyote mbinguni na duniani vinanitumikia—njama danganyifu za Shetani zingeweza kuwa tofauti? Huku ndiko hasa kukutana kwa hekima Yangu, ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu matendo Yangu, na ni kanuni ambayo mpango Wangu mzima wa usimamizi unafanywa kupitia. Wakati wa ujenzi wa ufalme, bado Mimi siepuki njama danganyifu za Shetani, ila Naendelea kufanya kazi ambayo lazima Nifanye. Kati ya vitu vyote katika ulimwengu, Nimechagua matendo ya Shetani kama foili Yangu. Je, hii si hekima Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 8

Ninapoanza kirasmi Kazi Yangu, watu wote wanatembea kama Mimi hatua kwa hatua, kiasi kwamba watu katika ulimwengu wote wanakuwa katika hatua na Mimi, kuna “shangwe” ulimwengu mzima, na mwanadamu anaendelezwa mbele na Mimi. Kwa sababu hii, joka kubwa jekundu mwenyewe anachapwa na Mimi mpaka anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na wazimu, na anahudumia Kazi Yangu, na, licha ya kutokuwa na nia, anashindwa kufuata tamaa zake mwenyewe, na kukosa njia nyingine ila kujiwasilisha kwa udhibiti Wangu. Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili[a] Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha “mahitaji” Yangu kwake. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya kazi Yangu katika mwili inakamilika katika nyumba ya joka huyu. Kwa njia hii, joka kubwa jekundu anapata uwezo zaidi wa kunitumikia Mimi vizuri, kwa njia ambayo Mimi Nitamshinda na kukamilisha Mpango Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 29

Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili ilipoanza kuenezwa kote duniani mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa binadamu; na hivyo basi kumshinda binadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwenye busara kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani kwa mbali. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Nimesema hapo awali: Mimi ni Mungu mwenye hekima. Ninatumia ubinadamu Wangu wa kawaida kuwafichua watu wote na tabia ya shetani, kuwafichua wale wenye nia mbaya, wale wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na kwa njia nyingine bila wao kufahamu, wale wanaonipinga, wale wasio waaminifu Kwangu, wale wanaotamani fedha, wale ambao hawaudhukuru mzigo Wangu, wale wanaojihusisha na ulaghai na udanganyifu pamoja na ndugu zao, wale wanaozungumza kwa maneno matamu ili kuwafanya watu wafurahi, na wale ambao hawawezi kuratibu na ndugu zao kwa umoja kwa kujitolea. Kwa sababu ya ubinadamu Wangu wa kawaida, watu wengi sana hunipinga kwa siri na kushiriki katika ulaghai na udanganyifu, wakidhani kuwa ubinadamu Wangu wa kawaida haujui. Na watu wengi sana wanatilia maanani maalum ubinadamu Wangu wa kawaida, wakinipa vitu vizuri nile na kunywa, wakinitumikia kama watumishi, na wakininenea yaliyo ndani ya mioyo yao, huku wakati wote wakitenda tofauti kabisa pasi na ufahamu Wangu. Binadamu vipofu! Hamnijui kabisa—Mungu ambaye huangalia ndani sana ya moyo wa mwanadamu. Bado hamnijui Mimi hata sasa; bado mnafikiri Sijui kile unachonuia. Fikiria jambo hilo: Ni watu wangapi ambao wamejiangamiza kwa sababu ya ubinadamu Wangu wa kawaida? Amka! Usinidanganye tena. Lazima uweke tabia na mwenendo wako wote, kila neno na tendo lako mbele Yangu, na ukubali ukaguzi Wangu wa hilo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 76

Natenda kwa busara. Bila kisu, bila bunduki na bila juhudi yoyote, Nitawashinda kabisa wale wanaonipinga na kuliaibisha jina Langu. Mimi ni karimu, na kwa kasi thabiti Naendelea na kazi Yangu hata wakati Shetani anasababisha usumbufu kama huo; Simjali na Nitamshinda kwa ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Hii ni nguvu Yangu na hekima Yangu, na hata zaidi ni sehemu ndogo ya utukufu Wangu usioisha.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 91

Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. …

Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. … Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 19

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp