Bwana Yesu alisema: “Ila yeyote akunywaye maji ambaye nitampa hatawahi kuwa na kiu; lakini maji hayo ambayo nitampa yatakuwa chemichemi ya maji ambayo yanachipuka katika uhai wa daima(Yohana 4:14). Watu wengi wanafikiri kwamba Bwana Yesu tayari ametupa njia ya uzima wa milele, lakini nimeyasoma maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele.” Haya yote yanahusu nini? Kwa nini yanasema kwamba ni Kristo tu wa siku za mwisho anayeweza kumpa mtu njia ya uzima wa milele?

08/06/2019

Jibu:

Kuhusu kile njia ya uzima wa milele kilicho kwa kweli, tunapaswa kwanza kujua inapotoka. Sisi sote tunajua kwamba Mungu alipokuwa mwili, Alitoa ushuhuda kwamba Yeye ndiye kweli, njia, na uzima. Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba Kristo pekee ndiye Anayeweza kuonyesha njia ya uzima wa milele. Kwa kuwa Kristo ndiye kuonekana kwa Mungu mwenye mwili, kwa kuwa Yeye ndiye Roho wa Mungu aliyejivika mwili, hiyo ina maana kwamba kiini cha Kristo ni kiini cha Mungu, na kwamba Kristo Mwenyewe ndiye kweli, njia, na uzima. Kwa hivyo, Kristo anaweza kuonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu. Hii ni ya hakika. Bila kujali Mungu anakuwa mwili katika enzi gani, kiini cha Kristo hakiwezi kubadilika kamwe. Bwana Yesu ni Mungu Mwenyewe katika mwili. Kwa hiyo Bwana Yesu alipokuja, Alijishuhudia kama ukweli, njia na uzima, na chanzo cha maji yaliyo hai ya uzima kwa wanadamu; Aliweza kuuonyesha ukweli na kumpa mwanadamu njia ya kutubu. Jinsi Bwana Yesu alivyosema: “Yeyote anayekunywa haya maji atakuwa na kiu tena: Ila yeyote akunywaye maji ambaye nitampa hatawahi kuwa na kiu; lakini maji hayo ambayo nitampa yatakuwa chemichemi ya maji ambayo yanachipuka katika uhai wa daima(Yohana 4:13-14). Kila kitu kilichonenwa na Bwana Yesu ni onyesho la asili Yake takatifu, na pia inaonyeshwa kwa mujibu wa kazi ya ukombozi iliyotekelezwa na Yeye. Jambo hili halikaniki! Bwana Yesu ni Mungu katika mwili; Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu. Yeye pia ni Mungu mwenye mwili, mfano halisi wa ukweli. Kwa hiyo, tangu kuwasili kwa Mwenyezi Mungu, Amejishuhudia pia kuwa ndiye ukweli, njia, na uzima na Akaonyesha ukweli wote ili Awasafishe na kuwaokoa wanadamu, Akimpa mwanadamu njia ya uzima wa milele. Kwa nini Mungu amejishuhudia kuwa ukweli, njia na uzima wakati wa kupata mawili Kwake mara mbili? Ni kwa sababu Kristo ni mwenye asili takatifu. Kwa kifupi, Mungu Mwenyewe ndiye njia ya uzima wa milele—Mungu Mwenyewe ndiye uzima wa milele. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili Anaweza kuonyesha ukweli, na Anaweza kumpa mwanadamu njia ya uzima wa milele na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe katika enzi tofauti. Kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu imegawanywa kwa hatua. Si kitu ambacho kinaweza kukamilika kupitia hatua moja tu ya kazi ya ukombozi. Baada ya Mungu kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, bado Anahitaji kutekeleza kazi Yake ya kuwahukumu, kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu kabisa katika siku za mwisho. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu aliahidi kwamba Atarudi, jambo ambalo linathibitisha kwamba kazi ya Mungu haikomi kusonga mbele, kwamba haingekoma hata kidogo wakati wa Enzi ya Sheria au Enzi ya Neema. Wokovu wa Mungu kwa wanadamu unajumuisha hatua tatu za kazi, yaani, kazi katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme. Kipindi cha kuanzia Enzi ya Sheria hadi Enzi ya Neema kilidumu takriban miaka 2,000, na kuanzia Enzi ya Neema hadi Enzi ya Ufalme ulidumu kwa kwa takriban miaka mingine elfu mbili. Kazi yote ya hukumu ikianzia nyumba ya Mungu iliyotekelezwa na Bwana Yesu aliyerudi ni kazi ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kabisa; pia ni kazi ya kuitamatisha enzi ya giza na uovu na kuianzisha Enzi ya Ufalme. Mpango wa usimamizi wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu utafanikishwa kupitia kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, na wanadamu wataletwa katika hatima nzuri. Kwa hiyo, kwa kuwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho inaweza kuzaa matunda haya, si waweza kusema kwamba ukweli wote ulioonyeshwa katika kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni njia ya uzima wa milele ambayo Mungu huwapa wanadamu? Ikiwa kuna watu wengi ambao watashindwa na ukweli ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho, ambao wanasafishwa, kukamilishwa, ambao wanapata maarifa kumhusu Mungu, ambao maisha yao yanabadilishwa, na ambao wanaishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu halisi, basi je, njia ya uzima ambayo wamepata ndiyo njia ya uzima wa milele kweli? Ikiwa kweli ndiyo njia ya uzima wa milele, basi ni hakika kwamba ni ukweli ambao unaweza kumsafisha, kumwokoa, na kumkamilisha mwanadamu, na ni hakika kwamba inaweza kuwaruhusu watu kufikia maarifa ya Mungu, utiifu kwa Mungu, na ibada kwa Mungu. Hii ni hakika. Ikiwa tuna ufahamu wa kweli wa jambo hili na kisha tuangalie tena ukweli wote ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu, basi tutaweza kujua njia ya uzima wa milele ni nini.

Nyakati zote mbili ambazo Mungu amekuwa mwili Ameweza kuwapa wanadamu ukweli, njia, na uzima, lakini yote ambayo Bwana Yesu alifanya ilikuwa tu kazi ya ukombozi. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho pekee ndiye Afanyaye kazi ya hukumu na utakaso, na kwa njia ya kazi Yake pekee ndiyo matokeo ya kuwasafisha kabisa na kuwaokoa wanadamu yanaweza kufanikishwa. Sasa katika ushirika labda baadhi ya watu watauliza: “Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi Yake, kwa nini hakufichua kabla kazi ambayo ingetekelezwa na ukweli ambao ungeonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho? Inawezekana kuwa Bwana Yesu hakuweza kuwahukumu na kuwaadibu wanadamu? Yawezekana kuwa Bwana Yesu hakuweza kutupa ukweli na uzima? Je, hatuwezi kupata uzima wa milele kwa njia ya neno la Bwana Yesu?” Bila shaka, watu wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu maswali haya, lakini ni lazima tuelewe kwamba kila hatua ya kazi ya Mungu ina kiini na maudhui yake yenyewe, na kila hatua ya kazi Yake itafanikisha matokeo fulani. Kwa hiyo, ukweli wote unaoonyeshwa katika kila hatua ya kazi ya Mungu na maneno yote Anayoyanena ni ya maana na yana madhumuni yake yenyewe; yote hutumikia kufikia matokeo. Maneno yote yaliyoonyeshwa katika kila hatua ya kazi ya Mungu yanahusu kazi Yake yote na yanatamkwa ili kufikia matokeo yaliyokusudiwa. Mungu hawezi kamwe kusema chochote kisichohusiana na kazi Yake—hii ndiyo kanuni ya kazi Yake na neno Lake. Kazi yote iliyofanywa na Bwana Yesu ilikuwa kazi ya ukombozi, si kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Kwa hiyo, ukweli wote ulioonyeshwa na Bwana Yesu ulihusu kazi Yake ya ukombozi na ni tofauti na ukweli wote unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kwa ajili ya utakaso, wokovu na ukamilifu wa mwanadamu. Hii ndiyo sababu ukweli wote pekee unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ndio unaoweza kuitwa njia ya uzima wa milele ambao unaweza kumsafisha, kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu, wakati ambapo ukweli wote ulioonyeshwa na Bwana Yesu ni ukweli tu unaowakomboa wanadamu. Kile Alichoonyesha ni njia ya toba tu kwa wanadamu kwa sababu kazi ya Mungu ina mpango, na ina hatua. Kazi yoyote ambayo Mungu anapaswa kufanya katika kila enzi tayari imepangwa—Mpango Wake hauwezi kubadilika, na hatavuruga mpango Wake Mwenyewe kupitia kwa kazi Yake. Jinsi ilivyokuwa katika Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa tu sheria ya kuyaongoza maisha ya wanadamu duniani kwa mujibu wa mahitaji ya wanadamu na mpango Wake wa kazi. Alikuwa Akifanya tu kazi ya kuyaongoza maisha ya wanadamu duniani. Kisha Bwana Yesu akaja, Akianzisha Enzi ya Neema, na Akaonyesha njia ya toba, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu,” na Akafanya kazi ya kuwakomboa wanadamu kwa njia ya kusulubiwa Kwake. Na katika siku za mwisho Mwenyezi Mungu amekuja, Akionyesha ukweli wote ili kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu. Anaitekeleza kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu, Akimalizia enzi iliyopita na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Hii inaturuhusu tuone kwamba kazi yoyote ambayo Mungu hutekeleza katika enzi yoyote, ukweli wowote Anaohitaji kuonyesha, yote imepangwa na ni yenye msimamo. Kazi ya Mungu ina muundo na husonga hatua kwa hatua, kila hatua ikikamilishana. Kila hatua ya kazi ya Mungu hutegemea mahitaji ya wanadamu, kimo halisi cha wanadamu, na mipango ya Mungu iliyoamuliwa kabla. Bwana Yesu alipokuwa Akifanya kazi Yake ya ukombozi, mwanadamu hakuwa na maarifa kumhusu Mungu au kazi ya Mungu; watu walitambua tu kwamba Mungu aliumba mbingu na ardhi na vitu vyote na walijua tu kufuata sheria na amri za Mungu. Kwa hiyo, Bwana Yesu alipotekeleza kazi Yake ya kuwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, Alionyesha tu njia ya kutubu, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu,” ili kumwezesha mwanadamu kuja mbele za Mungu, kukiri dhambi zake, na kutubu, na kukiri kwa Mungu dhambi zote alizozifanya ili aweze kumwomba Mungu msamaha wa dhambi na wokovu. Hii ilikuwa pia ili aweze kumwomba Mungu, kumshukuru Mungu na kumsifu Mungu, na kuweza kufurahia neema yote ya Mungu. Haya ni matokeo ambayo yamepatikana tayari kwa njia ya kazi ya Mungu ya ukombozi. Baada ya miaka mingi ya imani, watu wachache sana wanaweza kutambua kwamba dhambi zote ambazo wamezifanya zimeondolewa kabisa na Mungu, lakini asili yao halisi ya dhambi bado ipo kama ilivyokuwa awali, na imefanywa madhubuti kiasi kwamba bado wamo chini ya udhibiti wa asili yao ya dhambi, wakitenda dhambi mara nyingi na kumpinga Mungu. Hawajaondokana na mibano ya dhambi na kuwa safi. Hili ni jambo ambalo kila mtu anakubali kama ukweli. Kwa hiyo, kwa waumini kama sisi ambao tumeondolewa dhambi zetu, je, kweli tumepokea njia ya uzima wa milele? Je, kuondolewa dhambi zetu ina maana kwamba tumetakaswa? Je, inamaanisha kwamba tumepata wokovu kwa kweli na kwamba tumepokea sifa ya Mungu? Ikiwa matokeo haya hayawezi kufanikishwa, basi tunawezaje kusema kwamba tumepokea njia ya uzima wa milele kupitia imani yetu katika Bwana? Je, kuna mtu yeyote anayethubutu kusema jambo hili? Kazi ambayo Bwana Yesu alitekeleza ilikuwa ile ya ukombozi, na Alichohubiri kilikuwa njia ya kutubu. Kazi Yake bila shaka ilikuwa kuandaa njia ya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa hivyo, katika kumkubali Bwana Yesu tumepata tu kuondolewa dhambi zetu; hatujapata uzima wa milele kwa kweli. Ikiwa tunaweza kuikubali kazi ya hukumu katika siku za mwisho inayotekelezwa na Bwana Yesu aliyerudi, basi tutatakaswa na kupokea sifa ya Mungu, na wakati huo tu ndipo tutakuwa watu ambao wamepata uzima wa milele kwa kweli. Imani yetu katika Bwana Yesu inatuondolea tu dhambi zetu na kutuwezesha kumwomba Mungu na kufurahia neema Yake. Haya ni matokeo tu yaliyofanikishwa kupitia kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu. Kuna watu wengi ambao hawana ufahamu wa kazi ya Bwana Yesu. Wanafikiria kwamba kwa kuwa Bwana Yesu amekamilisha kazi Yake ya ukombozi na wameondolewa dhambi zao kwa sababu ya imani yao katika Bwana, kazi ya Mungu ya wokovu imekamilika kabisa. Wanafikiri kwamba kwa kuwa jambo moja limemalizika, kila kitu kimemalizika. Hili ni kosa kubwa mno! Ikiwa hii ingekuwa ukweli basi kwa nini Bwana Yesu alisema kwamba Atarudi? Watu wengi hawajui ni kazi gani hasa ambayo Bwana Yesu anapaswa kufanya wakati wa kurudi Kwake; huu ni ukosefu wa maarifa kuhusu kazi ya Mungu. Wanategemea tu mawazo na fikira za binadamu wanapoichunguza kazi ya Bwana Yesu. Wanafikiria kwamba tunapata uzima wa milele kwa kumwamini Bwana tu, kwamba tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni hivyo tu. Je, si haya ni mawazo na fikira za mwanadamu?

Sasa labda kila mtu anajua kwamba ni kupitia tu kazi iliyotekelezwa na Bwana Yesu aliyerudi katika siku za mwisho kuwa mtu anaweza kupata uzima wa milele. Huu ni ukweli mtupu. Kwa hivyo ni kwa nini Kristo pekee wa siku za mwisho ndiye anayeweza kumpa mwanadamu njia ya uzima wa milele? Je, yawezekana kwamba Bwana Yesu hawezi kumpa mwanadamu hilo? Huwezi kusema hivyo. Lazima tuwe na hakika juu ya hili: Bwana Yesu ni kupata mwili kwa Mungu, Yeye Mwenyewe ndiye kweli, njia na uzima, na Yeye Mwenyewe ana njia ya uzima wa milele. Kwa hiyo basi, kwa nini hatuwezi kupata uzima wa milele kwa kuamini tu katika Bwana Yesu? Kwa nini Kristo wa siku za mwisho pekee ndiye anayeweza kumpa mwanadamu njia ya uzima wa milele? Hii hasa inategemea matokeo yanayofanikishwa kupitia kazi ya Mungu. Sisi sote tunajua kwamba katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alitekeleza tu kazi ya ukombozi, kwa hiyo, ingawa sisi tuliondolewa dhambi zetu kuanzia wakati ambapo tulimwamini Bwana, bado tunaongozwa na asili yetu ya dhambi na mara nyingi sisi hutenda dhambi na kumpinga Mungu bila sisi kupenda. Hatuwezi kuondokana na mibano ya dhambi na kuwa safi, na hatustahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Hii inatosha kuthibitisha kwamba kazi ya Bwana Yesu ya kuwakomboa wanadamu haikuwa kazi ya kuwasafisha kabisa na kuwaokoa wanadamu—ni kazi ya hukumu katika siku za mwisho pekee inayofanywa na Bwana Yesu aliyerudi ndiyo inayoweza kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu. Ndiyo maana Bwana Yesu alitabiri kwamba Atarudi; kama vile Bwana Yesu alivyosema: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). “Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). Unabii wa Bwana Yesu tayari umetimia. Yaani, Mwenyezi Mungu anafanya kazi ya hukumu Akianzia nyumba ya Mungu katika siku za mwisho, na Ameonyesha ukweli wote ili kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu. Ukweli huu ni njia ya uzima wa milele ambao mwanadamu atapewa na Mungu katika siku za mwisho. Kupitia hukumu, Mwenyezi Mungu anaingiza ukweli wote anaouonyesha ndani ya wanadamu ili uweze kuwa uzima wa mwanadamu. Mungu haonyeshi ukweli bila sababu nzuri; Analenga mawazo na fikira mbalimbali za mwanadamu, Analenga asili na kiini cha mwanadamu cha kutotii na kumkataa Mungu pamoja na tabia mbalimbali za shetani za mwanadamu katika kuonyesha Kwake ukweli ili kuwahukumu na kuwafichua wanadamu. Mchakato wa wateule wa Mungu kukubali ukweli ni mchakato wa kupitia hukumu na adhabu na kuvumilia shida za usafishaji, pamoja na mchakato wa kutakaswa na kupata wokovu. Ndio maana kila mtu anayepitia hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho anaelewa ukweli mwingi; anajua kwa kweli kiini chake kipotovu ambacho humpinga na kumsaliti Mungu, na pia anaelewa kiini kitakatifu cha Mungu na tabia Yake ya haki, isiyokosewa. Ana uchaji na utiifu wa kweli kwa Mungu, na wote wamepokea ukweli na uzima kutoka kwa Mungu—wamefanyika kuwa washindi na Mungu. Kikundi hiki cha watu ni wale ambao walitabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo kuwa washindi ambao watatoka katika dhiki kuu. Hii inaonyesha kuwa wakati wa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, wateule Wake watalazimika kupitia shida nyingi ili waweze kutakaswa kabisa. Je, hilo linaweza kuwa jambo rahisi? Je, ni rahisi kwao kuukubali ukweli kama uzima wao? Lazima wavumilie shida nyingi, na hizi shida zote ni kupitia hukumu na kuadibiwa na Mungu; wanazipitia zote ili waupokee ukweli kama uzima wao. Yote yanaweza kuitwa matukio yanayotokea unapokaribia kufa, au kama vile kupitia mageuzi kamili. Watu hawa watakapotoka katika dhiki kuu na kuwa washindi, uzima ambao watapata utakuwaje kwa kweli? Utakuwa njia ya uzima wa milele inayotokana na kazi yote ya hukumu ya Kristo wa siku za mwisho.

Katika Enzi ya Neema Bwana Yesu alitekeleza kazi ya ukombozi, ambayo iliwapa watu njia hii pekee: “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu.” Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho, na Ameonyesha ukweli wote ili kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi iliyotekelezwa na Bwana Yesu. Anaiokoa kabisa jamii potovu ya wanadamu kutoka kwa ushawishi wa Shetani ili kwamba wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, kutoka kwa uchafu na upotovu wao, na warudie mfano wao wa asili wa binadamu. Hii itawawezesha wanadamu kuishi mbele za Mungu, ambapo wanaweza kuwa watu wanaomtii na kumwabudu Mungu, ikitamatisha mpango wa usimamizi wa Mungu wa kuiokoa jamii ya binadamu. Kwa hiyo, ni kwa kukubali tu kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ndipo tunaweza kusafishwa na kuokolewa, na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Wakati huu katika ushirika, kila mtu anapaswa kujua sasa kwa nini ni Kristo wa siku za mwisho pekee ndiye Anayeweza kumpa mtu njia ya uzima wa milele.

Kimetoholewa Kutoka Katika Majibu ya Mswada wa Filamu

Bwana Yesu ni Mungu aliyekuwa mwili, ni kuonekana kwa Mungu. Bwana Yesu alisema, “Na yeyote ambaye anaishi na kuniamini hatakufa kamwe(Yohana 11:26). “Maji hayo ambayo nitampa yatakuwa chemichemi ya maji ambayo yanachipuka katika uhai wa daima(Yohana 4:14). Biblia inasema, “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele(Yohana 3:36). Maneno haya yote ni ukweli, yote ni hakika! Kwa sababu Bwana Yesu ni Mungu kuwa mwili, Ana dutu ya Mungu na utambulisho. Yeye Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele. Yale yote Anayosema na kufanya ni maonyesho ya kawaida ya maisha ya Mungu. Yale yote anayoeleza ni ukweli na kile Mungu anacho na kile Alicho. Kwa hivyo Bwana Yesu Mwenyewe ni uzima wa milele, na anaweza kupeana njia ya uzima wa milele. Anaweza kuwafufua wafu. Kwa kumwamini Bwana Yesu, tunaamini katika Mungu pekee wa Kweli, na hivyo tunaweza kupokea uzima wa milele. Hili halina pingamizi. Ufufuo wa Bwana Yesu wa Lazaro ni ushahidi mzuri kuwa Bwana Yesu anaweza kutupa njia ya uzima wa milele, Ana mamlaka hii. Basi, mbona Bwana Yesu hakuridhia njia ya uzima wa milele katika Enzi ya Neema? Hii ni kwa sababu, Bwana Yesu alikuja kupigwa msumari msalabani ili kumkomboa binadamu, sio kufanya kazi ya utakaso na wokovu kama katika siku za mwisho. Kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ilijishughulisha tu na kusamehe dhambi za mwanadamu, lakini haikutoa asili ya kishetani na tabia kutoka kwa mwanadamu. Kwa hivyo, kwa kumwamini Bwana, tulisamehewa dhambi zetu, lakini tabia yetu ya kishetani haikuwahi takaswa. Bado tunatenda dhambi bila kupenda, tunampinga na kumsaliti Mungu. Baada ya kuthibitisha haya yote, tunafaa kuwa wazi kwa kitu fulani. Kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi katika Enzi ya Neema iliandaa njia kwa kazi ya hukumu katika siku za mwisho, kwa hivyo, baada ya Bwana Yesu kumaliza kazi ya ukombozi, Aliahidi pia kuwa Atarudi tena. Wakati mmoja Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Kutoka kwa maneno ya Bwana Yesu tunaweza kuona Bwana atakapokuja tena tu katika siku za mwisho ndipo Ataeleza ukweli wote unaotakasa na kuokoa mwanadamu. Hapa, “Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote.” Ukweli huu ni ukweli hasa ambao Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anaonyesha kwa kutakasa na kuwaokoa wanadamu. Ni maneno yanayosemwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa, na ni njia ya uzima wa milele ambayo Mungu ameweka juu ya mwanadamu katika siku za mwisho. Hii ndiyo sababu wafuasi wa Mungu hawakuweza kupata njia ya uzima wa milele katika Enzi ya Neema. Bwana Yesu alisema, “Na yeyote ambaye anaishi na kuniamini hatakufa kamwe.” Na Biblia inasema, “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele.” Lakini kwa kweli, Bwana alisema haya ili kushuhudia ukweli kuwa Yeye Mwenyewe ni kuonekana kwa Mungu, na Yeye tu ndiye anayeweza kumridhia mwanadamu uzima wa milele. Ahadi ya Bwana Yesu kuwa wale wanaomwamini hawatakufa kamwe ni ushuhuda kwa mamlaka ya Mungu. Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele, Mungu anaweza kupatia mwanadamu uzima wa milele. Hii sio kusema kuwa mwanadamu amepokea uzima wa milele baada ya kukubali kazi ya Bwana Yesu. Naamini kila mmoja anaelewa hili. Lakini kwa jamii ya kidini, watu wengi wanaamini kuwa bora tu dhambi zao zimesamehewa, watu wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Je, kuna msingi kwa mtazamo huu katika neno la Mungu? Bwana Yesu hakusema kitu chochote kama hicho. Tufikirie kuihusu: Kulingana na mawazo yetu na dhana, ili mradi dhambi zetu zimesamehewa tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele, lakini mbona Bwana Yesu alitabiri mara nyingi kuwa Atarejea tena? Na mbona Aliwaambia wanafunzi Wake unabii na mafumbo mengi? Unabii na mafumbo hayo ni vitu ambavyo Atatimiza Atakaporejea tena. Je, inaweza kuwa kwamba watu wanamwamini Bwana kwa miaka mingi lakini bado hawaoni vitu hivi kwa wazi? Watu wakimkubali tu Bwana lakini wasikubali kurejea Kwake, hii ni shida ya aina gani? Je, hii si kumsaliti Bwana? Sio ajabu Bwana Yesu alisema: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni. Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:21-23). Maneno ya Bwana sasa yamekuwa ukweli kabisa. Mtu akimkubali tu Bwana Yesu lakini asikubali kurudi Kwake, je, huyu ni mtu anayemwamini Mwana kweli? Huyu ni mtu anayemsaliti Bwana! Waumini wa kweli wa Mwana ni wale wasiomwamini Bwana tu lakini wanakubali kurudi kwake pia, wanaomfuata Kristo hadi mwisho. Mtu wa aina hii tu ndiye anaweza kupata uzima wa milele. Lakini wale wanaoamini katika Bwana Yesu tu lakini hawamkubali Mwenyezi Mungu wote ni watu wanaomsaliti Bwana Yesu. Wanaamini katika Bwana lakini kwa sababu hawamfuati Mungu hadi mwisho, imani yao ni ya bure—wanaanguka kando ya njia. Bwana Yesu anaamua kuwa ni watenda uovu kwa sababu wanatambua tu jina Lake lakini hawakubali kurudi kwake. Na Alisema: “Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Kwa hivyo mniambie, wale watu ambao wamelaaniwa hivyo na kutupwa nje na Bwana, wale wanashika jina Lake tu, je, wanaweza kupata uzima wa milele? Ni hakika kuwa hawatapata chochote. Hata zaidi, watateremshwa jahanamu na kuadhibiwa! Hii inaonyesha kabisa tabia ya Mungu ya haki na takatifu.

Licha ya kwamba wakati mwanadamu alikubali ukombozi wa Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, dhambi zao zilisamehewa na wakapewa haki ya kumuomba Mungu na kufurahia neema na baraka Zake, haiwezi kukataliwa katika wakati huu, mwanadamu bado anashurutishwa na asili yake ya dhambi, bado anaishi kwa unyonge katika dhambi, hawezi kabisa kutenda neno la Bwana na hana heshima na utii wa kweli kwa Mungu. Katika wakati huu, mwanadamu anaweza kila mara kumdanganya na kumlaghai Mungu, anatafuta umaarufu na ustawi, tamaa ya pesa na kufuata mwenendo wa ulimwengu. Hasa wakati kazi ya Mungu haiko sambamba na fikira za mwanadamu, mwanadamu angelaumu, hukumu na hata kumpinga Mungu. Watu kama hao hawangeweza hata kutubu kwa kweli, kwa hivyo, watu kama hao hawangeweza kupata kibali cha Bwana? Ingawa watu wengi wanaweza kufuata, kutoa ushahidi, hata kutoa maisha yao kama kafara kwa Bwana, na hata kutubu kweli, kwa kweli, je, tabia zao zilizopotoka zimetakaswa ili waweze kupata utakatifu? Hivyo je, wanamjua Bwana kweli? Je, wamejitoa kweli kutoka ushawishi wa Shetani na kutwaliwa na Mungu? Hapana kabisa, huu ni ukweli ambao unatambulika kwa kawaida. Hii inatosha kuthibitisha kuwa kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema ilikuwa tu kazi ya ukombozi. Hakika haikuwa kazi ya wokovu na ukamilisho ya siku za mwisho. Maneno ambayo Bwana Yesu alieleza katika Enzi ya Neema yaliwapatia watu tu njia ya toba, sio njia ya uzima wa milele, kwa hivyo hii ndio sababu Bwana Yesu alisema Atakuja tena. Kurejea kwa Bwana Yesu ni kufanya kazi ya kueleza ukweli na kukabidhi mwanadamu njia ya uzima wa milele, ili waweze kujitoa kabisa kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kupata ukweli kama maisha kuwa watu wanaomjua Mungu, kumtii Mungu, kumheshimu Mungu na kulingana na Mungu, ili waweze kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho Ameanzisha kazi ya hukumu akianzia nyumba ya Mungu na ameeleza ukweli wote kusafisha na kuokoa binadamu. Ameonyesha binadamu tabia ya Mungu ya haki, uadhimu na isiyokosewa, kuhukumiwa na kufichua dutu na ukweli wa mwanadamu kupotoshwa na Shetani. Amefukua chanzo cha uasi wa mwanadamu na upinzani kwa Mungu, na kumwambia mwanadamu nia yote ya Mungu na mahitaji. Wakati uo huo, Ameelezea wanadamu kwa masharti wazi ukweli wote ambao mwanadamu atahitaji kupokea wokovu, kama vile hadithi ya ndani na dutu ya hatua zote tatu ya kazi ya Mungu ya wokovu na pia uhusiano kati ya hatua hizi tatu, tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, hadithi ya ndani na ukweli wa Biblia, fumbo la hukumu katika siku za mwisho, fumbo la wanawali wenye busara wakinyakuliwa na ile ya kukamilisha watu kuwa washindi kabla ya majanga, fumbo la Mungu kuwa mwili, na kile kinachomaanisha kumwamini kweli, kumtii na kumpenda Mungu, jinsi ya kumheshimu Mungu na kuepuka maovu ili kulingana na Kristo, jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kadhalika. Ukweli huu, ni njia ya uzima wa milele iliyokabidhiwa na Mungu juu ya mwanadamu katika siku za mwisho. Hivyo, kama tunataka kupata ukweli na uzima, kupata wokovu, utakaso na kukamilishwa, basi lazima tukubali na kutii maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Hii ndio njia pekee ambayo tutaweza kupata ukweli na uzima.

Wacha tusome vifungo vichache vya neno la Mwenyezi Mungu: “Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ameeleza ukweli wote ambao utatakasa na kumuokoa mwanadamu. Maneno haya ni mengi, ya kina na yako na riziki yote ambayo Mungu anatoa. Yanafungua macho yetu na kujenga maarifa yetu, yakituruhusu kuona kuwa Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kristo ni njia ya uzima wa milele. Maneno ambayo Mungu ameeleza katika Enzi ya Ufalme yanaenda zaidi ya yale yaliyosemwa katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Hasa, kwa “Matamshi ya Mungu kwa Dunia Nzima” katika Neno Laonekana katika Mwili, Mungu anajijulisha kwa mara ya kwanza kwa binadamu wote. Pia ni mara ya kwanza binadamu wanasikia matamshi ya Muumba kwa wanadamu wote. Hii imetuma mawimbi ya mshtuko kwa dunia nzima, na kufungua macho ya mwanadamu. Hii ni kazi ya hukumu mbele ya kiti cheupe cha enzi katika siku za mwisho. Enzi ya Ufalme ni enzi ambapo Mungu anafanya kazi ya hukumu, na ni enzi ambapo tabia ya Mungu ya haki inafanywa wazi kwa binadamu wote. Hivyo, katika Enzi ya Ufalme, Mungu anaeleza neno Lake, akimhukumu, kumtakasa na kumkamilisha mwanadamu. Anatuma chini aina yote ya majanga juu ya mwanadamu, Akiwatuza wazuri na kuadhibu waovu. Anafichua haki ya Mungu, uadhama na ghadhabu kwa binadamu. Ukweli wote ambao Mwenyezi Mungu anaeleza ili kumtakasa, kumuokoa na kumkamilisha mwanadamu ni njia ya uzima wa milele ambayo Mungu anamkabidhi mwanadamu katika siku za mwisho. Ukweli huu ni maji ya mto wa uzima utiririkao kutoka kwa kiti cha enzi. Hivyo, katika imani yetu kwa Mungu kama tunataka kupata njia ya uzima wa milele, na kupata kunyakuliwa na kuingia ufalme wa mbinguni, lazima tukubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu, Kristo katika siku za mwisho, na pia hukumu na kuadibu ya maneno Yake. Jinsi hii tu ndipo tutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu, kuelewa na kupata ukweli, kufikia utakaso, na kuokolewa. Wale tu wanaopitia hukumu ya Mwenyezi Mungu na kuadibu katika siku za mwisho wana haki ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Huu ni ukweli kabisa! Tukiendelea kushikilia fikira zetu za kidini, mwishowe tutakuwa hao watakaopata hasara. Wanawali wenye busara wanalenga tu kutafuta ukweli na kusikiliza maneno ya Mungu, lakini wanawali wapumbavu wanashikilia tu barua ya Biblia na dhana zao na fikira, na hawatafuti ukweli ama kusikia sauti ya Mungu. Basi siku moja, ghafla wataangukia janga na watakuwa wanalia na kusaga meno yao, na hata majuto yatakuwa bure. Hivyo, wale wote wasiomkubali Mwenyezi Mungu wataanguka katika janga na kuadhibiwa. Hiki ndicho Mungu ameagiza na hakuna anayeweza kukibadilisha. Hasa wale ambao wanalaani kazi ya Mwenyezi Mungu sana katika siku za mwisho wamefichuliwa tayari na Mungu kuwa wapinga Kristo wa siku za mwisho—watu hao watapata adhabu ya milele na hawatakuwa tena na fursa ya kukutana na Mungu. Ni wazi kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni kuainisha mwanadamu kulingana na aina, kuamua matokeo ya watu, na kukamilisha enzi. Leo tunaweza kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, hivi tumepata kweli neema Yake na huruma Yake. Huku ni kuinuliwa kwa mwisho na Mungu! Sisi sote lazima tumpe Mwenyezi Mungu shukrani!

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tanbihi:

a. Kipande cha gogo lililokufa: Nahau ya Kichina yenye maana “-siyoweza kusaidiwa.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp