Wakati huo, wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Mafarisayo Wayahudi walimkana na kumhukumu Yeye vikali na kumtundika msalabani. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anapokuja kufanya kazi Yake, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia wanamkana Yeye vikali na kumhukumu Yeye, wakimtundika Mungu msalabani tena. Kwa nini Mafarisayo Wayahudi na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa huuchukia ukweli hivyo na kumpinga vikali Kristo kwa njia hii? Ni nini hasa kiini chao cha asili?

09/06/2019

Jibu:

Kila mtu anayeamini katika Bwana anajua Mafarisayo waliompinga Bwana Yesu, lakini mzizi, asili ya kweli ya upinzani wao ilikuwa nini? Unaweza kusema kwamba katika historia ya dini ya miaka 2,000, hakuna mtu aliyeelewa jibu la swali hili. Ingawa kulaani kwa Bwana Yesu kwa Mafarisayo kuliandikwa katika Agano Jipya, hakuna mtu ambaye ameweza kumaizi asili ya Mafarisayo. Mwenyezi Mungu anapowasili katika siku za mwisho, Anafichua jibu la kweli kwa swali hili. Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu, “Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).

Mwenyezi Mungu anasema waziwazi. Mzizi wa upinzani wa Mafarisayo na shutuma kwa Bwana Yesu ulikuwa kwamba hawakumcha Mungu au kutafuta ukweli katu. Ndani zaidi, walikuwa wakaidi na wenye kujisifu; hawakutii ukweli. Mafarisayo walimfafanua Mungu ndani ya dhana na mawazo yao wenyewe, ndani ya maneno halisi ya Biblia. Walimlinda Masihi katika jina tu. Bila kujali maneno ya Bwana Yesu yalikuwa ya kina na sahihi vipi, jinsi maneno Yake ni ukweli, au maneno Yake yana mamlaka au nguvu kiasi gani, kwa kuwa jina Lake si Masihi, Mafarisayo walimpinga na kumshutumu. Licha ya Mafarisayo kukosa kukubali ukweli ulioonyeshwa na Bwana Yesu, walimjaribu na kujaribu kumpata na hatia. Kwa mfano, walimjaribu Bwana Yesu kwa kuuliza alitumia mamlaka gani kufanya miujiza na kumuuliza Bwana Yesu kwa makusudi kama wangeweza kulipa kodi kwa Kaisari. Waliuliza Bwana Yesu kama alikuwa mwana wa Mungu, Kristo, nk. Bwana Yesu alijibu mipango yao ya uovu kwa ukweli na hekima. Mafarisayo hawakuwa na nguvu ya kumkana lakini bado hawakutafuta ukweli. Bado walimpinga na kumshutumu kwa ulokole Bwana Yesu; walimfanya Bwana Yesu akamatwe na kudai kwamba Akongomewe msalabani. Ilikuwa tu kama Bwana Yesu alivyosema alipowafunua, “Lakini sasa mwataka kuniua, mtu aliyewaambia ukweli, ambao nimesikia kutoka kwake Mungu(Yohana 8:40). “Na nikisema ukweli, mbona hamnisadiki?(Yohana 8:46). Kwa hivyo, tunaweza kuona kwamba Mafarisayo, katika asili na kiini, walikuwa pepo wa kishetani, maadui wa Mungu waliochukia ukweli! Je, ni aina gani ya watu wanaweza kuchukia na kumlaani Kristo? Hadithi ya Mafarisayo inaonyesha ukweli mmoja: Wote ambao wanaamini katika Mungu lakini hawaupendi ukweli, wanachoshwa na ukweli na wanauchukia ukweli hawamjui Mungu. Zaidi ya hayo, watu hawa hakika humpinga Mungu na kumchukulia kama adui yao. Kwa sababu asili ya Kristo ni ukweli, njia, na uzima, yeyote ambaye anachukia ukweli pia anamchukia Kristo. Watu wengi wanaochukia ukweli huonekana wema kwa nje; wao hufuata amri za Biblia na hawaonekani kama watu wabaya kamwe, lakini Kristo atakapokuja kufanya kazi Yake, hawa maadui wa kishetani wa Mungu watafunuliwa kabisa.

Upinzani mwovu wa Mafarisayo na shutuma kwa Bwana Yesu unafunua kabisa asili yao ya uovu: Wanachukia ukweli na kumpinga Mungu. Wakati ambapo Bwana Yesu alihubiri na kufanya kazi Yake, alionyesha ukweli mwingi, Alionyesha miujiza mingi na kuwapa watu neema tele. jambo ambalo lilifichua mamlaka na nguvu ya Mungu. Kazi ya Bwana Yesu ilitikisa misingi ya dini ya Kiyahudi na kushtua serikali ya Kiyahudi. Watu wengi walimfuata Bwana Yesu. Mafarisayo walijua kwamba Bwana Yesu angeendelea kufanya kazi Yake, waaminifu wote katika dini ya Kiyahudi wangemfuata; dini ya Kiyahudi ingeanguka, na vyeo vyao na riziki kutoweka. Kwa hivyo, waliamua kumwua Bwana Yesu. Kama vile Biblia inavyosema, “Kisha makuhani wakuu na Mafarisayo walikonga baraza, na wakasema, Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamsadiki: nao Warumi watafika na kuichukua nafasi yetu na taifa letu. … Hivyo kuanzia siku hiyo walishauriana pamoja ili wamuue” (Yohana 11:47-53). Ili kulinda hadhi yao na riziki, Mafarisayo walishirikiana na serikali ya Kirumi ili kumslubisha Bwana Yesu msalabani. Walisema, “Damu yake iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu” (Mathayo 27:25). Kama unavyoona, Mafarisayo walichukia ukweli na kumchukia Kristo. Walifika mahali ambapo hawakutaka kuishi tena pamoja na Kristo kitambo! Ni afadhali wangeacha sadaka yao ya dhambi kuliko kukosa kumsulubisha Bwana Yesu; ni afadhali wafanye dhambi za kuogofya kumpinga Mungu na kumkosea Mungu na kuwafanya watoto wao na wajukuu kulaaniwa kuliko kukosa kumgongomea Bwana Yesu msalabani, Yeye ambaye anaonyesha ukweli wa ukombozi kwa wanadamu. Hiyo ni kiini na asili halisi, ya kishetani, inayochukia ukweli ya Mafarisayo. Wakati ambapo Bwana Yesu alipigiliwa misumari msalabani, jua lilikuwa giza, nchi ilitetemeka na pazia ya hekalu lilipasuka na kuwa wazi. Baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alionekana mbele za watu tena. Baada ya watu kufahamu mambo haya, walitubu kwa ajili ya dhambi zao na kumgeukia Bwana Yesu. Na kwa mintarafu ya Mafarisayo? Licha ya wao kutotubu, pia walikuwa maadui hata zaidi wa Bwana Yesu. Waliwalipa askari kutoa ushahidi wa uongo na kusema Bwana Yesu hakuwa amefufuliwa. Mitume walipoeneza injili ya Bwana Yesu, Mafarisayo waliwakamata na kuwateswa mno. Walitaka kupiga marufuku kazi ya Bwana Jesu, ili kupata malengo yao ya udhibiti wa kudumu wa jumuiya ya dini. Mafarisayo waliamini katika Mungu kwa jina tu. Katika hali halisi, walichukia ukweli na walimpinga Mungu. Kiini cha upinzani wao na hukumu kwa Bwana Yesu kilikuwa kama ifuatavyo: Walikuwa wanajaribu kushindana na Mungu na kumpima; walikuwa wanapigana dhidi ya Mungu. Majivuno ya upinzani wao na chuki kwa Bwana Yesu yaliweka wazi kabisa malengo yao na kufunua uso wao wenye uovu, wa kishetani. Hata zaidi, yalifunua asili yao ya uovu ya mpinga Kristo: kukataa kutubu, chuki ya wenda wazimu wa ukweli na chuki kwa Mungu. Je, si hivyo ndivyo wachungaji na wazee wa kanisa wa jumuiya ya dini humchukulia Mwenyezi Mungu? Kama tungeweza kuona waziwazi jinsi wachungaji na wazee wa kanisa humpinga na kumlaani Mwenyezi Mungu, bila shaka tungejua kwamba Mafarisayo walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu kwa njia hiyo hiyo.

Miaka 2,000 iliyopita, wakuu wa makuhani, waandishi na Mafarisayo wa Kiyahudi walimpigilia misumari Bwana Yesu msalabani. Miaka 2,000 baadaye, viongozi wa dini wamesababisha historia kujirudia kwa kumpigilia msumari Mungu msalabani tena! Sote tumeona kwamba Mwenyezi Mungu anatekeleza kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Yeye anaonyesha ukweli unaotakata na kuokoa ubinadamu. Yeye hufichua siri zote za Mungu mpango wa usimamizi. Yeye huhukumu na kufunua asili ya kishetani ya ubinadamu ambayo humpinga na kumsaliti Mungu. Yeye huwaonyesha tabia Yake yenye haki ambayo haiwezi kukosewa. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli. Yana mamlaka na nguvu na hutusadikisha kikamilifu. Ukweli huu husafisha na kuokoa ubinadamu. Shukrani kwa Bwana. Basi vipi kuhusu wachungaji na wazee wa kanisa siku hizi? Hawajali jinsi maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, jinsi maneno Yake yana mamlaka na nguvu kiasi gani, jinsi yanaweza kusafisha na kumwokoa mtu. Kwa ukaidi, bado wanadumisha dhana ya uwongo: “Yeyote asiyeshuka juu ya wingu na kuniinua mimi katika ufalme wa Mbinguni si kurudi kwa Bwana Yesu.” Wao humpinga na kumlaani Mwenyezi Mungu kwa hasira. Wao hulifuata tu jina la Bwana Yesu na kufuata maneno haya mawili “Bwana Yesu” kwa upofu, lakini kwa ulokole wanampinga na kumlaani Mwenyezi Mungu. Je, hii ina tofauti na wakati ambapo Mafarisayo walilinda jina la Masihi lakini walimpinga na kumlaani Bwana Yesu? Je, si asili yao ni sawa na ile ya Mafarisayo: mkaidi, mwenye kiburi, hatii ukweli, anachukia ukweli? Wao huamini katika Mungu asiye yakini juu mbinguni, na wanamkana, wanampinga na kumlaani Kristo mwenye mwili; wao ni wapinzani wasiopatana na Kristo. Je, si ni wapinga Kristo tu wakimkana, kumlaani na kumpinga Kristo? Biblia inasema, “Na jinsi mlivyosikia kuwa mpinga Kristo atakuja, hata sasa kunao wapinga Kristo wengi; katika hili tunajua kuwa haya ni majira ya mwisho” (1 Yohana 2:18). “Kwa kuwa walaghai wengi wameingia ulimwenguni, ambao hawakubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili. Huyu ni mlaghai na anayempinga Kristo” (2 Yohana 1:7). Kwa hivyo, wote wasiomtambua Mungu mwenye mwili ni wapinga Kristo. Wote wampingao na kumlaani Kristo ni wapinga Kristo. Kwa hivyo, Mafarisayo wa Kiyahudi walifunuliwa kama wapinga Kristo na kazi ya Bwana Yesu. Wachungaji na wazee wa kanisa katika siku za mwisho wote ni wapinga Kristo ambao wanafunuliwa kazi ya Mwenyezi Mungu. Kazi ya Mungu mwenye mwili kweli huwafichua watu! Kila kitu ambacho Kristo anaonyesha katika siku za mwisho ni ukweli. Hafichui tu wanawali wenye busara na wapumbavu, Anafunua kila aina ya wapinga Kristo na wasioamini. Huu ni ukweli ambao hakuna mtu anaweza kuukataa!

Viongozi wa dini katika siku za mwisho na wakuu wa makuhani, waandishi na Mafarisayo wa Kiyahudi, kiini na mizizi ya upinzani wao kwa Mungu ni sawa. Namna ambazo wachungaji na wazee wa kanisa humpinga Mungu ni mbaya zaidi kuliko ile ya wakuu wa makuhani, waandishi na Mafarisayo. Tangu Mwenyezi Mungu aanze kufanya kazi Yake ya hukumu kutoka katika nyumba ya Mungu, watu wote wa kila madhehebu walinyakuliwa mbele ya kiti cha enzi Cha Mungu, almradi wanaupenda ukweli na kutamani sana kuonekana kwa Mungu. Wachungaji na wazee hufanya juu chini katika kumpinga na kumlaani Mwenyezi Mungu, yote katika jaribio la kuwazuia waamini na kuimarisha vyeo na riziki yao. Wao hueneza uvumi, hutoa ushahidi wa uongo na kumkufuru Mwenyezi Mungu; wao hulizuia kanisa na kuwakataza kabisa waumini kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Wao hutishia, huwaogofya, hukejeli na kuwapiga ndugu ambao wanaeneza injili ya ufalme. Wao hata hushirikiana na CCP ya kishetani ili kuwakamata na kuwatesa wakiwaacha mamia ya maelfu ya ndugu bila nyumbani pa kurudi. Watu wapatao elfu mia moja wameteswa kwa ukatili na CCP. Wengi hata wameuawa…. Upinzani wa wachungaji na wazee wa kanisa kwa Mwenyezi Mungu ni wa kukithiri zaidi kuliko upinzani wa Mafarisayo kwa Bwana Yesu ulivyokuwa. Matendo yao maovu katika upinzani dhidi ya Mungu ni mengi. Mwenyezi Mungu aliwahukumu na kuwalaani kitambo. Mwenyezi Mungu asema, “Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[1] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu kuliko mfalme wa wote, kujua kidogo kwamba wao si zaidi ya nzi wenye uvundo. Na bado, wanatumia vibaya uwezo wa nguruwe na mbwa ambao ni wazaziwe ili kukashifu uwepo wa Mungu. Kama nzi wadogo, wanaamini wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi wenye meno.[2] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, ilihali wazazi wao ni nguruwe wachafu mara mamia ya mamilioni kuliko wao wenyewe kwa ukubwa? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na kwa njia hizi wanaleta ukandamizaji kwa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea yale yanayoendelea kwa nyuma katika ulimwengu wa kidini). Ni jinsi gani mwanadamu angejua kwamba, licha ya urembo mzuri wa mbawa za nzi, nzi mwenyewe ni kiumbe mdogo tu, aliye na tumbo iliyojaa uchafu na mwili uliojaa vijidudu? Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza tena mkondo mwingine wa usaliti, wakianzisha kazi yao yenye miaka maelfu kadhaa iliyopita. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)). Maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yalishirikishwa hadharani kupitia magazeti, televisheni na Intaneti muda mrefu uliopita. Aina zote mbalimbali za sinema na video za injili tayari zimechapishwa katika Intaneti ili shuhudia waziwazi udhihirisho wa Mungu na kazi kwa dunia nzima. Hii imesababisha kiwimbi kikubwa miongoni mwa jamii ya dini na ubinadamu kwa ujumla. Wachungaji na wazee wa kanisa katika jumuiya ya dini tayari wameona mwelekeo unaoongezeka: Maneno ya Mwenyezi Mungu yanawashinda wale wa jumuiya ya dini na ubinadamu kwa ujumla. Hakuna mtu na hakuna nguvu inaweza kuyazuia. Wamekuwa wa kukerwa na wanampinga na kumlaani Mwenyezi Mungu kwa ulokole. Wanajaribu kuharamisha kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na kufikia ndoto zao zilizohemkwa; udhibiti wa milele juu ya jumuiya ya dini na mamlaka ya milele juu ya wateule wa Mungu. Ukweli huu unatosha kuthibitisha kwamba wachungaji wa dini na wazee wa kanisa katika siku za mwisho ni kujitokeza tena kwa Mafarisayo! Wao ni pepo wanaompinga Kristo ambao hufanya kazi kwa bidii kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu na kuapa kabisa kuwa maadui wa Mungu! Matendo yao mengi maovu tayari yamechochea tabia ya Mungu. Wanawezaje kutoroka hukumu na adhabu ya Mungu yenye haki?

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tanbihi:

1. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

2. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Unafiki ni nini?

Maneno Husika ya Mungu: Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp