Unyakuo ni lazima utegemezwe maneno ya Mungu na sio dhana na mawazo ya mwanadamu

24/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni” (Mathayo 6:9-10).

“Na mimi Yohana nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Na nikasikia kutoka mbinguni sauti kubwa ikisema, Tazama, maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka katika macho yao; na hakutakuwa na kifo tena, wala uchungu, wala kilio, wala hakutakuwa na maumivu tena; maana ile hali ya kale imepita!” (Ufunuo 21:2-3).

“Falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele” (Ufunuo 11:15).

“Na hakuna mwanadamu amepaa hadi mbinguni, isipokuwa yeye ambaye alishuka chini kutoka mbinguni, ambaye ni Mwana wa Adamu aliye mbinguni” (Yohana 3:13).

Ikiwa “kunyakuliwa” kweli kunamaanisha kuinuliwa hewani au mbinguni, na iwapo ufalme wa mbinguni uko duniani au mbinguni

Maneno Husika ya Mungu:

“Kunyakuliwa” si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanavyofikiria. Hili ni kosa kubwa sana. Kunyakuliwa kunarejelea kujaaliwa Kwangu na kuchagua. Kunawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale ambao wamepata hadhi ya mzaliwa wa kwanza, hadhi ya wana, au watu, ni wale wote ambao wamenyakuliwa. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 104

Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuwaongoza binadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. Mungu hataishi tena miongoni mwa binadamu, na mwanadamu pia hataweza kuishi na Mungu katika hitimisho la Mungu. Mungu na mwanadamu hawawezi kuishi ndani ya ulimwengu sawa; badala yake, wote wawili wana njia zao binafsi za kuishi. Mungu ndiye anayeongoza binadamu wote, wakati binadamu wote ni matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Ni binadamu wanaoongozwa; kuhusu kiini, binadamu si sawa na Mungu. Kuingia rahani kunamaanisha kurudi pahali pa awali pa mtu. Kwa hivyo, Mungu aingiapo rahani, kunamaanisha kwamba Mungu amerudi pahali Pake pa awali. Mungu hataishi tena duniani ama kushiriki kwa furaha na mateso ya binadamu wakati yupo miongoni mwa binadamu. Binadamu wanapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; binadamu watamwabudu Mungu wakiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na binadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Wakati mwanadamu anamwabudu Mungu katika pumziko, ataishi duniani, na wakati Mungu anaongoza sehemu iliyobaki ya binadamu katika pumziko, Atawaongoza kutoka mbinguni, sio kutoka duniani. Mungu bado atakuwa Roho, wakati mwanadamu bado atakuwa mwili. Mungu na mwanadamu wote wawili wana njia zao tofauti za kupumzika. Mungu anapopumzika, Atakuja na kujitokeza miongoni mwa mwanadamu, mwanadamu anapopumzika, ataongozwa na Mungu kutembea mbinguni na pia kufurahia maisha mbinguni. Baada ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, Shetani hatakuweko tena, na kama Shetani, wale watu waovu pia hawatakuweko tena. Kabla ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, wale watu waovu waliomtesa Mungu wakati mmoja duniani na adui waliokuwa hawamtii duniani watakuwa tayari wameangamizwa; watakuwa wameangamizwa na majanga makubwa ya siku za mwisho. Baada ya hao watu waovu kuangamizwa kabisa, dunia haitajua tena unyanyasaji wa Shetani. Binadamu watapata wokovu kamili, na hapo tu ndipo kazi ya Mungu itaisha kabisa. Haya ndiyo masharti ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Maangamizo ya mwisho ya wale wana wa uasi pia yatafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Unyakuo wa kweli ni nini?

Aya za Biblia za Kurejelea: “Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki. Kisha mabikira...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp