Unyakuo wa kweli ni nini?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki. Kisha mabikira hao wote wakainuka, na kuzitayarisha taa zao. Na wale wapumbavu wakasema kwa wenye busara, Tupeni mafuta yenu kiasi; kwani taa zetu zimezimika. Lakini wenye busara walijibu, wakisema, La; yasije yakakosa kututosha sisi na ninyi; lakini nendeni kwa wanaouza, na mkajinunulie. Na walipokuwa wameenda kuyanunua, bwana harusi alikuja; na wale waliokuwa tayari walienda naye kwa harusi: na mlango ukafungwa” (Mathayo 25:6-10).
“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).
“Na akaniambia, Andika, Wamebarikiwa wale wanaoitwa katika karamu ya arusi ya Mwanakondoo” (Ufunuo 19:9).
Maneno Husika ya Mungu:
“Kunyakuliwa” si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanavyofikiria. Hili ni kosa kubwa sana. Kunyakuliwa kunarejelea kujaaliwa Kwangu na kuchagua. Kunawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale ambao wamepata hadhi ya mzaliwa wa kwanza, hadhi ya wana, au watu, ni wale wote ambao wamenyakuliwa. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 104
Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!
…………
Leo Umefanya kamili makanisa yote—kanisa la Filadelfia—ambayo ni matunda ya miaka 6,000 ya mpango Wako wa usimamizi. Sasa watakatifu kwa unyenyekevu wanaweza kuwa watiifu mbele Yako; wao wameunganishwa pamoja katika roho na kuandama pamoja katika upendo. Wao wameunganishwa kwa chanzo cha chemchemi ya maji. Maji ya uhai ya maisha huenda bila mwisho na husafisha na kutakasa uchafu wote na taka katika kanisa, kwa mara nyingine tena yakitakasa hekalu Lako. Tumemjua Mungu wa ukweli wa vitendo, tumetembea ndani ya maneno Yake, tumetambua shughuli zetu na wajibu wetu wenyewe, na kufanya kila kitu tunachoweza kutumia kila rasilmali yetu kwa ajili ya kanisa. Tunapaswa kuchukua kila muda kuwa kimya mbele Yako na kutilia maanani kazi ya Roho Mtakatifu ili mapenzi Yako yasizuiwe ndani yetu. Miongoni mwa watakatifu kuna upendano, na nguvu za wengine zitafidia dosari za wengine. Tembea katika roho kila muda na upate nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu; fahamu ukweli na uuweke katika vitendo mara moja; kuwa sawa na nuru mpya na kufuata nyayo za Mungu.
…………
Shirikiana na Mungu kwa utendaji, tumikia kwa uratibu na kuwa moja, yakidhi mapenzi ya Mwenyezi Mungu, harakisha kuwa mwili mtakatifu wa kiroho, kanyaga Shetani, na kumaliza hatima yake. Kanisa la Filadelfia limechukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu na linajidhihirisha katika utukufu wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 2
Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, kushuka Kwake kwa utukufu, mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kuonekana kwa ufalme, na kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, Analeta maafa, Anawazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na Anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake juu kumlaki angani. Wakati wowote tunapowaza kuhusu haya, hatuwezi ila kujawa na hisia na kujawa na shukrani kwa kuwa tulizaliwa siku za mwisho na tuna bahati nzuri ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, tumepata badala yake “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Baraka gani hii! Hamu hii yote, na neema inayopewa na Bwana hutufanya kuingia kwenye maombi kwa kawaida, na hutufanya waangalifu zaidi katika kukusanyika pamoja. Labda mwaka ujao, labda kesho, na tena, labda kwa muda mfupi zaidi kuliko binadamu anavyoweza kung’amua, Bwana ghafla atashuka, akionekana kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa faragha ya hamu. Tunaharakisha ili tuwe mbele ya wenzetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, yote kwa ajili ya kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, ya kuwa miongoni mwa wale watakaonyakuliwa kwenda mbinguni. …
…………
Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia dunia nzima, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Yeye huendesha usimamizi Wake kwa hatua zilizopimwa na kulingana na mpango Wake kwa kimya, na bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake hukaribia, moja baada ya nyingine, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, na baada yake kiti Chake cha enzi mara moja hushuka kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima! Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho huja kati yetu. Yeye ni hekima, Yeye ni haki na uadhama, na Yeye huja kwa ukimya kati yetu, akiwa na mamlaka na akiwa amejawa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote ambacho yuko karibu kufanya. Maisha ya mwanadamu yanaendelea kama awali moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu huishi kati yetu, mwanadamu kama watu wengine, kama mmoja wa wafuasi wasio na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi ya hayo, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. …
…………
Na bado ni huyu mtu wa kawaida, aliyefichika kati ya watu, ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hatupi maelezo yoyote, wala Hatuambii kwa nini amerudi, lakini Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua zilizopimwa, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole na laini mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—lakini hakuna inayompa mwanadamu huruma na kumtia hofu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa tumejaa aibu isiyovumilika, tusijue pa kujificha. …
Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada ya nyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. …
Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huu, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, hatupingi tena kazi Yake na neno Lake, na tunasujudu, mbele Yake. Hakuna tunachotaka zaidi yakufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.
…………
Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu, waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, wale waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na wale maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, lakini sasa tumeshindwa na Yeye. Kutoka kwa Mungu tumepokea uzima, njia ya uzima wa milele. Licha ya mahali ambapo tunaweza kuwa duniani, licha ya mateso na dhiki tunazovumilia, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?