Unafiki ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu anachofanya, akijifanya kuwa mwema, mwenye fadhila, na mzuri. Je, hivyo ndivyo alivyo kwa kweli? Yeye ni mnafiki, na hivyo kila kitu kinachodhihirika na kufichuliwa ndani yake ni cha uongo, yote ni kujifanya—sio hali yake ya kweli. Hali yake ya kweli imefichwa ndani ya moyo wake; haionekani. Watu wasipofuatilia ukweli, kama hawaelewi ukweli, basi nadharia ambazo wamepata zinakuwa nini? Je, zinakuwa maneno ya mafundisho ambayo watu huzungumzia mara nyingi? Watu hutumia haya yanayodaiwa kuwa mafundisho sahihi kujifanya na kujionyesha kuwa wazuri. Popote waendapo, mambo wanayozungumzia, mambo wanayoyasema, na tabia yao ya nje huonekana kuwa sawa na nzuri kwa wengine. Yote yanalingana na fikira na mapendeleo ya mwanadamu. Machoni pa wengine, wao ni wenye kumcha Mungu na wanyenyekevu. Wao wanaweza kuvumilia na kustahamili, na wanaweza kuwapenda wengine na kumpenda Mungu—lakini kwa kweli, yote haya ni ya bandia; yote ni kujifanya tu na namna ya kuficha asili yao. Kwa nje, wao ni waaminifu kwa Mungu, lakini kwa kweli wanajifanya tu ili wengine waone. Wakati ambapo hakuna mtu anatazama, wao sio waaminifu hata kidogo na kila kitu wanachofanya ni cha uzembe. Kwa juujuu, wameacha familia zao na kazi zao, wanajitahidi kwa bidii na hujitumia—lakini kwa kweli wanafaidika kisirisiri kutoka kwa kanisa na kuiba sadaka! Kila kitu wanachofichua kwa nje, tabia yao yote ni bandia! Hii ndiyo maana ya Mfarisayo mnafiki. “Mafarisayo”—watu hawa hutoka wapi? Je, wanajitokeza kati ya wasioamini? Wote hujitokeza kati ya wasioamini. Kwa nini waumini hawa hugeuka kuwa hao? Inaweza kuwa kwamba maneno ya Mungu yaliwafanya wawe namna hiyo? Sababu kuu ya wao kuwa watu kama hao ni ipi? Ni kwamba wamechukua njia mbaya. Wameyachukulia maneno ya Mungu kama chombo cha kujihami nacho; wanajihami na maneno haya na kuyachukulia kama mtaji wa kupata riziki, na kupata kitu bila kutoa chochote. Hawafanyi chochote ila kuhubiri mafundisho ya kidini, ilhali hawajawahi kuyaweka maneno hayo katika vitendo. Watu ambao wanaendelea kuhubiri maneno na mafundisho ya dini licha ya kutowahi kufuata njia ya Mungu ni wa aina gani? Ni Mafarisayo wanafiki. Tabia yao inayokisiwa kuwa nzuri na mwenendo mzuri, hicho kidogo ambacho wameacha na kutumia kimelazimishwa kabisa, yote ni uigizaji tu wanaofanya. Yote ni bandia kabisa; yote ni kujifanya. Katika mioyo ya watu hawa hakuna uchaji kwa Mungu hata kidogo, na hawana hata imani yoyote ya kweli kwa Mungu. Zaidi ya hayo, wao ni wa wasioamini. Watu wasipofuatilia ukweli, watatembea njia ya aina hii, na watakuwa Mafarisayo. Je, hili silo jambo la kuhofisha?

Umetoholewa kutoka katika “Ishara Sita za Ukuaji katika Maisha” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Ufuatiliaji wa tabia nzuri ya juujuu, kisha kufanya kila muwezalo kujibunia kisingizio kwa kutumia sura ya mambo ya roho; kuiga mtu wa kiroho; kutoa sura ya kuthamini mambo ya kiroho katika kile mnachosema, kufanya, na kufichua; kufanya mambo machache ambayo, katika fikra na mawazo ya watu, yanastahili kusifiwa—yote haya ni ufuatiliaji wa mambo ya kiroho kwa njia ya uongo, na ni unafiki. Unasimama juu ukinena maneno na nadharia, ukiwaambia watu wafanye matendo mema, wawe watu wema, na walenge kufuatilia ukweli, lakini katika tabia yako mwenyewe na utendaji wa wajibu wako, hujawahi kutafuta ukweli, hujawahi kutenda kwa mujibu wa kanuni za ukweli, hujawahi kuelewa kile kinachosemwa katika ukweli, mapenzi ya Mungu ni nini, viwango ambavyo Anahitaji kwa mwanadamu ni vipi—hujawahi kuchukulia yoyote haya kwa uzito. Unapokabiliwa na masuala fulani, wewe hutenda kabisa kulingana na mapenzi yako na kumweka Mungu kando. Je, vitendo hivi vya nje na hali za ndani ni kumcha Mungu na kuepukana na uovu? Ikiwa hakuna uhusiano kati ya imani ya watu na ufuatiliaji wao wa ukweli, bila kujali wanamwamini Mungu kwa miaka mingapi, hawataweza kumcha Mungu na kuepukana na uovu kwa kweli. Na kwa hiyo watu kama hao wanaweza kuitembea njia gani? Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa na nini? Je, si ni kwa maneno na nadharia? Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa, wakivalia maneno na nadharia, ili kujifanya kama Mafarisayo zaidi, kama watu ambao hudhaniwa kwamba humtumikia Mungu zaidi? Vitendo hivi vyote ni nini? Wanafanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati; wanapeperusha bendera ya imani na kufanya kaida za dini, wakijaribu kumdanganya Mungu ili kufikia lengo lao la kubarikiwa. Hawamwabudu Mungu hata kidogo.

Umetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kuhusu uaminifu wako hadharani, bali tumia matendo yako halisi ili kuonyesha upendo wako kwa Mungu, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni tabia ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana tabia za kiajabu na heshima, na anaweza kushuhudia kokote aendako; yeye ni yule anayependwa na Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje; lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunjwa. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe, wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Watu wa aina hii ni watu wa dini, na wanafiki pia.

Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu. Wale ambao huzingatia uhalisi huwasilisha vyovyote vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao daima huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwingine anaimba, yeye anaanza kukatika, bila hata kugundua kuwa wali katika sufuria yake umeshaungua. Watu wa aina hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni maonyesho ya ukosefu wa ukweli! Wakati watu wengine wanawasiliana kuhusu masuala ya maisha katika roho, ingawa hawasemi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika uhalisi, si kwa bidii au maonyesho ya nje.

Je, matendo mazuri ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza matakwa ya Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyaruzuku maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo kama hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo matakwa ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, yanayokupendeza yanaweza kuwakilisha yanayompendeza Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama unahisi kuwa wewe ni mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuzungumzia jambo hilo kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unajivuta nadhari kwako mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza matakwa ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima yanaonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mazuri ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Mafarisayo wanafiki na watu wa dini! Msipoacha matendo yenu ya nje na hamuwezi kufanya mabadiliko, basi dalili za unafiki ndani yenu zitazidi kuimarika. Kadiri dalili za unafiki zinavyozidi, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, watu wa aina hii hakika watatupiliwa mbali!

Umetoholewa kutoka katika “Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maisha ya kawaida ya kiroho ni kuishi maisha mbele ya Mungu. Wakati wa kuomba mtu anaweza kutuliza moyo wake mbele ya Mungu, na kwa njia ya sala anaweza kutafuta kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, kujua maneno ya Mungu, na anaweza kuelewa mapenzi ya Mungu. Wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu mtu anaweza kuelewa zaidi na kuwa udhahiri zaidi juu ya ni nini Mungu anataka kufanya sasa hivi, na mtu anaweza kuwa na njia mpya ya matendo na asiwe wa kushikilia ukale, ili matendo ya mtu yote ni kwa lengo la kufanikisha maendeleo katika maisha. Kwa mfano, sala ya mtu si kwa ajili ya kusema baadhi ya maneno mazuri, au kupiga kelele mbele ya Mungu kuonyesha deni ya mtu, bali ni kwa kufanya mazoezi ya kutumia roho ya mtu, kutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu, kufanya mazoezi ya kutafuta uongozi wa maneno ya Mungu katika mambo yote, kufanya moyo wa mtu uwe moyo wa kuvutiwa na mwanga mpya kila siku, kutokuwa wa kukaa tu wala mvivu, na kuingia kwenye njia sahihi ya kutenda maneno ya Mungu. Kwa sasa watu wengi wanalenga mbinu, na hawajaribu kufuata ukweli ili kufikia maendeleo katika maisha; hapa ndipo watu hupotoka. Pia kuna baadhi ya watu ambao, hata kama wao wana uwezo wa kupokea mwanga mpya, taratibu zao hazibadiliki, wao huunganisha fikra za dini za zamani ili kupokea neno la Mungu leo, na wanayoingiza bado ni kanuni ambayo hubeba fikra za dini kwa pamoja, na hawaingiziwi mwanga wa leo kabisa. Kwa hivyo, matendo yao ni machafu wanafanya matendo yale yale kwa jina jipya, na haijalishi matendo yao ni mazuri kiwango gani, bado ni ya unafiki. Mungu huongoza watu kufanya mambo mapya kila siku, na Anahitaji watu kuwa na umaizi mpya na ufahamu mpya kila siku, na si kuwa na mienendo ya zamani au wasiobadilika. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, ila mbinu zako hazijabadilika kamwe, kama bado wewe ni wa shauku na mwenye shughuli nyingi kwa nje, na wala huji mbele za Mungu kufurahia maneno Yake kwa moyo mtulivu, basi hutaweza kupata chochote.

Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watiifu kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu. Watu wanaoonekana watii kama kondoo, lakini mioyo yao inahifadhi nia mbovu, ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, wanamkosea Mungu moja kwa moja, na Mungu hatamwacha hata mmoja. Roho Mtakatifu atamfichua kila mmoja wao, ili wote waweze kuona kwamba kila mmoja wa hao ambao ni wanafiki hakika watachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Usiwe na shaka: Mungu atamshughulikia na kumkomesha kila mmoja.

Umetoholewa kutoka katika “Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kutofautisha kama wachungaji na wazee ni Mafarisayo wanafiki na wapinga Kristo au la hakuwezi kufanywa kwa kuangalia tu jinsi wanavyowatendea watu vizuri kwa nje. Jambo la msingi ni kuangalia jinsi wanavyomtendea Bwana na ukweli. Kwa nje wanaweza kuwa na upendo kwa waumini, lakini wana upendo kwa Bwana? Ikiwa wana upendo kabisa kwa watu lakini wamejawa na uchovu na chuki kwa Bwana na kweli, na kumhukumu na kumshutumu Kristo wa siku za mwishoMwenyezi Mungu, basi wao si Mafarisayo wanafiki? Je, sio wapinga Kristo? Wanaonekana kuhubiri na kufanya kazi kwa bidii nje, lakini ikiwa ni kwa ajili ya kuvikwa taji na kuzawadiwa, basi hii inamaanisha kwamba ni watiifu na waaminifu kwa Bwana? Ili kutofautisha kama mtu ni mnafiki, zaidi unapaswa kuangalia ndani ya mioyo yao na kuona malengo yao. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi kuhusu kutofautisha. Ni baada ya mawasiliano kama hayo tu ndiyo ninaelewa! Mungu huchunguza mioyo ya watu. Hivyo ili kuona kama mtu kweli anampenda na anamtii Bwana, jambo kuu ni kuangalia kama anafanya na kuzingatia neno Lake na kuzingatia amri Zake, na zaidi angalia kama wanamtukuza Bwana Yesu na kushuhudia Bwana Yesu, na ikiwa wanafuata mapenzi ya Mungu. Tunaona kwamba Mafarisayo mara nyingi walieleza Maandiko kwa watu katika masinagogi, walishikilia sheria za Biblia kwa kila kitu, na pia walikuwa na upendo kwa watu. Lakini kwa kweli, kila kitu walichofanya hakikuwa kutenda neno la Mungu au kuzingatia amri za Mungu, lakini ilifanyika kuonekana na watu. Kama Alivyosema Bwana Yesu alipowafunua: “Lakini vitendo vyao vyote huvitenda ili vionekane na watu: hupanua visanduku vyao vya maandishi, na hutanua mapindo ya nguo zao” (Mathayo 23:5). Wao hata walisimama kwa makusudi katika masinagogi na kwenye pembe za mitaani ili kushiriki katika sala ndefu. Wakati wa kufunga wao kwa makusudi walifanya nyuso zao kuangalia huzuni sana, ili watu waweze kujua kuwa walikuwa wanafunga. Walifanya hata kwa makusudi matendo mema mitaani ili watu wote waweze kuona. Hata waliendelea kushikilia mila ya kale na mila ya kidini kama vile “usile kama hujaosha mikono kwa uangalifu.” Kuwadanganya watu kuwasaidia na kuwaabudu, Mafarisayo kuendelea kufanya mambo madogo yaonekane kuwa makubwa ili wajifiche, na waliwaongoza watu tu kushiriki katika ibada za kidini, kuimba na kusifu, au kushikilia mila kadhaa za mababu, lakini hawakuwaongoza watu kutenda neno la Mungu, kushikilia amri za Mungu, na kuingia katika uhakika wa ukweli. Aidha, hawakuwaongoza watu kutenda ukweli na kumtii na kumwabudu Mungu. Yote waliyofanya yalikuwa kutumia vitendo vingine vya nje ili kuwachanganya na kuwadanganya waumini! Wakati Bwana Yesu alikuja kuhubiri na kufanya kazi, kwa ajili ya kulinda hadhi zao na riziki zao, Mafarisayo hawa ambao walijifanya kuwa wacha Mungu kwa hakika waliacha sheria na amri za Mungu waziwazi chini ya kisingizio cha “kulinda Biblia.” Walibuni uvumi, walitoa ushahidi wa uongo, na wakamhukumu kwa ukali na kumsingizia Bwana Yesu, wakifanya yote waliyoweza kuwazuia waumini wasimfuate Bwana Yesu. Mwishowe, hata walishirikiana na wale walio mamlakani kumtundika Bwana Yesu msalabani! Hivyo, unafiki wa Mafarisayo na kuchukia kwao kwa ukweli kulifunuliwa kabisa. Kiini chao cha upinga Kristo hivyo kilifunuliwa kabisa. Hii inaonyesha kwamba kiini cha Mafarisayo kilikuwa na unafiki, kidanganyifu, cha uongo na kiuovu. Wote walikuwa wachungaji wa uongo ambao waliacha njia ya Mungu, waliwadanganya watu na waliwafungia watu! Waliwadanganya na kuwafunga waumini, wakiudhibiti ulimwengu wa kidini kumpinga Mungu, wakikataa kwa ukali, kumshutumu na kumchukia Kristo mwenye mwili. Hii inatosha kuthibitisha kuwa walikuwa wapinga Kristo ambao walitaka kuimarisha utawala wao wenyewe wa kujitegemea!

Sasa tunaona wazi maneno mbalimbali ya unafiki wa Mafarisayo, tunapowafananisha na wachungaji wa kidini na wazee wa leo, je, hatutambua kwamba wao ni kama Mafarisayo? na wote ni watu ambao hawatendi neno la Bwana au kuzingatia amri za Bwana, na zaidi ya hayo si watu wanaomwinua Bwana na kumshuhudia Bwana? Wao ni watu tu ambao wanaamini kwa upofu katika Biblia, kuabudu Biblia, na kuinua Biblia. Wanashikilia tu ibada mbalimbali za dini, kama vile kuhudhuria huduma za mara kwa mara, kesha za asubuhi, kuvunja mkate, kushiriki katika Sakramenti Takatifu, na kadhalika. Wao huwa makini na kuzungumza na watu juu ya kuwa wanyenyekevu, wenye subira, wacha Mungu na wenye upendo, lakini hawampendi Mungu mioyoni mwao, na zaidi ya hayo hawamtii Mungu na hawana moyo unaomwogopa Mungu. Kazi yao na mahubiri yanalenga tu kuendelea na kueleza ujuzi wa Biblia na nadharia ya kiteolojia. Lakini linapokuja suala la jinsi ya kutenda na kujifunza neno la Bwana, jinsi ya kuzingatia amri za Bwana na jinsi ya kueneza na kulishuhudia neno la Bwana, jinsi watu wanapaswa kufuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, jinsi ya kumpenda Mungu kweli, kumtii Mungu, na kumwabudu Mungu, na mambo haya yote ambayo Bwana Yesu anahitaji kwa wanadamu, hawatafuti, wala kuchunguza, na wala hawajui nia za Bwana, na hata hivyo usiwaongoza watu kufanya mazoezi au kuzingatia. Kusudi lao wanazunguka kila mahali wakihubiri ujuzi wa Biblia na nadharia ya kiteolojia ni kujionyesha wenyewe, kujijenga wenyewe, na kuwafanya watu kuwatazamaia na kuwaabudu yao. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu alipokuja kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, hawa wachungaji na wazee, kwa ajili ya kufikia mamlaka ya kudumu katika ulimwengu wa kidini, na kwa tamaa yao kuu ya kuwadhibiti waumini na kujenga ufalme wao wenyewe wa kujitegemea, ilikiuka wazi wazi neno la Bwana Yesu, kubuni uvumi, kuhukumu, kushambulia na kumkufuru Mwenyezi Mungu, kufanya vyovyote ili kuwazuia waumini kutokana na kuchunguza njia ya kweli. Kwa mfano, Bwana Yesu aliwafundisha watu kuwa wanawali wenye busara: Mtu anaposikia mtu akisema “Tazama, anakuja bwana arusi,” anapaswa kwenda kumpokea. Lakini baada ya wachungaji na wazee kusikia habari ya kuja kwa pili kwa Bwana Yesu, wao badala yake walifanya yote waliyoweza kufunga kanisa na kuwazuia waumini wasitafute na kuchunguza njia ya kweli! Bwana Yesu alitufundisha “Mpende jirani yako kama unavyojipend.” Na bado, waliwachochea waumini kukashifu na kuwapiga ndugu ambao wanashuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Bwana Yesu alimwambia mwanadamu asiseme uongo, asishuhudie uongo, lakini wachungaji na wazee walibuni uongo wa kila aina kumtukana Mwenyezi Mungu, na hata kuungana na CCP ya kishetani kupinga, kushutumu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kulipaka tope Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba kile ambacho wachungaji wa kidini na wazee wamesema na kufanya kabisa kinakiuka mafundisho ya Bwana. Wao ni kama Mafarisayo wanafiki. Wao ni watu wote ambao huongoza bila kufikiria, kumpinga Mungu, na kuwadanganya watu.

Umetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana