Watu mara nyingi husema, “Wema una thawabu yake na uovu una adhabu yake,” basi kwa nini Mungu hawaondoi watu wote waovu sasa?

08/03/2020

Aya Husika za Biblia

“Kila kitu kina majira, na muda wa kila madhumuni chini ya mbingu” (Mhubiri 3:1).

“Na jinsi ilivyokuwa katika siku za Nuhu, hivyo ndivyo itakavyokuwa pia katika siku za Mwana wa Adamu. Walikula, walikunywa, walioa, waliolewa, mpaka siku ambayo Nuhu aliingia ndani ya safina, na gharika ikaja, na kuwaangamiza wote.Vile vile pia ilivyokuwa siku za Loti: walikula, wakanywa, walinunua, waliuza, walipanda, walijenga;Lakini siku iyo hiyo ambayo Loti alitoka Sodoma kulinyesha moto na kiberiti kutoka mbinguni, na kuwaangamiza wote.Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika siku ambapo Mwanadamu atafunuliwa”.(Luka 17:26-30).

“Kwa kuwa Mwana wa Adamu atafika katika utukufu wa Babake akiwa na malaika Wake; na kisha Atamtuza kila mwanadamu kulingana na vitendo vyake” (Mathayo 16:27).

“Tazama, Naja upesi; na Nina thawabu Yangu, kumpa kila mwanadamu kulingana na vile matendo yake yatakuwa”.(Ufunuo 22:12).

“Kwa kuwa, tazama, siku inawadia, ambayo itawaka kama joko; na watu wote wenye majivuno, ndiyo, na wote wanaotenda maovu, watageuka makapi: na siku inayowadia itawateketeza, alisema Yehova wa majeshi, kiasi kwamba haitawaachia mzizi wala tawi. … Na mtawakanyaga walio waovu; kwani watageuka majivu chini ya soli za miguu yenu katika siku ambayo nitafanya hili” (Malaki 4:1,3).

Maneno Husika ya Mungu:

Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.” Kauli hii “kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu, wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioamini, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Sasa, bila kujali matendo yao ni yapi, na alimradi tu hawazuii usimamizi wa Mungu na hawafanyi chochote kuhusiana na kazi mpya ya Mungu, watu kama hao hawatapata adhabu inayolingana na matendo yao, kwa kuwa siku ya ghadhabu bado haijatimia. Yapo mengi ambayo watu wanaamini kuwa Mungu angekuwa ameyashughulikia tayari, na wanafikiri kuwa wale watenda maovu wanastahili kuadhibiwa haraka iwezekanavyo. Lakini kwa sababu kazi ya usimamizi wa Mungu bado haijafikia kikomo, na siku ya ghadhabu haijatimia bado, wadhalimu bado wanaendelea kutenda matendo yao maovu. … Sasa si wakati wa adhabu ya mwanadamu, ila ni wakati wa kutekeleza kazi ya ushindi, isipokuwa kama kuna wale wanaoiharibu kazi ya usimamizi wa Mungu, ambao wataadhibiwa kulingana na uzito wa matendo yao kama ni hivyo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Madhumuni ya kazi ya Mungu juu ya mwanadamu ni ili aweze kukidhi mapenzi ya Mungu na yote yamefanywa kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo wakati wa wokovu wake wa mwanadamu Yeye hafanyi kazi ya kumwadibu mtu. Wakati wa wokovu wa mwanadamu, Mungu haadhibu maovu au kulipa mema, wala Yeye hafunui hatima ya aina zote za watu. Badala yake, ni baada tu ya hatua ya mwisho ya kazi Yake kukamilishwa ndipo basi Atafanya kazi ya kuadhibu maovu na kulipa mazuri, na kisha basi ndipo Atafunua mwisho wa aina zote za watu. Wale ambao wanaadhibiwa hakika hawataweza kuokolewa, wakati wale waliookolewa watakuwa wale ambao wamepata wokovu wa Mungu wakati wa wokovu Wake wa mwanadamu. Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, wale wote ambao wanaweza kuokolewa wataokolewa kwa upeo wa juu zaidi, hakuna hata mmoja wao atakayeachwa, kwa kuwa kusudi la kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu wa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia zao, wote ambao hawawezi kumtii Mungu kabisa, wote watakuwa walengwa wa adhabu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya Yeye kumaliza kutekeleza kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp