Kwa nini dunia ni yenye giza na mbovu sana? Kwa kuwa wanadamu wapo katika upeo wa upotovu, inapaswa kuharibiwa?

08/03/2020

1) Kwa nini dunia ni yenye giza na mbovu sana?

Aya Husika za Biblia:

“Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1 Yohana 5:19).

“Nayo nuru hung’aa gizani, wala giza halikuielewa nuru” (Yohana 1:5).

Maneno Husika ya Mungu:

Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu hapo mwanzo wakiwa watu watakatifu, ni kama kusema, katika bustani ya Edeni, walikuwa watakatifu, wasiokuwa na uchafu. Walikuwa watiifu kwa Yehova, na hawakujua chochote kuhusu kuasi Yehova. Hii ni kwa sababu hawakuwa na kusumbuliwa na ushawishi wa Shetani, hawakuwa na sumu ya Shetani, na walikuwa watu wasafi kati ya binadamu wote. Waliishi katika bustani ya Edeni, bila kutiwa najisi na uchafu wowote, bila kuingiliwa na mwili, na heshima kwa Yehova. Baadaye, walipojaribiwa na Shetani, wakawa na sumu ya nyoka, na tamaa ya kuasi Yehova, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hapo mwanzo, walikuwa watakatifu na wenye kuheshimu sana Yehova; hivyo tu ndivyo walikuwa binadamu. Baadaye, baada ya kujaribiwa na Shetani, wakala tunda la maarifa ya kujua mazuri na mabaya, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Waliendelea kupotoshwa na Shetani, na wakapoteza sura asili ya mwanadamu. Hapo mwanzo, mwanadamu alikuwa na pumzi ya Yehova, na hakuwa muasi hata kidogo, na hakuwa na uovu wowote katika moyo wake. Wakati huo, mwanadamu alikuwa binadamu wa kweli. Baada ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu akawa mnyama. Fikra zake zikajawa na uovu na uchafu, bila mazuri ama utakatifu. Je, huyu si Shetani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. … Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika “taasisi za elimu ya juu.” Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope. Hata wanaposikia ukweli, wale wanaoishi gizani hawafikiri kuuweka katika vitendo, na wala kuelekea kumtafuta Mungu hata kama wameuona mwonekano Wake. Jinsi gani wanadamu wapotovu kiasi hiki wawe na nafasi yoyote ya wokovu? Jinsi gani wanadamu waovu kiasi hiki kuishi katika mwanga?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Usiku uingiapo polepole, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au wapi linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu hukaribisha mwanga wa mchana, lakini ikija kwa kulikotoka nuru na jinsi imeliondoa giza la usiku, mwanadamu anajua hata machache na hata ana ufahamu mchache zaidi Mabadiliko haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu kutoka kipindi kimoja hadi kingine, kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine, wakati huu wote yakihakikisha kwamba kazi ya Mungu katika kila kipindi na mpango Wake wa kila enzi unatekelezwa. Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili. Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

2) Kwa kuwa wanadamu wapo katika upeo wa upotovu, inapaswa kuharibiwa?

Aya Husika za Biblia:

“Naye Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.Naye Mungu akasema kwake Nuhu, Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia” (Mwanzo 6:12-13).

“Na jinsi ilivyokuwa katika siku za Nuhu, hivyo ndivyo itakavyokuwa pia katika siku za Mwana wa Adamu. Walikula, walikunywa, walioa, waliolewa, mpaka siku ambayo Nuhu aliingia ndani ya safina, na gharika ikaja, na kuwaangamiza wote.Vile vile pia ilivyokuwa siku za Loti: walikula, wakanywa, walinunua, waliuza, walipanda, walijenga;Lakini siku iyo hiyo ambayo Loti alitoka Sodoma kulinyesha moto na kiberiti kutoka mbinguni, na kuwaangamiza wote.Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika siku ambapo Mwanadamu atafunuliwa” (Luka 17:26-30).

“Wakati waovu wanachipuka kama nyasi, na wakati wote wanaotenda uovu wanafanikiwa; ni ili waangamizwe daima” (Zaburi 92:7).

“Na itatimia, kuwa katika nchi nzima, alisema Yehova, sehemu mbili hapo ndani zitakatwa na watakufa; lakini ya tatu itawachwa humo. Na nitaileta sehemu ya tatu na kuipitisha kwa moto, na nitawasafisha jinsi fedha isafishwavyo, na kuwajaribu jinsi dhahabu ijaribiwavyo; wataliita jina Langu, na nitawasikia: Nitasema, ni watu Wangu, nao watasema, Yehova ni Mungu wangu” (Zekaria 13:8-9).

Maneno Husika ya Mungu:

Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.” Kauli hii “kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu, wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioamini, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Wanadamu walikuwa wapotovu sana, walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanatunzwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa waasherati kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko wa kutisha. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo zaidi, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Wakati binadamu walikuwa wamejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake, na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza binadamu hao. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi. Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwaangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu. Hivyo ni nini ambacho Mungu alifanya kwenye kipindi hiki kabla ya kuangamiza wanadamu? Mungu alifanya kiwango kikubwa cha kazi ya kukumbusha na kazi ya kusihi. Haijalishi ni maumivu kiasi kipi na huzuni ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Mungu, Aliendelea kufanyisha zoezi utunzaji Wake, wasiwasi, na huruma nyingi juu ya binadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Kunacho mpaka kwa subira ya Mungu kwa upotovu, uchafu, na vurugu la binadamu. Anapofikia ule mpaka, Hatawahi tena kuwa na subira na badala yake Ataanza usimamizi Wake mpya na mpango mpya, kuanza kufanya kile ambacho lazima Afanye, kufichua matendo Yake na upande ule mwingine wa tabia Yake. Kitendo hiki Chake si cha kuonyesha kwamba lazima Asiwahi kukosewa na binadamu au kwamba Yeye amejaa mamlaka na hasira, na wala si kuonyesha kwamba Anaweza kuangamiza binadamu. Ni kwamba tabia Yake na kiini chake takatifu ambacho hakiwezi tena kuruhusu, hakina tena subira kwa aina hii ya binadamu kuishi mbele Yake, kuishi chini ya utawala Wake. Hivyo ni kusema, wakati wanadamu wote wako dhidi Yake, wakati hakuna mtu yeyote Anayeweza kuokoa katika ulimwengu mzima, Hatakuwa tena na subira kwa binadamu kama hawa, na Ataweza, bila ya utundu wowote, kutekeleza mpango Wake—kuangamiza binadamu wa aina hii. Kitendo kama hicho cha Mungu kinaamuliwa na tabia Yake. Hii ni athari inayohitajika, na athari ambayo kila kiumbe aliyeumbwa chini ya utawala wa Mungu lazima ashuhudie.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. Anaweza kuonyesha hasira Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Mungu hulalamikia wakati ujao wa wanadamu, huhuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu na anaumizwa kwamba binadamu wanatembea, hatua baada ya nyingine hadi kuoza na katika njia ambayo hawawezi kurudi. Wanadamu ambao wameuvunja moyo wa Mungu na wakamkana kumfuata yule mwovu: je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaza kuhusu mwelekeo ambao wanadamu wa aina hii huenda wanafuata? Ni kwa sababu hii haswa kwamba hakuna anayehisi hasira ya Mungu, hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuja karibu na Mungu na isitoshe, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mwenyewe, anazidi kwenda mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli Wake, akiona heri kujiuza kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amefikiri—iwapo mwanadamu ataendelea kuwa mkaidi—jinsi Mungu atakavyowatendea wanadamu hawa ambao wamempuuza bila kusita? Hakuna anayejua kwamba maana ya ukumbusho wa mara kwa mara na kusihi kwa Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa yasiyokuwa ya kawaida ambayo ameandaa, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Maafa haya siyo tu adhabu ya mwili bali pia ya roho. Unafaa kujua hili: Mpango wa Mungu utakaposhindikana na wakati makumbusho Yake na kusihi Kwake hakutapata majibu yoyote, atatoa hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, majanga haya hayana mengine ya kulinganishwa nalo awali na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu ni mpango wa Mungu kuumba wanadamu mara hii moja tu na kuwaokoa wanadamu mara hii moja tu. Hii ndiyo mara ya kwanza na pia ni ya mwisho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp