Katika miaka ya hivi karibuni, makundi ya kidini na madhehebu mbalimbali katika ulimwengu wa kidini yamekosa matumaini zaidi na zaidi, watu wamepoteza imani yao ya asili na upendo na wamekuwa hasi zaidi na zaidi na dhaifu. Pia tunahisi kunyauka kwa roho na tunahisi kuwa hatuna chochote cha kuhubiri na kwamba sote tumepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Tafadhali tuambie, kwa nini ulimwengu wote wa kidini umekosa matumaini hivyo? Mungu kweli anauchukia na umetelekezwa na Mungu? Tunafaaje kuelewa laana ya Mungu ya ulimwengu wa kidini katika Kitabu cha Ufunuo?

09/06/2019

Jibu:

Sasa, dunia nzima ya dini inakumbwa na ukiwa ulioenea pote, isiyo na kazi ya Roho Mtakatifu, na imani na upendo wa watu wengi umepungua—hili tayari limekuwa ukweli unaokubalika. Nini hasa ni sababu ya msingi ya ukiwa katika jumuiya ya dini ni swali ambalo sisi wote lazima tulielewe kikamilifu. Kwanza, hebu tuangalie nyuma kwa muda kwa mbona hekalu liligeuka la ukiwa katika siku za baadaye za Enzi ya Sheria, na kisha tutaweza kuelewa kikamilifu sababu ya ukiwa wa dunia ya dini katika siku za mwisho. Katika siku za baadaye za Enzi ya Sheria, viongozi wa Kiyahudi hawakuzifuata amri za Mungu Waliitembea njia yao wenyewe na kumwasi Mungu; hii ndiyo sababu kuu ambayo ilisababisha ukiwa wa hekalu moja kwa moja. Bwana Yesu aliwafunua na kuwakemea Mafarisayo akisema: “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, nyinyi wanafiki! Kwani nyinyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, ambayo kwa nje yanaonekana mazuri sana, lakini ndani yake mna mifupa ya wafu, na yenye uchafu wote. Hata hivyo ninyi pia mnaonekana wenye haki kwa wanadamu, lakini ndani yenu mmejaa unafiki na dhambi(Mathayo 23:27-28).

Ole wenu, ninyi waandishi na Mafarisayo, wazandiki! kwa sababu mnajenga makaburi ya manabii, na kupamba makaburi ya wenye haki, Na kusema, iwapo tungelikuwa katika siku za baba zetu, hatungelishiriki na wao kuwaua manabii. Kwa nini mnakuwa mashahidi kwenu wenyewe, kuwa ninyi ni wana wa hao ambao waliwaua manabii. Basi kijazeni kiwango cha baba zenu. Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu? Hivyo, tazama, natuma kwenu manabii, na wanadamu wenye busara, na waandishi: na mtauwa na kusulubisha baadhi yao; na mtawacharaza baadhi yao katika masinagogi yenu, na kuwatesa kutoka mji mmoja hadi mji mwingine: Ili damu yote yenye haki iliyomwagika duniani iweze kuwa juu yenu, kuanzia damu ya Habili aliyekuwa mwenye haki hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia, ambaye mlimwua katikati ya hekalu na madhabahu. Kweli nawaambieni, Mambo haya yote yatakifuata kizazi hiki(Mathayo 23:29-36).

Akajibu na kuwaambia, Isaya ametabiri vizuri kuhusu ninyi wazandiki, jinsi ilivyoandikwa, Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, bali mioyo yao iko mbali na mimi. Hata hivyo, wananiabudu bure, wakifundisha mafundisho ambayo ni amri za wanadamu. Kwa kuiweka kando amri ya Mungu, mnashikilia desturi ya wanadamu, kama kuosha vyungu na vikombe: nanyi mnafanya mambo mengine mengi kama haya. Naye akawaambia, Mnakataa kabisa amri ya Mungu, ili mweze kuizingatia desturi yenu wenyewe(Marko 7:6-9).

Inaweza kuonekana kwa dhahiri kutoka kwa maneno ya Bwana Yesu ambayo yaliwafunua Mafarisayo, kwamba matendo ya makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo yalimwasi Mungu na kumpinga. Yalikiuka sheria na amri za Mungu wakifuata tu desturi za dini. Hili linatosha kudhibitisha kwamba wao kumtumikia Mungu kulikuwa kwa kweli kumwasi, na kulienda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hasa wakati wa maonyesho na kazi ya Bwana Yesu, walimshutumu na kumwasi kwa nguvu nyingi, na kiini na asili yao vilifunuliwa kikamilifu. Inaweza kuonekana basi kwamba sababu kuu iliyosababisha ukiwa wa Uyahudi ilikuwa kwamba makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo walimwasi Mungu na kumpinga. Nyingine ilikuwa kwamba kazi ya Mungu tayari ilikuwa imehama. Bwana Yesu mwenye mwili alikuwa ameanzisha kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema nje ya hekalu. Yaani, kazi ya Mungu iliendelea mbele kwa msingi wa kazi ya Enzi ya Sheria, na kiini cha kazi ya Mungu kiliendelea katika kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Mara Bwana Yesu alipoanza kazi Yake ya ukombozi, Enzi ya Neema ilianzishwa na Enzi ya Sheria kukamilishwa. Wale waliomkubali Bwana Yesu tu ndio waliokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao na walikuwa na mwongozo wa Bwana, ilhali wale waliobaki katika hekalu, waliomtupa Bwana Yesu kando, kumwasi na kumshutumu, kwa kawaida walitelekezwa na kazi ya Mungu, wakianguka katika giza na kupitia laana na adhabu ya Mungu. Kwa hivyo, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba ukiwa wa dunia ya dini wakati wa Enzi ya sheria hakika ulisababishwa na mwanadamu na ulikuwa kabisa kwa sababu viongozi wa dini walipotoka kutoka katika njia ya Bwana, hawakuzifuata amri za Bwana, waliyaasi mapenzi ya Mungu na kujiweka kama maadui wa Mungu. Kama viongozi wa Kiyahudi wangekuwa na uwezo wa kushikilia njia ya Bwana na kuzifuata amri za Bwana, Bwana Yesu bado angeenda nyikani kuhubiri na kufanya kazi? Bado Angeenda miongoni mwa wasioamini kuwatafuta wale ambao wangemfuata Mungu? Bila shaka la. Bwana Yesu hakika angeenda kwanza katika hekalu na katika masinagogi kuhubiri, akionekana kwa mwanadamu na kufanya kazi Yake. Hivyo kwa nini Bwana Yesu hakufanya hili? Ni dhahiri, ilikuwa kabisa kwa sababu wale waliokuwa ndani ya hekalu na ndani ya masinagogi hawakumkubali Bwana Yesu, lakini badala yake walimshutumu na kumwasi, hata kuenda kila mahali kujaribu kumkamata. Kwa sababu ya hili, Bwana Yesu hakuwa na chaguo ila kuenda nyikani kuhubiri na kufanya kazi na kuenda miongoni mwa wasioamini kuwatafuta wale ambao wangemfuata. Watu wote wenye akili wanaweza kuona ukweli huu kwa dhahiri.

Sasa kwa kuwa tunaelewa sababu ya ukiwa wa dunia ya dini katika siku za baadaye za Enzi ya Sheria, hebu tuangalie sababu ya ukiwa wa dunia ya dini katika siku za mwisho. Sote tunaweza kuona kwamba wachungaji na wazee wa dunia ya dini katika siku za mwisho hasa wanachukulia kuhubiri maarifa ya Biblia na nadharia za teolojia kama aula yao ndani ya makanisa. Mara kwa mara wanatumia ufasiri wa maandiko kujishaua na kujionyesha ili wengine wawaabudu, na hawafuati maneno au amri za Bwana Yesu na hawafuati njia ya Bwana. Wanahubiri kwa nadra kuhusu kuingia katika maisha, na hawawaongozi watu kutenda au kupitia maneno ya Bwana kamwe kwa njia ambayo itawapa ufahamu wa ukweli na maarifa ya Bwana. Hili huwasababisha waumini wote katika jumuiya za dini kupotoka kutoka katika njia ya Bwana. Hata huenda wakawa wamemwamini Bwana kwa miaka mingi, lakini yote wanayoelewa ni maarifa ya biblia tu na nadharia ya teolojia; hawana maarifa ya Bwana hata kidogo, na hawana uchaji au utii Kwake. Wamepotoka kabisa kutoka kwa maneno ya Bwana na kuwa watu wanaomwamini Bwana lakini hawamjui, na ambao wanaweza kumwasi na kumsaliti Bwana. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba viongozi wa dunia ya dini wamepotoka kabisa kutoka katika njia ya Bwana, ambayo imesababisha wao kupoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupoteza baraka za Mungu; inaweza kusemwa kwamba hii ndiyo sababu ya msingi ya ukiwa wa dunia ya dini. Sababu nyingine ni kwamba kazi ya Mungu imehama na Bwana Yesu tayari amerudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili akifanya kazi ya hukumu akianzia katika nyumba ya Mungu inayotegemezwa kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Ameanzisha Enzi ya Ufalme na kukamilisha Enzi ya Neema. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu kimehamishwa katika kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, na ni wale tu wanaomkubali Mwenyezi Mungu ndio watakaokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na kuweza kufurahia ugavi wa maji hai ya uzima yanayotiririka kutoka katika kiti cha Mungu cha enzi. Wale ambao hawawezi kuwa na kasi sawa na kazi ya Mungu ya sasa na wanaokataa kumkubali Mwenyezi Mungu wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na wameanguka katika giza. Wachungaji na wazee wa dunia ya dini hasa, wakikabiliana na kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, hawaitafuti na kuichunguza tu, lakini pia wanampinga na kumshutumu Mungu kwa shauku, wakieneza kila aina ya uvumi na uongo kudanganya na kuwadhibiti waumini, na kuwazuia watu kutafuta na kuichunguza njia ya kweli. Waliikera tabia ya Mungu kitambo na kupata chuki na laana ya Mungu, hivyo wanawezaje kukosa kutelekezwa na kuondolewa na Mungu? Sasa tumeona kwamba baada ya kuonekana kwa miezi minne ya damu maafa makuu yatakuwa karibu sana kutendeka. Wale wote ambao hawajamkubali Mwenyezi Mungu hakika wataanguka katika maafa na hapo watapitia kuadibu na usafishaji, wakati wale ambao wamemkubali Mwenyezi Mungu watakuwa wale wanaonyakuliwa kabla ya maafa. Wale ambao hawajamkubali Mwenyezi Mungu wanaweza kuanguka tu katika maafa na kungoja kunyakuliwa baada ya maafa. Je, watu kama hawa hawatatelekezwa na kuondolewa na Bwana? Baada ya maafa, ni watu wangapi wanaoweza kuwa wamebaki wa kunyakuliwa? Sasa, karibu dunia nzima ya dini iko chini ya udhibiti wa kundi la wachungaji na viongozi wanaochukia ukweli na kujiweka kuwa maadui wa Mungu, kwa hivyo inawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu katika hali hii? Na ingeepuka vipi kuwa yenye ukiwa? Hii ndiyo sababu ya msingi ya ukiwa wa dunia ya dini.

Sasa tunaelewa sababu ya msingi ya ukiwa wa dunia ya dini, ambayo ni kwamba viongozi wa dunia ya dini hawafuati maneno ya Bwana, lakini kinyume chake wamepotoka kutoka kwa njia Yake, hawafuati amri Zake, wamekiuka mapenzi ya Mungu kabisa na kuwa watu wanaomwasi Mungu. Pili, kwa sababu viongozi wa dunia ya dini wamekuwa watu wanaomwasi Mungu na hakuna mmoja wao anayeweza kukubali au kutii kazi ya Mungu, Mungu iameihamisha kazi Yake, na dunia ya dini imepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kuanguka katika giza. Mbona, wakati Bwana Yesu alifanya kazi Yake wakati huo, Hakuhubiri hekaluni? Ilikuwa kwa sababu makuhani wote na wazee katika hekalu walikuwa watu waliomwasi Bwana. Kama Bwana Yesu angeingia katika hekalu, Angetupwa kando na kushutumiwa tu, au kukamatwa mara moja na kusulubiwa—huo si ukweli? Hii ndiyo sababu ya msingi ya Mungu kuhamisha kazi Yake. Kama makuhani na wazee katika hekalu wangeweza kukubaliana na maneno ya Bwana na kumtumikia Mungu kulingana na mapenzi Yake, hekalu lingekuwaje lenye ukiwa? Na Mungu angehamishaje kazi Yake? Je, hali siyo hii? Ukiwa wa dunia ya dini pia unakamilisha kabisa unabii katika Biblia: “Na pia nimeizuia mvua isije kwenu, ilipokuwa miezi mitatu kabla ya wakati wa mavuno: Na nimefanya kunyeshe katika mji mmoja, na kufanya kusinyeshe katika mji mwingine: kulinyesha katika sehemu moja, na sehemu ambayo haikunyesha ikanyauka. Basi watu kutoka miji miwili au mitatu wakazurura kuingia mji mmoja, ili kunywa maji; lakini hawakutosheka: hata hivyo hamjanirudia. Atamka Yehova” (Amosi 4:7-8). “Tazama, siku zinafika, alisema Bwana Yehova, ambapo nitaileta njaa ardhini, sio njaa ya ukosefu wa chakula, au kiu ya maji, ila ya kutoyasikia maneno ya Yehova(Amosi 8:11). Kutoka kwa vifungu hivi viwili vya andiko tunaweza kuelewa kwamba “mji mmoja” katika “kunyeshe katika mji mmoja” inahusu kanisa ambapo Mungu mwenye mwili huonekana na kufanya kazi Yake, na “mji mwigine” katika “kusinyeshe katika mji mwingine” kwa kawaida inahusu dunia ya dini ambayo haitii maneno ya Mungu, haifuati amri za Mungu, na ambayo hukataa, kuasi na kushutumu maonyesho na kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu husababisha njaa kuifikia dunia ya dini ili kuwalazimisha wale walio katika dini wanaomwamini Mungu kwa dhati na kupenda ukweli kuiacha, kuzitafuta nyayo za kazi ya Mungu, kutafuta kile ambacho Roho Mtakatifu anasema kwa makanisa yote na kutafuta maonyesho na kazi ya Mungu. Wale wote wanaoisikia sauti ya Mungu na wanaokubali na kuitii kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni wanawali wenye busara na ni wale wanaoinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Watu hawa wote wanahudhuria sherehe ya harusi ya Mwanakondoo na kufurahia ruzuku ya maji hai ya uzima yanayotiririrka kutoka katika kiti cha Mungu cha enzi; imani yao ya asili na upendo umerejeshwa. Wanajifunza kula na kunywa maneno ya Mungu, wapitia maneno ya Mungu na kuyaweka katika vitendo, na watafikia ufahamu wa ukweli na kuingia katika uhalisi. Mara watu wanapouelewa ukweli na wana ufahamu wa kweli wa Mungu, wataweza kumcha Mungu na kumtii, na kwa njia hii kupata maisha mapya kutoka kwa Mungu! Haya mashirika yote ya dini au watu wasioikubali kazi ya Mwenyezi Mungu wanachukiwa sana, kukataliwa na kuondolewa na Mungu, na hawana kazi ya Roho Mtakatifu—hili ni bila shaka yoyote! Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili). “Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?).

Tunaona wazi kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba Mungu hajawahi kuwatupa wale wanaomwamini kwa dhati na wanaotamani sana maonyesho Yake. Kupitia uenzi Wake na hekima, Mungu huwaokoa wale wanaomwamini kwa dhati ili waweze kujinasua kutoka kwa minyororo na udhibiti wa wapinga Kristo na wanadamu waovu wa dunia ya dini, na Anawasababisha wainuliwe mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kukubali hukumu, utakaso na ukamilishaji wa maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho hufanya kazi Yake ya hukumu na kuonyesha ukweli wote unaowatakasa na kuwaokoa wanadamu, ili kikundi cha washindi kiweze kufanywa kabla ya maafa, haya yakiwa malimbuko Yake. Hili linatimiza unabii katika Kitabu cha Ufunuo: “Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo(Ufunuo 14:4). Baada ya kikundi hiki cha washindi kufanywa na Mungu, hatua ya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu inayofanywa na Mungu mwenye mwili itatamatishwa kwa muda, baada ya hapo Mungu atashusha chini maafa makubwa ili kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Wakati huo, wale wote ambao hawajakubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, wanaoshutumu na kumwasi Mwenyezi Mungu, wote wataanguka katika maafa na watapitia humo usafishaji wa kuhukumiwa na kuadibiwa. Tukiacha dini tu, kuwa wenye kasi sawa na nyayo za Mwanakondoo, kukubali na kutii kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, na kupitia hukumu na utakaso mbele ya kiti cha Kristo, ndiyo tunaweza basi kukamilishwa na Mungu kuwa washindi. Ni hapo tu ndipo tutanusurika kutoka kwa majaribu wakati wote chini ya mbingu watalazimika kupitia majaribu. Washindi hawa tu ambao wamefanywa na Mungu—haya malimbuko—ndio wanaostahili kurithi ahadi na baraka za Mungu! Mungu sasa tayari amefanya kikundi cha washindi katika China Bara, na maafa makuu yakiwa karibu, wale wote wanaomshutumu na kumwasi Mwenyezi Mungu wataanguka katika maafa na kuadhibiwa, wakipoteza milele nafasi yoyote ya kuokolewa.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Kwa kweli, historia ya jumuiya ya dini ya upinzani kwa Mungu inakwenda nyuma angalau hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Mungu alipokuwa mwili na kufanya kazi Yake kwa mara ya kwanza wakati wa Enzi ya Neema, jumuiya ya dini ilikuwa tayari imechukuliwa madaraka na Mafarisayo na wapinga Kristo muda mrefu uliopita. Ilikuwa nguvu ya upinzani kwa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Wakati ambapo Mwenyezi Mungu, Kristo siku za mwisho, Anaonekana na kufanya kazi Yake, wale katika jumuiya ya dini bado wanasimama kama maadui wa kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Licha ya kumlaani na kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa ulokole tu wanashirikiana na utawala wa kishetani wa CCP kuwatesa na kulikandamiza Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wametenda dhambi mbaya sana ya kumsulubisha Mungu msalabani tena! Bwana Yesu hakuwalaani Mafarisayo tu, akifichua giza la jumuiya ya dini, ila pia Mwenyezi Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, bado alifunua kiini cha kweli cha wachungaji na wazee wa kansia: upinzani wao kwa Mungu. Aidha, Aliwalaani wapinga Kristo ambao mara nyingine tena walimsulubisha Mungu msalabani. Hili kweli linachochea fikra! Mara zote Mungu alifanyika mwili, Aliilaani na kuishutumu jumuiya ya dini. Hii inaonyesha nini? Wateule wa Mungu hatimaye wanaelewa kwamba jumuiya ya dini, Babeli ulio mkuu, unatakiwa kuanguka. Jumuiya ya dini inaamini katika Mungu kwa jina tu, lakini kamwe haimtukuzi Mungu kwa kweli au kuwa na ushuhuda Kwake. Wao bila shaka hawatekelezi mapenzi Yake. Hawawezi kuwaleta wateule wa Mungu kwenye kiti Chake cha enzi. Wao hakika hawawezi kuwaongoza kwenye njia sahihi, ili waweze kuelewa ukweli na kumjua Mungu kwa kutenda na kupitia maneno Yake. Viongozi wa dini huenda kabisa kinyume na mapenzi ya Mungu. Wao wenyewe hawatendi ukweli, lakini huhubiri maarifa ya kibiblia na nadharia ya kiteolojia ili kuringa na kufanya watu wawaheshimu na kuwaabudu. Wao huongoza waumini kwenye njia ya unafiki ya Mafarisayo. Wao huumiza na kuharibu wateule wa Mungu. Hii inatosha kuthibitisha kwamba viongozi wa dini wote wamekuwa zana za Shetani, wapinga Kristo halisi. Wakati wa hatua tatu za kazi Yake ili kuokoa wanadamu, Mungu amefanyika mwili mara mbili ili kuwakomboa wanadamu na kuokoa ubinadamu. Jumuiya yote ya dini ni maadui wa Kristo; wamekuwa vikwazo kwa kazi ya Mungu ya wokovu. Wamemsulubisha Mungu mara mbili na wameuvunja moyo wa Mungu; wameikosea tabia ya Mungu na walilaaniwa na kuadhibiwa na Yeye kutokana na hayo. Ni kama vile unabii unasema, “Babeli mkuu umeanguka, umeanguka, na umekuwa makazi ya pepo, ngome ya kila pepo mwovu(Ufunuo 18:2), “Babeli umeanguka, umeanguka, mji ule mkubwa, kwa sababu uliwafanya mataifa yote kunywa kutoka kwa mvinyo wa hasira ya uasherati wake(Ufunuo 14:8), “Ole, ole ule mji mkuu Babeli, ule mji ulio na uwezo! kwani hukumu yako imekuja katika saa moja(Ufunuo 18:10).

Hebu tuangalie jinsi Mwenyezi Mungu anawalaani hawa wapinga Kristo ambao hupinga Mungu kwa ulokole na jumuiya ya dini inayodhibitiwa na wapinga Kristo. Mwenyezi Mungu asema, “Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote).

Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote).

Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Dunia inaanguka! Babeli imelemaa! Dunia ya kidini—itakosa kuharibiwa vipi na mamlaka Yangu duniani? Ni nani bado anathubutu kuniasi na kunipinga? Waandishi? Wakuu wote wa kidini? Viongozi na wenye mamlaka wa duniani? Malaika? Ni nani asiyesherehekea ukamilifu na wingi wa mwili Wangu? Miongoni mwa watu wote, nani asiyeimba sifa Zangu bila kukoma, ni nani asiye na furaha isiyoshindwa?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22).

Kila sentensi ya maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, ina mamlaka na nguvu; inaonyesha kabisa mtakatifu, haki na tabia ya Mungu isiyokosewa. Wale ambao humpinga Mungu, hukatiza au kuvuruga kazi ya Mungu bila shaka watapokea adhabu na rada kutoka kwa Mungu. Hili linaamuliwa na tabia ya Mungu ya haki! Sote tunajua, katika Enzi ya Sheria, raia wa Sodoma walimkana Mungu hadharani na kumpinga. Walighadhabisha tabia Yake na wote waliangamizwa na Mungu; walishushwa na kuwa bure. Wakati wa Enzi ya neema, wakuu wa makuhani, waandishi na Mafarisayo wa Kiyahudi walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu hadharani. Walikula njama na serikali ya Kirumi kumsulubisha Bwana Yesu msalabani. Walifanya dhambi kubwa ambayo ilichokoza tabia ya Mungu. Taifa zima la Kiyahudi lilipatwa na uharibifu usiowahi kutokea. Katika siku za mwisho viongozi wa dini humkumu, humpinga na kumlaani Mwenyezi Mungu kwa ukorofi. Wao hata hushirikiana na kula njama na ibilisi CCP kuwakomesha, kuwakamata na kuwatesa wale ndugu ambao hueneza injili ya ufalme. Walifanya dhambi mbaya sana ya kukufuru dhidi Roho Mtakatifu na kumsulubisha Mungu tena msalabani muda mrefu uliopita. Tabia yao yenye uovu ni mbaya zaidi kuliko ile ya watu wa Sodoma. Ni mbaya zaidi kuliko ile ya Mafarisayo wa Kiyahudi kiasi cha kutolinganishwa. Wao ni wapinga Kristo waliofunuliwa na kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho. Wao ni nguvu ya uovu ya dini ambayo imempinga Mungu vibaya zaidi na kwa ulokole kuliko yoyote nyingine katika historia! Jumuiya ya dini inajumuisha kabisa majeshi ya uovu ambayo hupinga Mungu. Ni maficho ya pepo wanaompinga Kristo. Ni ngome madhubuti ambayo hujaribu kushindana na ufalme wa Kristo kama iliyo sawa. Wao ni kambi ya kishetani ya maadui wa jadi wa Mungu ambao huasi dhidi Yake kwa ukaidi! Tabia ya Mungu yenye haki haiwezi kukosewa. Utakatifu wa Mungu hauwezi kuchafuliwa! Kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni mwanzo wa enzi mpya na mwisho wa ile ya zamani. Jumuiya ya dini ambayo inadhibitiwa na kila aina ya pepo wanaompinga Kristo na ulimwengu huu wenye uovu, itaangamizwa hivi karibuni na msiba wa Mungu katika siku za mwisho. Adhabu ya haki ya Mungu tayari imefika! Ni kama vile Mwenyezi Mungu asemavyo, “Dunia inaanguka! Babeli imelemaa! Dunia ya kidini—itakosa kuharibiwa vipi na mamlaka Yangu duniani?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22).

Wale wote wasiokubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, bila kujali wanalitunza jina la Bwana Yesu jinsi gani katika jumuiya ya dini, bila kujali jinsi wanavyofuata Biblia, wokovu wa msalaba au sherehe za dini, bila kujali jinsi wanavyojitahidi, kuteseka kwao au dhabihu, wasipotubu na kumgeukia Mwenyezi Mungu, wataangushwa na kuangamizwa pamoja na wengine wa jumuiya ya dini. Mungu aliamua hili kitambo; hakuna mtu anayeweza kulibadilisha! Mungu aliwaita wateule Wake kitambo katika unabii wa Ufunuo, “Ondokeni kwake, watu wangu, ili msiwe washiriki wa dhambi zake, na ili msipate tauni yake(Ufunuo 18:4).

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp