Unashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye mwili ambaye kwa sasa anafanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Lakini wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanasema kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu kwa kweli ni kazi ya mwanadamu, na pia watu wengi ambao hawamwamini Bwana Yesu wanasema kuwa Ukristo ni imani katika mtu. Bado hatuwezi kutambua hasa ni nini tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, hivyo tafadhali shiriki hili kwa ajili yetu.

08/06/2019

Jibu:

Kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu bila shaka ni tofauti. Tukichunguza kwa makini sote tutaweza kuliona. Kwa mfano, tukiangalia matamshi na kazi ya Bwana Yesu na kisha tuangalie maneno na kazi ya mitume, tunaweza kusema kuwa tofauti ni wazi kabisa. Kila neno lililotamkwa na Bwana Yesu ni ukweli na lina mamlaka, na linaweza kufunua mafumbo mengi. Haya yote ni mambo ambayo mwanadamu kamwe hawezi kufanya. Hiyo ndio maana kuna watu wengi sana wanaomfuata Bwana Yesu, ilhali kazi ya mitume inaweza tu kueneza injili, kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na kutoa kwa kanisa. Matokeo ni machache sana. Tofauti katika ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ni wazi sana. Basi, ni kwa nini watu hawawezi kuitambua? Sababu ni nini? Ni kwa sababu wanadamu wapotovu hawajui Mungu na hawana ukweli wowote. Kwa hivyo, inasababisha mwanadamu kutojua tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, na hufanya kuwa rahisi kuchukulia kazi ya Mungu mwenye mwili kama kazi ya mwanadamu na hufanya kuwa rahisi kuchukulia kazi ya mwanadamu tunayempenda na kazi ya pepo waovu, kazi ya Makristo wa uongo na manabii kama kazi ya Mungu ya kukubaliwa na kufuatwa. Huku ni kukengeuka kutoka kwa njia ya kweli na kumpinga Mungu, na inachukuliwa kama kumpenda mwanadamu, kumfuata Shetani na kumwabudu Shetani. Ni kosa kubwa sana dhidi ya tabia ya Mungu na italaaniwa na Mungu. Watu kama hawa watapoteza fursa ya kuokolewa. Hiyo ndio maana swali lako ni muhimu sana kwa watu wanaochunguza njia ya kweli na kwa kufahamu kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Kutoka nje, kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu zote zinaonekana kama mwanadamu anafanya kazi na anaongea. Lakini kuna tofauti kubwa katika kiini chao na asili ya kazi yao. Leo, Mwenyezi Mungu amekuja na kufunua ukweli wote na mafumbo na amefunua tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Ni sasa tu ambapo tuna ufahamu na utambuzi wa kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Hebu tuangalie maneno ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mitindo ya kazi ya Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu).

Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. …

Maneno ya Mungu mwenye mwili yanaanzisha enzi mpya, yanaongoza wanadamu wote, yanafichua mafumbo, na kumwonyesha mwanadamu mwelekeo mbele katika enzi mpya. Nuru anayoipata mwanadamu ni utendaji au elimu rahisi. Haiwezi kuelekeza binadamu wote kuingia enzi mpya au kufichua fumbo la Mungu Mwenyewe. Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu yuko na dutu ya Mungu, na mwanadamu yuko na dutu ya mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Mungu mwenye mwili ana tofauti kubwa na wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya uungu, lakini wanadamu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu huongea binafsi kuzindua enzi mpya na kuleta mwanadamu kwenye mwanzo mpya. Wakati Yeye Amemaliza kuongea, hili linaashiria kwamba kazi ya Mungu katika uungu Wake imekamilika. Baada ya hapo, wanadamu wote hufuata mwongozo wa wale ambao wametumiwa na Mungu kuingia katika uzoefu wa maisha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu).

Kile ambacho Mungu anaonyesha ndivyo hivyo Mungu Mwenyewe alivyo, na hii ni nje ya uwezo wa mwanadamu, yaani, nje ya uwezo wa kufikiri kwa mwanadamu. Anaonyesha kazi Yake ya kuwaongoza wanadamu wote, na hii haihusiani na undani wa uzoefu wa mwanadamu, badala yake inahusu usimamizi Wake. Mwanadamu anaonyesha uzoefu wake wakati Mungu anaonyesha nafsi Yake—nafsi hii ni tabia Yake ya asili na iko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uzoefu wa mwanadamu ni kuona kwake na kupata maarifa kulingana na uonyeshaji wa Mungu wa nafsi Yake. Kuona kama huko na maarifa kama hayo yanaitwa asili ya mwanadamu. Yanaonyeshwa kwa msingi wa tabia asili ya mwanadamu na ubora wa tabia yake halisi; hivyo pia vinaitwa nafsi ya mwanadamu. … Maneno yaliyosemwa na mwili wa Mungu ni onyesho la moja kwa moja la Roho na huonyesha kazi ambayo imefanywa na Roho. Mwili haujaipitia au kuiona, lakini bado huonyesha asili Yake kwa sababu kiini cha mwili ni Roho, na huonyesha kazi ya Roho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu).

Kazi ambayo Mungu anafanya haiwakilishi uzoefu wa mwili Wake; kazi ambayo mwanadamu anafanya inawakalisha uzoefu wa mwanadamu. Kila mtu anazungumza kuhusu uzoefu wake binafsi. Mungu anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja, wakati mwanadamu anaweza tu kuonyesha uzoefu unaolingana na huo baada ya kupata uzoefu wa ukweli. Kazi ya Mungu haina masharti na haifungwi na muda au mipaka ya kijiografia. Anaweza kuonyesha kile Alicho wakati wowote, mahali popote. Anafanya kazi vile Anavyopenda. Kazi ya mwanadamu ina masharti na muktadha; vinginevyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawezi kuonyesha ufahamu wake wa Mungu au uzoefu wake wa ukweli. Unatakiwa tu kulinganisha tofauti baina yao ili kuonyesha kama ni kazi ya Mungu mwenyewe au kazi ya mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu).

Kama mwanadamu ndiye ambaye angefanya kazi hii, basi kazi hii ingekuwa kidogo sana. Ingemchukua mwanadamu hadi kiwango fulani, lakini haingekuwa na uwezo wa kumleta mwanadamu katika hatima ya milele. Mwanadamu hana uwezo wa kuamua hatima ya mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, hana uwezo wa kuhakikisha matarajio na hatima ya baadaye ya binadamu. Kazi inayofanywa na Mungu, hata hivyo, ni tofauti. Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yamefanya tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu kuwa wazi kabisa. Kwa maana kiini cha Mungu mwenye mwili na wanadamu wanaotumiwa na Mungu ni tofauti, kazi wanayofanya pia ni tofauti sana. Mungu mwenye mwili huonekana kama mtu wa kawaida kutoka nje, lakini Yeye ni Roho wa Mungu aliyetimilika katika mwili. Hivyo Ana dutu ya kiungu na anamiliki mamlaka, nguvu, uweza usio kifani, na hekima. Hivyo Mungu mwenye mwili anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja katika kazi Yake na kuonyesha tabia ya haki ya Mungu na yote Aliyo nayo na Alicho, na anaweza kuanza enzi mpya na kukamilisha enzi nzee, na anaweza kufunua mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa Mungu, akionyesha nia ya Mungu na mahitaji ya Mungu ya mwanadamu. Maneno yote yanayoonyeshwa na Mungu mwenye mwili ni ukweli na yanaweza kuwa uhai wa mwanadamu na kubadilisha tabia ya maisha ya mwanadamu. Kazi ya Mungu mwenye mwili inaweza kushinda na kutakasa na kumuokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani, na kuleta wanadamu kwa hatima nzuri. Matokeo ya kazi kama hiyo ni kitu ambacho hakuna mtu angeweza kufanya. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na nafasi yake haiwezi kuchukuliwa na yeyote. Kwa upande mwingine, kiini cha mwanadamu anayetumiwa na Mungu ni mwanadamu. Wana utu tu na hawamiliki kiini cha kiungu cha Kristo, hivyo hawawezi kuonyesha ukweli au tabia ya Mungu na yote Aliyo nayo na Alicho. Wanaweza tu kuwasilisha ufahamu wao binafsi wa maneno ya Mungu kwa misingi ya matamshi na kazi ya Mungu, au kuzungumza waliyopitia na ushuhuda wao wenyewe. Ufahamu na ushuhuda wao wote unawakilisha ufahamu na mitazamo yao binafsi ya maneno ya Mungu. Bila kujali jinsi ufahamu wao ni mkubwa au jinsi maneno yao ni sahihi, wanachosema hakiwezi kusemekana ni ukweli, na zaidi ya hayo hakiwezi kusemekana kuwa maneno ya Mungu, hivyo hakiwezi kuwa uhai wa mwanadamu na kinaweza tu kumpa mwanadamu usaidizi, toleo, msaada, na ujenzi wa maadili, hakiwezi kupata matokeo ya kumtakasa mwanadamu, kumuokoa mwanadamu, na kumfanya mwanadamu kuwa kamili. Kwa hivyo, mwanadamu anayetumiwa na Mungu hawezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe na anaweza tu kuratibu na Mungu ili kutimiza wajibu wa mwanadamu.

Kuhusu tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, tunaweza kupeana mfano halisi ili kufanya iwe wazi zaidi kwa kila mmoja. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alihubiri njia ya toba, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu,” akifunua mafumbo ya ufalme wa mbinguni. Na Yeye binafsi alisulubiwa kama kafara ya dhambi kwa mwanadamu, akimfanya mwanadamu kukiri na kutubu, na kumsamehe mwanadamu dhambi, akiwaondolea hatia na laana ya sheria hivyo wanaweza kuhitimu kuja mbele ya Mungu kuomba na kuwasiliana kwa karibu na Mungu, na kufurahia neema tele na ukweli wa Mungu, na kuwaruhusu kuona tabia ya Mungu ya huruma na rehema. Kazi ya Bwana Yesu ilianzisha Enzi ya Neema na kukamilisha Enzi ya Sheria. Hii ndiyo sehemu ya kazi ya Mungu ya Enzi ya Neema. Baada ya Bwana Yesu kukamilisha kazi Yake, mitume Wake waliwaongoza watu wateule wa Mungu kushuhudia na kutenda kulingana na maneno ya Bwana Yesu kwa misingi ya matamshi na kazi Yake, wakieneza ushuhuda wa wokovu Wake na kueneza injili Yake ya kuwakomboa wanadamu duniani kote. Hii ni kazi ya mitume katika Enzi ya Neema, na pia kazi ya wanadamu ambao walitumiwa na Mungu. Hili linaturuhusu kuona kuwa kuna tofauti ya kiini kati ya kazi ya Bwana Yesu na kazi ya mitume. Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho alionyesha ukweli wote ili kutakasa na kuokoa wanadamu, akifunua mafumbo ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka 6,000, akifanya kazi ya hukumu kuanzia kwa nyumba ya Mungu, akiwaokoa wanadamu kikamilifu kutokana na upotovu na ushawishi wa Shetani, akimfanya mwanadamu kuona tabia ya Mungu ya haki, uadhama, hasira, na isiyochukizwa, ili wanadamu wapotovu waweze kuwa huru kutokana na dhambi, wapate utakaso, na wapatwe na Mungu. Kazi ya Mwenyezi Mungu ilianzisha Enzi ya Ufalme na kukamilisha Enzi ya Neema. Hii ni kazi ya Mungu ya Enzi ya Ufalme. Kazi ya mwanadamu anayetumiwa na Mungu kwa misingi ya kazi na neno la Mwenyezi Mungu, hunyunyizia na kuchunga watu wateule wa Mungu, ikiwaongoza kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu na kuingia kwa njia sahihi ya kumwamini Mungu, na kueneza na kushuhudia injili ya Mwenyezi Mungu ya kushuka kwa ufalme. Hii ndiyo kazi ya mwanadamu anayetumiwa na Mungu katika Enzi ya Ufalme. Hili huturuhusu kuona kuwa kazi ya Mungu katika nyakati zote mbili Alipofanyika mwili ilikuwa kazi kuanzisha enzi na kumaliza enzi. Hili linawaelekea wanadamu wote na yote ni hatua ya kazi ya kumaliza mpango wa usimamizi wa Mungu. Hususan ndiyo kazi ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu. Kazi ya Mungu katika nyakati zote mbili Alipofanyika mwili inahakikisha kikamilifu kuwa Mungu pekee ndiye anaweza kuonyesha ukweli katika kazi Yake ili kutakasa na kuokoa wanadamu. Hakuna mwanadamu anaweza kufanya kazi ya Mungu. Mungu mwenye mwili pekee ndiye anaweza kufanya kazi ya Mungu. Hivyo katika nyakati zote mbili ambapo Mungu alifanyika mwili, Anashuhudia kuwa Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima. Kando na Mungu katika mwili, hakuna mwingine yeyote anaweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Hawawezi kuanzisha enzi mpya, kumaliza enzi nzee, na zaidi ya hayo hawawezi kuokoa wanadamu. Kazi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu inaweza tu kuratibu na kazi ya Mungu, ili kuongoza, kuchunga watu wateule wa Mungu na kutimiza wajibu wa mwanadamu. Bila kujali ni miaka ngapi mwanadamu amefanya kazi au ni maneno mangapi yamezungumza, au ni jinsi gani kazi yao inaonekana kuwa njema kutoka nje, kiini chake chote ni kazi ya mwanadamu. Huu ni ukweli. Hiyo ndio tofauti kuu kati ya kazi ya Mungu katika mwili na kazi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu.

Maneno ya Mwenyezi Mungu yametufanya kutambua tofauti muhimu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Ni sasa tu tumefahamu kuwa kadri Mungu mwenye mwili anavyofanya kazi Anaweza kuonyesha ukweli, kuonyesha tabia ya Mungu na yote ambayo Mungu Anayo na Alicho. Tukikubali na kushuhudia kazi ya Mungu tutaweza kuelewa ukweli, na tuweze kuelewa tabia ya Mungu ya utakatifu na haki, kiini cha Mungu, nia za Mungu za kuwaokoa wanadamu, mbinu za Mungu za kuwaokoa wanadamu, na upendo wa Mungu kwa wanadamu zaidi na zaidi. Wakati huo huo, tutapata ufahamu wa kiini, asili, na ukweli wa nafsi yetu iliyopotoshwa na Shetani. Kwa njia hiyo, tabia yetu potovu inaweza kupata utakaso na badiliko, na tunaweza kutoa utiifu na hofu ya kweli kwa Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Hata hivyo, kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu ni tofauti kabisa. Kwa sababu mwanadamu hawezi kuonyesha ukweli na anaweza tu kujadili aliyopitia na ufahamu wake binafsi wa maneno ya Mungu, hata kama unaambatana na ukweli, unaweza tu kuongoza, kuchunga, kutoa msaada, na kusaidia watu wateule wa Mungu. Hii inaonyesha kuwa ikiwa ni mtu aliyeidhinishwa na Mungu, kazi wanayofanya ni kuratibu tu na kazi ya Mungu na kutimiza wajibu wa mwanadamu. Ikiwa ni mtu asiyetumiwa na Mungu, mtu asiye na kazi ya Roho Mtakatifu, basi yeye ni mtu anatukuza vipaji, vipawa, na umaarufu wa mwanadamu. Hata wakati wanapoeleza Biblia, wanatukuza maneno ya watu katika Biblia, wakiyafanya maneno ya Mungu kukosa maana na kuchukua nafasi ya maneno ya Mungu. Kazi ya watu kama hao ni kazi ya Mafarisayo na ni kazi ya kumpinga Mungu. Kazi ya mwanadamu hasa inaainika katika hali hizi mbili tofauti. Bila kujali chochote, tofauti kubwa zaidi kati ya kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu ni hii: Ikiwa ni kazi ya mwanadamu tu, haiwezi kupata matokeo ya kutakasa na kuokoa mwanadamu. Ilhali kazi ya Mungu inaweza kuonyesha na kutakasa na kuokoa mwanadamu. Huo ni ukweli. Jambo kuu tunalozungumzia hapa ni tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya watu wanaotumiwa na Mungu. Kazi ya viongozi hao wa dini wasiotumiwa na Mungu ni suala lingine.

Kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu zina tofauti wazi hivyo, basi ni kwa nini bado tunaweza kuabudu na kufuata mwanadamu wakati huo huo kama kumwabudu Mungu? Ni kwa nini bado kuna watu wengi sana wanaochukulia kazi ya wale wanaowaabudu, kama watu mashuhuri wa kiroho na viongozi wa dini kama kazi ya Mungu? Ni kwa nini kuna watu ambao hata huchukulia udanganyifu wa Makristo wa uongo na pepo waovu kama kazi ya Mungu? Ni kwa sababu hatumiliki ukweli na hatuwezi kutofautisha kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Hatujui kiini cha Mungu mwenye mwili na kiini cha mwanadamu, na hatujui jinsi ya kutambua ukweli ni nini na ni nini kinaambatana na ukweli. Hatuwezi kutofautisha kati ya sauti ya Mungu na matamshi ya mwanadamu, tena tumepotoshwa na Shetani na sote tunaabudu ufahamu na vipaji, hivyo ni rahisi sana kuchukulia ufahamu wa Biblia, mafundisho ya dini, na nadharia za kitheolojia zinazotoka kwa mwanadamu kama ukweli. Kukubali kwetu kwa mambo haya ambayo si ya kweli na yanayotoka kwa mwanadamu kunaweza kuleta ongezeko la ufahamu wetu, lakini hakitoi chochote kwa uhai wetu, na zaidi hakiwezi kupata matokeo ya kumjua Mungu na kumuogopa Mungu. Huu ni ukweli usiokanwa. Kwa hivyo, bila kujali ni kiasi gani cha kazi inayofanywa na mwanadamu, ni maneno mangapi mwanadamu anazungumza, ni kwa muda gani mwanadamu anafanya kazi, au kazi yake ni nzuri kiasi gani, haiwezi kupata matokeo ya kutakasa na kuokoa mwanadamu. Maisha ya mwanadamu hayatabadilika. Hii inafunua kuwa kazi ya mwanadamu haiwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Ni kazi ya Mungu pekee ndio inaweza kuokoa mwanadamu. Bila kujali ni kwa kiasi gani kazi ya Mungu ni fupi na jinsi maneno Anayotamka ni machache, bado inaweza kuanzisha enzi na kumaliza enzi, na inaweza kupata matokeo ya kukomboa na kuokoa wanadamu. Hii ndiyo tofauti wazi kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Wakati tu tutakapoelewa tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ndipo tutakosa kuabudu na kufuata mwanadamu bila kufikiria, na tuweze kutambua na kukataa udanganyifu na udhibiti wa Makristo wa uongo na wapinga Kristo. Kwa njia hii, tutaweza kukubali na kutii kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kupata hukumu na utakaso wa Mungu ili tupate wokovu wa Mungu. Ikiwa mwanadamu hawezi kutofautisha kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, hatutaweza kuwa huru kutokana na udanganyifu na udhibiti wa Makristo wa uongo na wapinga Kristo. Kwa njia hii, tunamwamini Mungu kwa jina tu, lakini kwa kweli tunaamini mwanadamu, tunamfuata mwanadamu, na kumuabudu mwanadamu; tunaabudu sanamu. Huku ni kumpinga Mungu, kumsaliti Mungu. Ikiwa bado tunakosa kutambua kasoro ya njia zetu, hatimaye tutalaaniwa na Mungu na kuondolewa na Mungu kwa kuchukiza tabia ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Kama hatuwezi kutofautisha kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, au kutofautisha kati ya watu ambao Mungu huwatumia na wale Mafarisayo wanafiki, tutaelekea kuwaabudu na kuwafuata wanadamu na tutaweza kupotoka kirahisi toka kwenye njia ya kweli! Itakuwa tu kama wakati Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi Yake, na watu wateule wa Mungu katika dini ya Kiyahudi wote waliwafuata Mafarisayo wanafiki, wakimtelekeza Yeye. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anatenda kazi ya hukumu. Katika ulimwengu wa kidini, wachungaji na viongozi, Mafarisayo wa siku za leo, wanadanganya, wanazuia, na kuwafungia watu wengi sana, wakiwaelekeza kumtelekeza Kristo wa siku za mwisho. Hili ni somo kubwa ambalo ni lazima tujifunze. Kumfuata Mungu, ni lazima tuwe na uwezo wa kutambua asili ya viongozi wa kidini. Yaani, wao si lolote bali Mafarisayo wanafiki. Wanatenda kazi kupitia vipawa na talanta zao, wakifasiri Biblia kulingana na mawazo, fikira, na utoaji hoja wao wa kimantiki. Yale hasa wanayohubiri ni nadharia za theolojia na masomo ya Biblia. Wanajali tu kuhusu kufasiri na kuhubiri maneno ya wanadamu katika Biblia, badala ya kuinua na kuwa na ushuhuda kwa maneno ya Mungu. Wanatumia maneno ya wanadamu kubadilisha na maneno ya Bwana Yesu, wakimgeuza Bwana kuwa mkubwa wa jina tu. Kazi hii inaenda kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Kiini cha upinzani wa Mafarisayo kwa Mungu kiko hapa. Watu wa kidini wanapenda uongozi wa Mafarisayo, na wanafuata bila kufikiria. Wanamwamini Mungu kwa miaka na miaka, lakini kamwe hawapokei lishe yoyote ya ukweli au uzima. Sanasana, wanaweza tu kutumaini kupata maarifa kiasi ya Biblia na nadharia za theolojia. Wanaongezeka zaidi na zaidi katika majivuno, kujihesabia haki, na wenye dharau katika tabia, na wanakosa hata chembe ya uchaji kwa Mungu. Polepole, Mungu anapoteza nafasi Yake katika moyo wa mwanadamu, na bila wao kujua, wanaifuata njia ya Mafarisayo katika upinzani kwa Mungu. Hususani, kuna viongozi wengi wa dini na watu ambao huiweka Biblia nje ya muktadha na kuifasiri kimakosa, wakieneza uzushi na dhana zenye makosa zinazokubaliana na mawazo na fikira za mwanadamu na kuridhisha tamaa zao za makuu na shauku zao ili wawadanganye, wawafunge, na kuwaendesha wao kiufundi. Kuna watu wengi ambao huchukulia uzushi na dhana hizi zenye makosa kana kwamba ni neno la Mungu, ukweli. Wanaongozwa kwenye njia mbaya. Hawa viongozi wa dini na wale waitwao watu maarufu hakika ni wapinga Kristo ambao Mungu amewafunua kupitia kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Ukweli huu unatosha kuthibitisha kwamba kazi ya hawa waitwao viongozi wa dini na watu wa kiroho haitoki katika kazi ya Roho Mtakatifu. Bali, ni Mafarisayo na wapinga Kristo tu wanaotudanganya na kutuumiza sisi. Wote wanapingana na Mungu na wanamsaliti Yeye. Ni wao ndio wanampigilia misumari msalabani kwa mara nyingine, na Mungu amewalaani!

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Kuna tofauti tatu kuu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, Tofauti ya kwanza ni kwamba kazi ya Mungu inahusisha kuanzisha na kutamatisha enzi. Kwa hiyo, kazi Yake inaelekezwa kwa jamii nzima ya binadamu. Hailengi tu nchi moja, jamii moja ya watu au kundi fulani la watu. Ni ya jamii nzima ya binadamu. Kazi yote ya Mungu bila kuzuilika huathiri jamii nzima ya binadamu. Hapa ndipo tofauti kubwa zaidi kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ipo. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili kama Bwana Yesu na kutekeleza hatua ya kazi ya ukombozi wa wanadamu. Baada ya Bwana Yesu kutundikwa msalabani, kutimiza kazi ya ukombozi, Roho Mtakatifu alianza kuwaongoza watu wa Mungu wateule kumshuhudia Bwana Yesu na hatimaye kueneza kazi Yake kotekote kwa jamii nzima ya binadamu. Injili ya ukombozi wa Bwana Yesu ulienezwa basi kwa miisho ya ulimwengu—hili linathibitisha kwamba hii ilikuwa kazi ya Mungu. Hii ingalikuwa kazi ya mwanadamu, hakika haingalienea kwa miisho ya ulimwengu. Miaka elfu mbili ilitenga Enzi ya Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme. Kwa zaidi ya miaka elfu mbili, hakuna mtu aliyeonekana ambaye aliweza kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya. Aidha, hakukuwa na mtu ambaye aliweza kufanya aina yoyote ya kazi maalum ambayo ingeenea kotekote kwa mataifa yote ya dunia. Hakukuwa na mifano kama hii ya hili mpaka Mungu alipopata mwili katika siku za mwisho kutekeleza kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua ya majaribio ya kazi ya Mungu tayari imekuwa ya ufanisi nchini Uchina—mradi mkuu wa Mungu tayari umekamilishwa, na kazi Yake imeanza kuenea katika kila pembe ya dunia. Kwa njia hii tunaweza kuthibitisha zaidi kwamba kazi yote ya Mungu inaelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anaanza kazi Yake ya majaribio katika nchi, na baada ya hiyo kukamilishwa kwa ufanisi, kazi ya Mungu inaanza kuenea na kufikia wanadamu wote. Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. …

Tofauti ya pili kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ni kwamba kazi ya Mungu inaonyesha kile Mungu alicho. Inawakilisha tabia ya Mungu kabisa. Kila kitu ambacho Mungu anakionyesha ni ukweli, njia, na uzima kabisa. Wale wote wanaopitia kazi ya Mungu wanatambua haki, utakatifu, uweza, hekima, ajabu na kutoweza kueleweka kwa Mungu. Kile ambacho kazi ya mwanadamu inaonyesha ni uzoefu na ufahamu wa mwanadamu—inawakilisha ubinadamu wa mwanadamu. Bila kujali ni kiasi gani cha kazi mwanadamu anafanya au ni kikubwa kiasi gani, hakuna kati yake inayoweza kuwa ukweli hata kidogo. Inaweza tu kuwa ufahamu au uzoefu wa mwanadamu wa ukweli—haiwezi kusemekana hata kidogo kwamba ni ukweli kabisa au kwamba inawakilisha ukweli. …

Kipengele cha tatu cha tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ni kwamba kazi ya Mungu ina uwezo wa kuwashinda watu, kuwabadili watu, au kugeuza tabia zao na kuwaweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani. Bila kujali kiasi cha uzoefu na ufahamu ambao mwanadamu anao kuhusu neno la Mungu, kazi yake haiwezi kuwaokoa watu. Aidha, haiwezi kubadili tabia ya mtu mwingine. Hii ni kwa sababu neno la Mungu ni ukweli na ni ukweli pekee unaoweza kuwa uzima wa mtu. Neno la mwanadamu, katika hali bora zaidi, ni ufahamu unaokubaliana na ukweli. Linaweza kuwasaidia na kuwarekebisha watu maadili kwa muda tu, lakini haiwezi kuwa uzima wa mtu. Hii ndiyo maana kazi ya Mungu inaweza kumwokoa mwanadamu na kazi ya mwanadamu haiwezi kumpa yeyote mwingine wokovu. Kazi ya Mungu inaweza kubadili tabia za watu wakati kazi ya mwanadamu haiwezi kubadili tabia ya yeyote. Wale wote walio na uzoefu wanaweza kuona hili wazi. Kimsingi, bila kujali kiasi cha kazi cha Roho Mtakatifu ambacho mtu anacho, hata kama amekuwa akifanya kazi miongoni mwa watu kwa idadi fulani ya miaka, kazi yake haiwezi kutimiza badiliko katika tabia yake. Haiwezi kumsaidia kutimiza wokovu kamili, wa kweli. Hii ni hakika. Ni kazi ya Mungu pekee inayoweza kufanya hili. Mwanadamu akifanya vyema katika kupitia na kufuatilia kwake ukweli, ataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na atatimiza badiliko katika tabia yake ya maisha. Atatimiza ufahamu wa kweli wa asili yake mwenyewe potovu. Mwishowe, ataweza kujiweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani na kupata wokovu kutoka kwa Mungu. Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi kati ya kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Tofauti kubwa zaidi kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu yapatikana katika ukweli kwamba Mungu ana uwezo wa kuanzisha na kukamilisha enzi. Mungu pekee Mwenyewe ndiye anayeweza kufanya kazi hiyo; wanadamu hawawezi. Mbona hivyo? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na wao sio ukweli; Mungu pekee yake ndiye. Haijalishi jinsi maneno ya watu yanakubaliana na ukweli kwa ukaribu, jinsi mahubiri yao yalivyo ya kifahari, au ni kiasi gani wanaelewa, ni uzoefu na ufahamu mdogo tu wa maneno ya Mungu na wa ukweli, na ni kitu kidogo tu ambacho wamepata kwa kupitia kazi ya Mungu. Huo si ukweli sahihi. Kwa hiyo, haijalishi ni ukweli kiasi gani ambacho mtu anafahamu, yeye hawezi kufanya kazi ya kuanzisha na kukamilisha enzi. Hii inaamuliwa na kiini cha wanadamu. …

Yote ambayo mtu anayo na aliyo, na ubinadamu wake, bila kujali kama ni ya kifahari au mazuri, ni kitu kidogo kinachopaswa kumilikiwa ndani ya ubinadamu wa kawaida; hiki hakiwezi kulinganishwa kabisa na kile Mungu anacho na alicho; wala na uhalisi wa ukweli ambao Mungu anadhihirisha. Ni tofauti kati ya mbingu na dunia; kwa hivyo mwanadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu. … Licha ya ukubwa wa kazi unayofanya, unafanya kazi kwa miaka ngapi, ni miaka ngapi zaidi ambayo umefanya kazi kuliko Mungu mwenye mwili, au ni maneno mangapi zaidi ambayo umetamka kuliko Yeye, kile unachoonyesha si zaidi cha kile mwanadamu anacho na alicho. Ni sehemu kidogo tu ya uzoefu wa mwanadamu na maarifa ya maneno ya Mungu na ukweli. Hakiwezi kuwa uzima halisi wa mtu. Kwa hiyo bila kujali ni mahubiri mangapi mtu anatoa, bila kujali jinsi wengine wanavyofikiria mahubiri yake ni makuu na bila kujali ni kiasi kipi cha kazi anafanya, hakuna anachoonyesha ambacho kina ukweli na si onyesho sahihi zaidi la ukweli, sembuse kuweza kuwaongoza wanadamu wote mbele. Hata kama maneno ya mtu yana nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, yanaweza kuwaletea watu ujenzi wa maadili na riziki kidogo tu. Yote yanayoweza kufanya ni kuletea watu msaada kidogo kwa kipindi fulani cha muda pekee. Hili ndilo linaloweza kutimizwa kupitia kazi ya mwanadamu. Je, kwa nini basi, kazi ya mwanadamu haiwezi kufikia matokeo sawa na kazi ya Mungu? Ni kwa sababu kiini cha wanadamu si ukweli; kiini cha mwanadamu kina baadhi ya vitu tu ambavyo ubinadamu wa kawaida unavyo na ulivyo. Kiko tofauti kabisa na kile Mungu anacho na alicho, tofauti kabisa na ukweli ambacho Mungu anadhihirisha. Kwa maneno mengine, mwanadamu akiondoka kwenye kazi ya Mungu na Roho Mtakatifu aache kufanya kazi, kazi ya mwanadamu itakuwa ya faida kidogo zaidi kwa wengine na watu watakosa njia polepole. Kuna matokeo machache dhahiri ambayo ni kazi ya Mungu pekee inaweza kutimiza na kazi ya mwanadamu haiwezi kamwe: Chochote anachofanya mwanadamu, hakiwezi kubadili tabia ya maisha ya watu; chochote anachofanya mwanadamu, hakiwezi kuwaruhusu watu kumjua Mungu kwa kweli au kutakaswa Hili ni bila shaka. Wengine wanasema: “Hiyo si kwa sababu muda wao wa kufanya kazi sio mrefu vile.” Hilo si kweli hata kidogo. Hata kipindi kirefu cha muda hakitasaidia. Je, kazi ya mwanadamu inaweza kumruhusu mwanadamu kutimiza ufahamu wa Mungu? Haijalishi ni miaka mingapi unawaongoza wengine, huwezi kuwaongoza kufikia ufahamu wa Mungu. Hebu tuangalie mifano michache. Je, kazi ya Paulo inaweza kuwaruhusu watu kumjua Mungu? Je, nyaraka hizo zote za mitume katika Agano Jipya zinaweza kuwaruhusu watu kumjua Mungu? Je, kazi ya manabii na watumishi wengi wa Mungu wa Agano la Kale inaweza kuwaruhusu watu kumjua Mungu? Hakuna hata mmoja wao anayeweza. Matokeo ambayo yanaweza kutimizwa na kazi ya mwanadamu ni machache sana; yote yanayoweza kufanya ni kuunga mkono kipindi fulani cha kazi ya Mungu. ... Kazi ya mwanadamu haiwezi kumsaidia mwanadamu kumjua Mungu, kazi ya mwanadamu haiwezi kubadilisha tabia ya mwanadamu, na kazi ya mwanadamu haiwezi kumsaidia apate utakaso. Huu ndio ushahidi. Je kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho? Kuna ushuhuda zaidi na zaidi kutoka kwa wateule wa Mungu kupitia kazi ya Mungu. Watu wengi sana wameshindwa na wameweka kando kila kitu ili kumfuata Mungu, watu wengi sana wamekuwa na ushahidi mkubwa, na watu wengi sana wameandika makala mengi yakitoa ushahidi kuhusu uzoefu wao binafsi; kuna kila aina za ushuhuda. Watu wengine ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa miaka minane au kumi wana ushuhuda mzuri sana; wengine wana ushuhuda mzuri baada ya miaka mitatu hadi mitano tu. Ikiwa watu hawa ambao wamepata ushuhuda kiasi wangekuwa na miaka kumi au ishirini zaidi ya uzoefu, huo ungekuwa ushahidi wa aina gani? Je, ungekuwa ushahidi mkubwa hata zaidi na adhimu zaidi? Je, haya ndiyo yanayotimizwa kupitia kazi ya Mungu? Ni matokeo ya muongo mmoja wa kazi ya Mungu ambayo yanazidi matokeo ya karne au milenia ya kazi ya mwanadamu. Je, hii inaonyesha nini? Kwamba kazi ya Mungu pekee ndiyo inaweza kutimiza wokovu, mabadiliko, nakukamilishwa kwa mwanadamu, wakati hakuna kiwango chochote cha muda cha ya kazi ya mwanadamu kingeweza kutimiza matokeo kama hayo. Je, kazi ya mwanadamu inaweza kuwa na matokeo gani hatimaye? Ni kuwafanya wengine wanapendezwa, kumwidhinisha, na kumwiga mtu huyo tu. Kwa kiwango cha juu zaidi, watu huenda wakawa na tabia nzuri kiasi tu; mabadiliko ya tabia yao ya maisha hayawezi kufikiwa, kumtii Mungu na ufahamu wa Mungu hauwezi kufikiwa, kumcha Mungu na kuepuka uovu hakuwezi kufikiwa, na kumwona Mungu kupitia utakaso wa kweli hakuwezi kufikiwa. Matokeo hayawezi kutimizwa katika vipengele hivi vyovyote vikubwa.

Kipengele kimoja cha kazi ya Mungu ni kwamba kwa kuipitia, tunaweza kugundua kile Mungu anacho na alicho, kuona tabia ya Mungu, na tunaweza kujua hekima na uwezo Wake. Hiki ni kitu ambacho kinaweza kutimizwa moja kwa moja kupitia maneno ya Mungu. Kipengele kingine ni kwamba neno la Mungu linaweza kuwa maisha ya mwanadamu. Tunapokuwa na uzoefu na ufahamu wa kweli wa neno la Mungu, moyo wa kumcha Mungu utakua ndani yetu na kisha tutaweza kuendelea kufyonza maji hai yatoayo riziki ya neno Lake, na huku likikita linakita mizizi ndani yetu, tutaweza kuishi kwa kudhihirisha ushuhuda ambao Mungu anahitaji kwetu nyakati zote. Yaani, neno Lake litakuwa maisha yetu hasa. Neno la Mungu ni chemchemi yetu ya maisha isiyo na mwisho wala mipaka. Je, kuhusu kazi ya mwanadamu? Haijalishi jinsi maneno ya mtu yalivyo sahihi au yanalingana na ukweli jinsi gani, hayawezi kuwa kama maisha yenyewe kwa wengine; yanaweza tu kutoa msaada na ujenzi wa maadili wa muda mfupi. Sasa unaweza kuona hili, siyo? Je, hii siyo tofauti kati ya kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu? Hiyo ni kusema, kile mwanadamu anaonyesha ni kile alicho tu, lakini kile Mungu anaonyesha ni chote Alicho. Yote ambayo mwanadamu anaweza kufanya ni kuleta faida kiasi na ujenzi kiasi wa maadili kwa wengine, ilhali kile Mungu anacholeta kwa mwanadamu ni riziki ya milele ya maisha—tofauti hizo ni kubwa sana. Tukiondoka kwa mwanadamu, bado tunaweza kuendelea mbele; bila neno la Mungu, tungepoteza chemchemi ya maisha. Kwa hiyo Mungu alisema, “Kristo ni ukweli, njia, na uzima.” Maneno ya Mungu ni hazina yetu, kiini chetu, na ni ya lazima kwa kila mtu. Tukiwa na maneno ya Mungu, tuna mwelekeo katika maisha yetu, tuna lengo la maisha yetu na pia riziki ya maisha na kanuni za kuishi.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp