524 Neno la Mungu Kweli Limekuwa Maisha Yako?

1 Mara nyingi watu husema kuwa wamemfanya Mungu kuwa maisha yao, lakini bado wangali kupitia hatua hii. Wanasema tu kuwa Mungu ndiye maisha yao, kuwa Anawaongoza kila siku, kuwa wanakula na kunywa maneno Yake kila siku, na kuwa wanamwomba kila siku, na hivyo Amekuwa ndiye maisha yao. Ufahamu wa wanaosema hili ni wa juu juu. Ndani ya watu wengi hakuna msingi; maneno ya Mungu yamepandwa ndani yao, lakini bado hayajaota, au hata kuzaa tunda lolote. Siku moja ukishakuwa na uzoefu hadi kiwango fulani, Mungu akitaka kukuacha, hutaweza kufanya hivyo. Daima utahisi kuwa huwezi kuishi bila Mungu ndani yako.

2 Kuwa bila Mungu itakuwa kama kupoteza uhai wako, hutaweza kuishi bila Mungu. Unapopitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefanikisha imani yako kwa Mungu, na kwa njia hii Mungu atakuwa maisha yako, atakuwa msingi wa kuishi kwako, na hutaweza tena kumuacha Mungu. Unapokuwa umepitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefurahia upendo wa Mungu kwelikweli, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa karibu mno, Mungu atakuwa maisha yako, upendo wako. Hiki ni kimo halisi cha watu; ni maisha halisi.

3 Lazima ugundue kuwa Mungu yupo maishani mwako, kiasi kwamba kama Mungu angeondolewa kutoka katika moyo wako ingekuwa kama kupoteza uhai wako; Mungu lazima awe maisha yako, na lazima uwe huwezi kumwacha. Kwa njia hii utakuwa umekutana na Mungu, na kwa wakati huu, unapompenda Mungu, utampenda Mungu kwa kweli, na utakuwa upendo wa kipekee, upendo safi. Siku moja, matukio unayopitia yatakapokuwa kwamba maisha yako yamefikia kiwango fulani, unapomwomba Mungu, na kula na kunywa maneno ya Mungu, hutaweza kumwacha Mungu ndani, wala hutaweza kumsahau hata kama unataka.

4 Mungu atakuwa maisha yako, waweza kuusahau ulimwengu, waweza kumsahau mkeo, mmeo, au watoto, lakini itakuwia vigumu kumsahau Mungu—hilo haliwezekani, haya ndiyo maisha yako halisi, na upendo wako wa ukweli kwa Mungu. Upendo wa watu kwa Mungu ufikiapo kiwango fulani, upendo wao kwa kitu kingine chochote huwezi kulinganishwa na upendo wao kwa Mungu; upendo wao kwa Mungu unapewa kipaumbele. Kwa njia hii wanaweza kuacha vitu vingine vyote, na wawe tayari kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Unapopata pendo kutoka kwa Mungu ambalo linazidi mengine yote, utaishi katika uhalisi, na katika upendo wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 523 Fuata Maneno ya Mungu na Huwezi Kupotea

Inayofuata: 525 Tafuta Kuwa Yule Anayemwabudu Mungu kwa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp