444 Una Uhusiano wa Kawaida na Mungu?

1 Kama unataka kutafuta kukamilishwa na Mungu na kuingia katika njia sahihi ya maisha, basi moyo wako siku zote unapaswa kuishi katika uwepo wa Mungu, usiwe fisadi, usimfuate Shetani, usimwachie Shetani fursa yoyote kufanya kazi yake, na usimruhusu Shetani kukutumia. Unapaswa kujitoa kikamilifu kwa Mungu na kumwacha Mungu akutawale. Upo radhi kuwa mtumishi wa Shetani? Upo radhi kunyonywa na Shetani? Je, unamwamini Mungu na kumtafuta Mungu ili kwamba uweze kukamilishwa na Yeye, au ni ili uwe foili katika kazi ya Mungu? Je, upo radhi kupatwa na Mungu na kuishi maisha ya maana, au upo radhi kuishi maisha tupu na yasiyo na thamani?

2 Upo radhi kutumiwa na Mungu, au kunyonywa na Shetani? Upo radhi kuacha maneno ya Mungu na ukweli kukujaza, au kuacha dhambi na Shetani kukujaza? Litafakari na kulipima hili. Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu.

3 Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili na kiini cha mwanadamu, na kujielewa mwenyewe kweli; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata tamaa ya kutii. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 443 Zingatia Maneno ya Mungu kwa Ajili ya Uhusiano Ufaao na Wengine

Inayofuata: 445 Mfanano wa Wale Wanaotumiwa na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki