780 Mungu Anataka Kuwapata Wale Walio na Maarifa ya Kweli Kumhusu

1 Ufahamu wa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vinaweza kuwa na athari nzuri kwa binadamu. Vinaweza kuwasaidia kuwa na imani zaidi kwa Mungu, na kuwasaidia kufanikisha utiifu wa kweli na uchaji Kwake. Basi, wao tena si wafuasi wasioona, au wanaomwabudu tu bila mpango. Mungu hataki wajinga au wale wanaofuata umati bila mpango, lakini Anataka kundi la watu ambao wana ufahamu na maarifa wazi katika mioyo yao kuhusu tabia ya Mungu na wanaweza kuchukua nafasi ya mashahidi wa Mungu, watu ambao hawawezi kamwe kumwacha Mungu kwa sababu ya uzuri Wake, kwa sababu ya kile Alicho nacho na kile Alicho, na kwa sababu ya tabia Yake ya haki.

2 Kama mfuasi wa Mungu, endapo katika moyo wako bado kuna ukosefu wa ubayana, au kuna hali tata au mkanganyo kuhusu kuwepo kwa kweli kwa Mungu, tabia Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mpango Wake wa kumwokoa binadamu, basi imani yako haiwezi kupata sifa za Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii kumfuata Yeye, na pia Hapendi mtu wa aina hii akija mbele Yake. Kwa sababu mtu wa aina hii hamwelewi Mungu, hawezi kutoa moyo wake kwa Mungu—moyo wake umemfungwa Kwake, hivyo basi imani yake katika Mungu imejaa kasoro mbalimbali. Kumfuata kwake Mungu kunaweza tu kusemwa kuwa ni kwa kipumbavu.

3 Watu wanaweza tu kupata imani ya kweli na kuwa wafuasi wa kweli kama watakuwa na ufahamu na maarifa ya kweli wa Mungu, jambo ambalo linaleta utiifu na uchaji wa kweli Kwake. Ni kwa njia hii tu ndiyo anaweza kuutoa moyo wake kwa Mungu, kuufungua Kwake. Hili ndilo Mungu anataka, kwa sababu kila kitu wanachofanya na kufikiria, kinaweza kustahimili majaribu ya Mungu, na kinaweza kumshuhudia Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 779 Mungu Anatumaini Mwanadamu Anaweza Kumjua na Kumwelewa

Inayofuata: 781 Kumjua Yeye ni Hitaji la Mungu la Mwisho kwa Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp