Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

639 Bado Hujapata Mengi Kutoka kwa Mungu?

1 Ingawa Ayubu alipitia majaribu kutoka kwa Yehova, alikuwa tu mtu mwenye haki aliyemwabudu Yehova, na hata alipokuwa akipitia majaribu hayo hakulalamika kumhusu Yeye, lakini alithamini sana kukutana kwake na Yehova. Watu wa leo hawathamini tu uwepo wa Yehova, bali humkataa, humchukia sana, hulalamika kumhusu, na hudhihaki uwepo Wake. Je, hamjapata zaidi ya kidogo? Je, mateso yenu kweli hayajakuwa makubwa sana? Je, baraka zenu hazijakuwa nyingi kuliko zile za Maria na Yakobo? Je, upinzani wenu haujakuwa hafifu? Inawezekana kuwa yale Nimehitaji kwenu, yale Nimeuliza kutoka kwenu yamekuwa makuu mno na mengi sana?

2 Ghadhabu Yangu iliachiliwa huru tu juu ya wale Waisraeli walionipinga Mimi, si moja kwa moja juu yenu, lakini kile ambacho mmepata kimekuwa tu hukumu Yangu isiyo na huruma na mafichuzi pamoja na utakaso mkali usio na huruma. Licha ya haya watu bado wananipinga na kunikana Mimi bila hata chembe ya utii. Na hata kuna baadhi ya watu ambao hujitenga na Mimi na kunikataa; aina hiyo ya mtu si bora zaidi kuliko bendi ya Kora na Dathani wakimpinga Musa. Mioyo ya watu imekuwa migumu sana, na asili zao ni kaidi sana. Kamwe hawatabadili mienendo yao ya zamani. Je, watu na aina hii ya tabia wanawezaje kujua kwamba wamefurahia baraka zaidi ya mara mia kuliko zile za Ayubu?

3 Wanawezaje kugundua kwamba kile wanachokifurahia ni baraka ambazo zimeonekana katika enzi zote kwa nadra sana, ambazo hakuna mtu aliyewahi kuzifurahia awali? Dhamiri za watu zinawezaje kuhisi aina hii ya baraka ambayo hubeba adhabu? Chote Ninachohitaji kwenu ni ili muweze kuwa mifano kwa kazi Yangu na kuwa mashahidi kwa ajili ya tabia Yangu yote na matendo Yangu yote, na ili muweze kuwekwa huru kutokana na mateso ya Shetani. Lakini wanadamu daima huchukizwa na kazi Yangu na wanakuwa na uhasama kwake kimakusudi. Aina hiyo ya mtu anawezaje kutonichochea Mimi kurejesha sheria za Israeli na kuleta juu yake ghadhabu Yangu kwa ajili ya Israeli?

Umetoholewa kutoka katika “Ufahamu wako wa ‘Baraka’ ni Upi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Cha Kusikitisha Zaidi Kuhusu Imani ya Binadamu kwa Mungu

Inayofuata:Wewe ni Mwasi Sana

Maudhui Yanayohusiana

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …