328 Watu Hawajampa Mungu Mioyo Yao Kabisa
Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu.
1 Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye.
2 Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili