459 Tilia Maanani Kazi ya Roho Mtakatifu

1 Ni watu wa aina gani ambao hupewa nuru na Roho Mtakatifu? Wale ambao ni hodari na waangalifu katika mawazo yao. Wanapopewa hisia, na nuru, watu kama hao wanaweza kutambua kuwa hii imefanywa na Roho Mtakatifu, kwamba Mungu anatamani kufanya kazi kwa njia hii. Kunaweza pia kuwa na nyakati ambazo wanakaripiwa; mara tu wanapogundua jambo hili, wanazuiwa—ni mtu wa aina hii anayepewa nuru na Roho Mtakatifu. Kwa wale ambao hawajali, na hawana ufahamu wa kiroho, wanapewa hisia, lakini hawawezi kutambua. Hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa hivyo Roho Mtakatifu hawapi nuru tena. Wakati ambapo hawakubali nuru mara tatu au nne mfululizo, basi Roho Mtakatifu hafanyi kazi tena.

2 Watu wengine si waangalifu katika mawazo yao; wao kila wakati hutegemeza uamuzi wao kwenye ndoto zao. Wanaweza kufanya uamuzi sahihi kwa njia hiyo? Kujijua na kuelewa mapenzi ya Mungu lazima kuwe kupitia katika ukweli, kupitia kujua, na kwa njia ya kupitia, si kupitia mambo ya nje. Kazi ya Roho Mtakatifu ni halisi zaidi. Wengine wana uwezo wa kuelewa ukweli tu, lakini kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu, hawana uzoefu. Katika siku zijazo, lazima mzingatie hisia zilizo ngumu zaidi kutambua, nuru iliyo mgumu zaidi kutambua. Kitu kinapokutendekea, lazima ukichunguze na kukikabili kwa mtazamo wa ukweli, na utaingia kwenye njia sahihi polepole.

Umetoholewa kutoka katika “Lazima Uangalie Masuala Yote kwa Makini kwa Mtazamo wa Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 458 Roho Mtakatifu Afanyapo Kazi kwa Mwanadamu

Inayofuata: 460 Tii Kazi ya Roho Mtakatifu na Utakuwa Kwenye Njia Kuelekea Kukamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp