685 Shikilia Imara Kile Mwanadamu Lazima Afanye

1 Kwa sababu una uhakika kuwa njia hii ni ya kweli, lazima uifuate hadi mwisho; lazima udumishe ibada yako kwa Mungu. Kwa sababu umeona kuwa Mungu Mwenyewe amekuja duniani kukukamilisha, lazima umpe moyo wako Kwake kabisa. Haijalishi ni nini Anafanya, hata kama Anaamua tokeo lisilofaa kwako mwishowe, bado unaweza kumfuata. Hii ni kudumisha usafi wako mbele za Mungu. Kupeana mwili wa kiroho mtakatifu na bikira safi kwa Mungu inamaanisha kuweka moyo mwaminifu mbele za Mungu. Kwa wanadamu, uaminifu ni usafi, na kuweza kuwa mwaminifu kwa Mungu ni kudumisha usafi.

2 Unapaswa kuweza kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa, na haijalishi matokeo yako ya usoni na hatima yako inaweza kuwa ipi, unapaswa kuweza kufuatilia maarifa na upendo kwa Mungu katika miaka ambayo uko hai, na haijalishi jinsi Mungu anavyokutendea, unapaswa kuweza kuepuka kulalamika. Kuna sharti moja kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya watu. Bora wana hamu na wanatafuta na hawasitisiti ama kuwa na shaka kuhusu matendo ya Mungu, nao wanaweza kushikilia wajibu wao kila wakati, hivi tu ndivyo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu.

3 Katika kila hatua ya kazi ya Mungu, kinachohitajika kwa wanadamu ni imani kuu na kutafuta mbele za Mungu—kupitia tu kwa mazoea ndipo watu wataweza kugundua jinsi Mungu Anavyopendeka na jinsi Roho Mtakatifu Anavyofanya kazi ndani ya watu. Usipopata uzoefu, usipoihisi njia yako kupitia hayo, usipotafuta, hutapata chochote. Lazima uhisi njia yako kupitia mazoea yako, na kwa kupitia mazoea yako tu ndipo utaona matendo ya Mungu, na kugundua maajabu Yake na mambo Yake yasiyoeleweka.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 684 Wote Wamtafutao Mungu kwa Kweli Wanaweza Kupata Baraka Zake

Inayofuata: 686 Ni Wale tu Wanaopata Wokovu wa Mungu Ndio Waishio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp