981 Mungu Atumai Watu Wote Wapate Njia Ng’avu

1 Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo.

2 Lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine. Natumai mtaniendekeza, nami Natumai hata zaidi kwamba mtaweza kuamini kila neno Ninalosema, na bado zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Labda katika siku zijazo hakuna mtu yeyote atakuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninayowaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma sana, sembuse kuwaeleza mambo haya kwa uvumilivu hivi.

3 Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kugumia kwa maumivu, au mtakuwa mkiishi katika usiku wa giza bila hata chembe ya ukweli au kupewa maisha, au kusubiri tu bila matumaini, au katika majuto machungu mengi kiasi kwamba hamwezi kufikiri…. Huu uwezekano mbadala hauwezi kuepukika kabisa kwa mtu yeyote kati yenu.

4 Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu ambaye anamiliki kiti ambacho kwacho kwa kweli mnamwabudu Mungu; mnajitumbukiza katika dunia ya uasherati na maovu, kuchanganya ndani ya imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili, mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yanapingana nayo. Hivyo kile Ninachotumai kwenu ni kuwa muweze kuletwa kwa njia ya mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba muweze kujitunza, muweze kujiangalia, si kuweka mkazo mwingi sana juu ya hatima yenu kiasi kwamba muitazame mienendo na dhambi zenu kwa kutojali.

Umetoholewa kutoka katika “Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 980 Umepungukia Kaisi Kipi Matakwa ya Mungu?

Inayofuata: 982 Matokeo ya Makosa ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp