873 Jinsi Kazi ya Mungu Ilivyo Ngumu

1 Jinsi kazi Yake duniani ilivyo ngumu! Hatua za kazi ya Mungu duniani zinahusisha shida kubwa: Kwa ajili ya udhaifu wa mwanadamu, upungufu, utoto, ujinga na kila kitu cha mwanadamu, Mungu hufanya mipango yenye uangalifu na hufikiria kwa makini. Mwanadamu ni kama duma wa kutisha ambaye mtu hathubutu kumtega au kumchokoza; anapoguswa tu anauma, au vinginevyo anaanguka chini na kupoteza mwelekeo wake, na ni kana kwamba, akipoteza umakini kidogo tu, anarudia uovu tena, au anampuuza Mungu, au anakimbia kwa wazazi wake walio kama nguruwe na mbwa kuendeleza mambo machafu ya miili yao. Ni kizuizi kikubwa kiasi gani!

2 Katika kila hatua ya kazi Yake, Mungu anakabiliwa na ushawishi, na takribani katika kila hatua Mungu anakumbana na hatari kubwa. Maneno yake ni ya kweli na ya uaminifu, na bila uovu, lakini nani yupo tayari kuyakubali? Nani yupo tayari kutii kikamilifu? Inavunja moyo wa Mungu. Anafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwanadamu, Anasongwa na wasiwasi kuhusu maisha ya mwanadamu na Anauonea huruma udhaifu wa mwanadamu. Amevumilia shida nyingi katika kila hatua ya kazi Yake, kwa kila neno Analozungumza; Yupo katikati ya mwamba na sehemu ngumu, na kufikiria juu ya udhaifu wa mwanadamu, ukaidi, utoto, na vile alivyo hatarini wakati wote … tena na tena. Nani amewahi kulijua hili? Nani anaweza kuwa na imani? Nani anaweza kufahamu?

3 Anachukia dhambi za wanadamu daima, na ukosefu wa uti wa mgongo, mwanadamu kutokuwa na uti wa mgongo, ndiko kunamfanya kuwa na hofu juu ya hatari aliyonayo mwanadamu, na kutafakari njia zilizopo mbele ya mwanadamu; siku zote, anapoangalia maneno na matendo ya mwanadamu, je, yanamjaza huruma, hasira, na siku zote vitu hivi vinamletea maumivu moyoni Mwake. Hata hivyo, wasio na hatia wamekuwa wenye ganzi; kwa nini ni lazima Mungu siku zote afanye vitu kuwa vigumu kwao? Mwanadamu dhaifu, ameondolewa kabisa uvumilivu; kwa nini Mungu awe na hasira isiyopungua kwa mwanadamu? Mwanadamu aliye dhaifu na asiye na nguvu hana tena uzima hata kidogo; kwa nini Mungu anamkaripia siku zote kwa ukaidi wake? Nani anayeweza kuhimili matishio ya Mungu mbinguni?

4 Hata hivyo, mwanadamu ni dhaifu, na yupo katika dhiki sana, Mungu ameisukuma hasira Yake ndani kabisa moyoni Mwake, ili kwamba mwanadamu ajiakisi mwenyewe taratibu. Ilhali mwanadamu, aliyepo katika matatizo makubwa, hazingatii hata kidogo mapenzi ya Mungu; amedondoshwa miguuni na mfalme mzee wa pepo, na bado haelewi kabisa, siku zote anajiweka dhidi ya Mungu, au si moto wala baridi kwa Mungu. Mungu amezungumza maneno mengi sana, lakini nani ambaye ameyazingatia?

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 872 Mungu Huvumilia Aibu Kubwa

Inayofuata: 874 Kila Kitu Ambacho Mungu Humfanyia Mwanadamu Ni Cha Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp