Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

235 Nimeona Jinsi Ukweli Ulivyo wa Thamani

1 Baada ya miaka michache ya imani nilielewa mafundisho fulani ya kiroho. Nilidhani nilielewa ukweli na kupata uhalisi wake. Nilitekeleza wajibu wangu kidogo na kila mara nilijionyesha. Nilifuatilia jina na hadhi kwa moyo wangu wote, kila wakati nikijilinganisha na wengine. Ingawa nimeteseka na kujitumia kazini, yote yalikuwa ili niheshimiwe na wengine. Nimejitahidi katika fedheha lakini kwa ajili ya sifa na hadhi tu, lakini nilidhani nilikuwa mwaminifu kwa Mungu. Naonekana mnyenyekevu na mvumilivu, lakini asili yangu ni ya kiburi na kujidai sana. Sasa kwa kuwa nimepitia hukumu na kuadibu kwa Mungu hatimaye nimegutushwa. Katika miaka hii yote ya Imani, tabia yangu ya maisha haijabadilika, mimi bado ni wa Shetani.

2 Katika majaribu na usafishaji naona jinsi nilivyo mwasi. Mimi ni duni kama mnyoo, bado natupa kila kitu katika kutafuta hadhi na jina. Mara nyingi mimi hujitahidi kupata sifa ya wengine ili nifurahie. Siku zote nataka kuwa kiongozi ili niweze kutawala watu wateule wa Mungu, kwa kweli sina mantiki. Maneno ya Mungu yanahukumu upotovu na uovu wa wanadamu na yanafichua haki Yake. Mungu anafichua ukweli wa upotovu wa wanadamu, bila kuacha chochote. Mwishowe nimeona chanzo cha giza, uovu, na upotovu wa dunia. Binadamu wamepotoshwa sana na Shetani hatufanani kabisa na mwanadamu. Nina bahati sana kwamba hukumu ya Mungu imeniletea utakaso na wokovu, nimeona jinsi upendo wa Mungu ulivyo wa kweli.

3 Kwa kupitia maneno ya Mungu hatimaye nimeelewa mapenzi Yake. Hukumu, majaribio, na usafishaji wa maneno ya Mungu yote ni ili kumtakasa binadamu. Ukweli wote ambao Mungu anaonyesha ni zawadi Yake ya uzima kwa wanadamu. Kwa kupata nuru na hukumu ya maneno ya Mungu, nachukia upotovu wangu mwenyewe zaidi. Nimeona jinsi ukweli ulivyo wa thamani kweli, unaweza kuwasafisha na kuwakamilisha watu. Natamani kuacha kila kitu kutafuta na kupata ukweli na kujifanya upya. Haijalishi mateso yangu au usafishaji wangu ulivyo mkubwa, nitamfuata Kristo hadi mwisho kabisa. Haijalishi mateso yangu yalivyo makubwa, nitatimiza wajibu wangu kumtukuza Mungu hadi pumzi yangu ya mwisho. Upendo wa Mungu tu ndio halisi, nitamshukuru na kumsifu Mungu daima kwa dhati.

Iliyotangulia:Bila Kufuatilia Ukweli, Kutofaulu Hakuwezi Kuepukika

Inayofuata:Nampenda Mungu Zaidi Baada ya Kupitia Hukumu Yake

Maudhui Yanayohusiana

 • Upendo Safi Bila Dosari

  1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vizuizi au ba…

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. 1 …

 • Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu

  1 Ni Muumba pekee anayeshiriki na binadamu mapatano ya huruma na upendo yasichovunjika. Ni Yeye pekee Anayetunza viumbe Wake wote, vuimbe Wake wote. K…