560 Jinsi ya Kuelewa Asili ya Binadamu

1 Inapofikia kujua asili ya wanadamu, kitu cha muhimu zaidi ni kuijua kutoka kwa mtazamo wa maoni yao ya dunia, maoni ya maisha, na maadili. Wale wote walio wa ibilisi wote huishi kwa ajili yao wenyewe. Mitazamo yao ya maisha na kanunizinatoka kwa misemo ya Shetani, kama vile, “Kila mtu kivyake, na ibilisi achukue ya nyuma kabisa.” Maneno yaliyonenwa na hao ibilisi wafalme, wakuu, na wanafalsafa wa dunia yamekuwa maisha yao. Hasa, maneno mengi ya Konfyushasi, ambaye anatangazwa na watu wa Kichina kuwa “mtu mwenye hekima” yamekuwa maisha ya watuyamekuwa maisha ya watu. Pia kuna methali maarufu ya Ubudha na Utao, na misemo maarufu zaidi ya inayosemwa mara kwa mara ya watu mbalimbali mashuhuri; haya yote ni muhtasari wa falsafa ya Shetani na asili ya Shetani. Pia ni vielezo vizuri sana na maelezo ya asili ya Shetani.

2 Sumu hizi ambazo zimetiliwa mioyoni mwa wanadamu zote hutoka kwa Shetani; hakuna hata chembe yao inayotoka kwa Mungu. Uongo na upuuzi kama huu pia ni upinzani wa moja kwa moja kwa neno la Mungu hasa. Ni wazi kabisa kuwa uhalisi wa vitu vyote vyema hutoka kwa Mungu, na vitu vyote hivyo hasi ambavyo huwatia sumu wanadamu hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, unaweza kumaizi asili ya mtu na yeye yu wa nani kutoka kwa maoni yake ya maisha na maadili. Wanadamu wamepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na inaweza kuonekana kwamba asili ya mwanadamu imepotoka, ni yenye uovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—kwa jumla ni asili inayomsaliti Mungu. Hii ndiyo maana watu humkataa Mungu na humpinga Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 559 Elewa Hali Zako za Kweli ili Ujielewe

Inayofuata: 561 Jinsi ya Kuchunguza Asili Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp