809 Jinsi ya Kuitemba Njia ya Petro

1 Kwa ufupi, kuichukua njia ya Petro katika imani ya mtu kunamaanisha kuitembea njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kupata kujijua na kubadilisha tabia yako kwa kweli. Ni kwa kuitembea njia ya Petro tu ndipo mtu atakuwa katika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe jinsi hasa ya kuitembea njia ya Petro, na vilevile jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia na vitu vyote vya mwili wake mwenyewe. Yeye lazima ajitolee kwa moyo wote; yaani, lazima ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, alenge kula na kunywa maneno ya Mungu, azingatie kutafuta ukweli na kutafuta madhumuni ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi na muhimu zaidi ya utendaji. Hilo ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu anaweza kufanikisha matokeo bora zaidi.

2 Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu kimsingi kunajumuisha kutafuta ukweli, kutafuta nia za Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka katika maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini, sembuse kuzingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alitilia maanani kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na vile vile kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Petro pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka katika maneno ya Mungu, na vile vile asili potovu ya mwanadamu na dosari yake halisi hivyo kufikia vipengele vyote vya matakwa ya Mungu kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. petro alikuwa na vitendo vingi sahihi vilivyofuata maneno ya Mungu; hili lililingana zaidi na mapenzi ya Mungu, na ni njia bora zaidi ambayo mtu angeshirikiana huku akipitia kazi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 808 Petro Alimjua Mungu Vyema Zaidi

Inayofuata: 810 Petro Daima Alifuatilia Kumjua Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp