793 Dhana na Fikira Hazitawahi Kukusaidia Kumjua Mungu
1 Tabia ya haki ya Mungu ni hali halisi ya kweli ya Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuandikwa na binadamu. Tabia Yake ni tabia Yake ya haki na haina uhusiano au miunganisho yoyote na uumbaji wowote ule. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na hali halisi Yake havitabadilika.
2 Kumjua Mungu si kujua kifaa; si kuchunguza kitu, wala si kuelewa mtu. Kama mwanadamu atatumia dhana au mbinu yake ya kujua kifaa au kuelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu.
3 Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na hali halisi ya kweli ya Mungu. Hutawahi kufanikiwa kama utategemea kufikiria kwako ili kuelewa hali halisi ya Mungu. Njia ya pekee ni hivi: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya hamu yako ya kutaka ukweli.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili