469 Umuhimu wa Maneno ya Mungu
1 Waumini katika Mungu wanapaswa, angalau, kuwa na tabia njema kwa nje; la muhimu zaidi ni kuwa na maneno ya Mungu. Bila kujali chochote, kamwe huwezi kuyaacha maneno Yake. Kumjua Mungu na kutimiza nia Zake vinafanikishwa kupitia katika maneno Yake. Katika siku zijazo, kila taifa, dhehebu, dini, na sehemu zitashindwa kwa njia ya maneno ya Mungu. Mungu atazungumza moja kwa moja, na watu wote watashikilia maneno ya Mungu mikononi mwao, na kwa njia hii, binadamu watakamilishwa. Ndani na nje, maneno ya Mungu yanapenyeza kotekote: Binadamu watazungumza maneno ya Mungu kwa vinywa vyao, watende kulingana na maneno ya Mungu, na kuweka maneno ya Mungu ndani, wakisalia wamelowa na maneno ya Mungu ndani na nje. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa.
2 Wale wanaotimiza nia za Mungu na wanaweza kumshuhudia, hawa ni watu wanaomiliki maneno ya Mungu kama ukweli wao. Kuingia katika enzi ya Neno—Enzi ya Ufalme wa Milenia—ni kazi ambayo inatimizwa leo. Kuanzia sasa kuendelea, fanya mazoezi ya ushirika kuhusu maneno ya Mungu. Ni kwa njia ya kula na kunywa na pia kupitia maneno ya Mungu ndiyo utaweza kuishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu. Lazima uwe na uzoefu wa vitendo ili uwashawishi wengine. Ikiwa huwezi kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa huwezi kutoa ukweli huu na kumshuhudia Mungu, hii inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu hajafanya kazi ndani yako, na kwamba wewe hujakamilishwa. Huu ndio umuhimu wa maneno ya Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili