404 Kitu Muhimu Sana Ambacho Waumini Katika Mungu Wanapaswa Kupata

1 Mungu ametoa maisha Yake kwa wanadamu bure, hivyo kuyafanya yawe maisha yao. Basi ni nini ambacho wanadamu wamepata kutoka kwa Mungu? Ni maisha ya Mungu! Kwa hivyo, kile ambacho binadamu wanapata kutoka kwa Mungu ni cha thamani mno, na, wakati Mungu anawapa binadamu kitu hiki cha thamani mno, Mungu hapati chochote; wanufaishwa wakubwa zaidi ni binadamu. Wanadamu hupata faida kubwa zaidi; wao ndio wanufaishwa wakubwa zaidi.

2 Kwa kulinganisha faida kubwa kama hiyo inayopatwa na wanadamu na ahadi ambazo wanafikiria Mungu angewapatia, au kwa bahati nzuri wanayoitamani, ni kipi ambacho binadamu wanahitaji zaidi? Ni kipi kilicho muhimu zaidi: Matamanio yako ya baraka, au kuishi kweli kwa kudhihirisha maisha ambayo Mungu amekupa? Ni nini kinachoweza kukuruhusu uje mbele za Mungu na umwabudu kweli, ili asije Akakuchukia, kukuacha, au kukuadhibu? Ni nini kinachoweza kukuruhusu uishi milele?

3 Ni kwa kukubali tu maisha yanayotoka kwa Mungu ndipo unaweza kuyaokoa maisha yako. Ukiyapata maisha haya, basi maisha yako yatakuwa bila mwisho; huu ni uzima wa milele. Ikiwa mtu hajapata uzima utokao kwa Mungu, basi lazima afe, na kwamba maisha yao yanaweza kutamatishwa. Je, maisha yawezayo kutamatika yanaweza kuitwa uzima wa milele? Unapata uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Je, tamaa yako ya baraka inaweza kuwa mbadala wowote? Je, tamaa za watu za baraka zinaweza kuwaokoa kutokana na kufa?

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Ndiye Mnufaishwa Mkuu wa Mpango wa Usimamizi wa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 403 Umepata Mengi Sana Kwa Sababu ya Imani

Inayofuata: 405 Hii ni Imani ya Kweli Katika Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp