862 Mungu Mwenye Mwili Anapendeza Sana
1 Inaweza kusemekana kwamba baada ya Mungu kuwa mwili, baada ya Yeye binafsi kupitia maisha miongoni mwa wanadamu na kuwa na maisha ya binadamu, na baada ya Yeye kuona uharibifu wa tabia wa wanadamu na hali ya maisha ya binadamu, Mungu katika mwili alihisi kwa kina zaidi jinsi mwanadamu alikuwa asiyejiweza, mwenye masikitiko na wa kuonewa huruma. Mungu alipata huruma zaidi kwa hali ya binadamu kwa sababu ya ubinadamu Wake wakati akiishi katika mwili, kwa sababu ya silika Zake katika mwili. Hili lilimsababisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya wafuasi Wake.
2 Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili