180 Kupata Mwili kwa Mungu ni Hasa ili Kuonyesha Neno Lake

1 Ufahamu wa watu leo kuhusu Mungu wa vitendo bado unaegemea upande mmoja, na ufahamu wao kuhusu umuhimu wa kupata mwili bado ni mdogo sana. Kuhusu suala la mwili wa Mungu, watu huona kupitia katka kazi na maneno Yake kwamba Roho wa Mungu ana mengi, kwamba yeye ni tajiri. Leo unaweza kumwabudu huyu mtu, lakini kwa hakika unamwabudu Roho. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa kinachopaswa kufahamiwa kuhusu ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliyepata mwili: kujua kiini cha Roho kupitia kwa mwili, kujua kazi ya uungu ya Roho katika mwili na kazi ya wanadamu katika mwili, kukubali maneno yote ya Roho na matamshi katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anauelekeza mwili na kudhihirisha uwezo Wake katika mwili.

2 Kimsingi Mungu alitoka mbinguni kuja duniani ili kuonyesha maneno ya Mungu kupitia mwili, kukamilisha kazi ya Roho wa Mungu kwa kutumia mwili. Hivi ni kusema kuwa, mwanadamu anapata kumjua Roho aliye mbinguni kupitia kwa mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumemwondoa Mungu asiye yakini kutoka katika dhana za wanadamu; ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utiifu wao kwa Mungu; na kupitia kwa uungu wa kazi ya Roho wa Mungu katika Mwili, na kazi ya wanadamu katika miili, mwanadamu hupata ufunuo, na kuongozwa, na mabadiliko hupatikana katika tabia ya maisha yake. Hii tu ndiyo maana halisi ya ujio wa Roho katika mwili, kimsingi, ili kwamba watu waweze kushirikiana na Mungu, kumtegemea Mungu, na kuupata ufahamu wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 179 Mungu Anapokuwa Mwili Tu Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake

Inayofuata: 181 Mamlaka na Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp