110 Melezo ya Ndani ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

1 Kazi ya awali ya hatua tatu za kazi ya Mungu ilifanywa moja kwa moja na Roho, na wala si mwili. Hata hivyo, kazi ya mwisho ya hatua tatu za kazi ya Mungu, inafanywa na Mungu mwenye mwili, na wala haifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya ukombozi ya hatua ya katikati pia imefanywa na Mungu mwenye mwili. Katika kazi yote ya usimamizi, kazi muhimu sana ni wokovu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Kazi muhimu ni kumshinda kabisa mwanadamu aliyepotoka, na hivyo kurejesha heshima ya awali ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumruhusu kufikia maisha ya kawaida, ni sawa na kusema, maisha ya kawaida ya kiumbe wa Mungu. Kazi hii ni muhimu, na ni kiini cha kazi ya usimamizi.

2 Hatua mbili hizi za kazi ya Mungu zinafanywa na Mungu katika utambulisho Wake katika mwili kwa sababu zina umuhimu sana katika kazi nzima ya usimamizi. Inaweza kusemwa kuwa, bila kazi ya Mungu mwenye mwili katika hatua mbili hizi, kazi nzima ya usimamizi ingefikia kikomo kwa ghafla, na kazi ya kumwokoa mwanadamu isingekuwa kitu isipokuwa maneno matupu. Haijalishi kazi hii ni muhimu au si muhimu lakini imejikita katika mahitaji ya mwanadamu, na uhalisi wa upotovu wa mwanadamu, na uzito wa kutotii kwa Shetani na usumbufu wake katika kazi. Mhusika sahihi ni yule anayeifanya kazi ametabiriwa na asili ya kazi inayofanywa na huyo mfanyakazi, na umuhimu wa kazi.

3 Kuna umuhimu na msingi katika kila hatua ya kazi. Siyo fikra tu zisizo na msingi, na wala hazifanywi kiholela; kuna hekima fulani ndani yake. Huo ndio ukweli wa kazi zote za Mungu. Bila kujali kama ni kazi ya Roho au kazi ya Mungu mwenye mwili, kila kazi inajumuisha mpango wa kazi Yake. Hafanyi kazi bila kuwa na msingi, na hafanyi kazi isiyokuwa na maana. Roho anapofanya kazi moja kwa moja, ni kwa malengo Yake, na Anapokuwa mwanadamu (ambayo ni sawa na kusema, Anapobadilisha ganda Lake la nje) kufanya kazi, ni zaidi hata na lengo Lake. Kwa sababu ipi nyingine kwa urahisi Abadilishe utambulisho Wake vivi hivi tu? Kwa sababu ipi nyingine kwa urahisi Abadilike awe mtu ambaye anachukuliwa kuwa ni duni na kuteswa?

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 109 Kazi Nzima ya Wokovu

Inayofuata: 111 Mungu Ndiye Mkuu wa Mpango wa Usimamizi wa Miaka Elfu Sita

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp