Sura ya 5

Mungu anapoweka mahitaji kwa wanadamu ambayo ni magumu kwao kueleza, na maneno Yake yanapogonga moja kwa moja katika moyo wa mwanadamu na watu wanatoa mioyo yao ya dhati ili Afurahie, basi Mungu huwapa watu nafasi ya kutafakari, kufanya uamuzi, na kutafuta njia ya kutenda. Kwa njia hii, wote ambao ni watu Wake kwa mara nyingine, ngumi zikiwa zimekunjwa kwa ujasiri, watatoa nafsi zao zote kwa Mungu. Baadhi, labda, wanaweza kuunda mpango na kuanzisha ratiba ya kila siku, wanapojiandaa kujisisimua na kwenda kazini, wakitoa sehemu yao ya nguvu kwa mpango wa usimamizi wa Mungu, ili kuleta utukufu kwa mpango huu na kuharakisha hitimisho lake. Na, kama vile watu wanavyojipata katika hali hii ya kisaikolojia, wakishikilia mambo haya kwa karibu akilini mwao wakati wanapokuwa wakiendelea na kazi zao, wanapozungumza, na wanapokuwa wakifanya kazi, Mungu, kwa haraka akifuatilia hili, Huanza kusema tena: “Wakati Roho Wangu anatoa sauti, anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, nyinyi mnalifahamu hili?” Kadri mwanadamu alivyo na uamuzi zaidi, ndivyo atakavyokuwa na tamaa zaidi ya kufahamu mapenzi ya Mungu na ndivyo atakavyotamani kwa ari zaidi Mungu aweke madai kwake; na hivyo Mungu atawapa watu kile ambacho wanataka, Akitumia fursa hii kutoa maneno Yake, yaliyokuwa yamewekwa tayari kwa muda mrefu, kwa maficho ya ndani kabisa ya nafsi zao. Ingawa maneno haya yanaweza kuonekana kuwa makali au ya kukwaruza kiasi, kwa binadamu ni matamu zaidi kulinganishwa na kitu chochote. Mara moja, moyo unachanua kwa furaha, kana kwamba binadamu wako mbinguni, au wamepelekwa katika ulimwengu mwingine, paradiso ya hakika ya mawazo, ambako mambo ya nje ya ulimwengu hayawaathiri tena binadamu. Ili kwamba watu wasizungumze tena, kama walivyokuwa na tabia ya kufanya zamani, kwa nje na kutenda kwa nje, na hivyo kushindwa kuweka misingi wa kufaa: ili kuiepuka hatima hii, wakati kile ambacho watu wanatamani mioyoni mwao kimefanikiwa, na zaidi wanapojiandaa kwenda kazini kwa shauku kubwa, Mungu bado anabadili njia Yake ya kuzungumza kulingana na hali yao ya kisaikolojia, na, kwa ufupi na bila kujizuia, Hubainisha shauku yote na sherehe ya kidini ndani ya mioyo yao. Kama Mungu alivyosema: “Je, kweli mmeona umuhimu ulioko humu?” Ikiwa ni kabla au baada ya mwanadamu kuweka dhamira yake juu ya kitu fulani, haweki umuhimu mkubwa juu ya kumjua Mungu katika matendo Yake au kwa maneno Yake, lakini badala yake anaendelea kutafakari swali hili: “Ninaweza kumfanyia nini Mungu? Hilo ndilo suala muhimu!” Hii ndiyo maana Mungu anasema: “Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia ya aibu, sembuse mantiki yoyote!” Mara tu baada ya Mungu kusema maneno haya, mara moja watu hutambua, na kana kwamba wamepatwa na mshtuko wa umeme, wanaharakisha kuificha mikono yao kwa vifua vyao, wakiwa na uoga mwingi kuchochea ghadhabu ya Mungu mara ya pili. Kuongezea kwa hili, Mungu amesema pia: “Siku moja, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu. Usithubutu kunidanganya, ukifikiri kwamba umesimama kwa ajili ya ushuhuda Wangu!” Wanaposikia maneno kama haya, watu wanaogopa hata zaidi, kama vile wangeogopa wakiwa wamemwona simba. Wanajua vizuri kabisa mioyoni mwao. Wao kwa upande mmoja wana wasiwasi wasiliwe na simba huku kwa upande mwingine wanahisi kutojua pa kutorokea. Wakati huu, mpango ndani ya moyo wa mwanadamu hupotea usionekane tena, kabisa na kikamilifu. Kupitia maneno ya Mungu, ninahisi kama kwamba ninaweza kuona kila kipengele cha aibu ya binadamu: Tabia ya kuinamisha kichwa na kuona aibu, kama mtahiniwa ambaye ameanguka mtihani wa kuingia chuo kikuu, maadili yake ya fahari sana, familia yenye furaha, siku za usoni zenye ufanisi, na kadhalika na kadhalika, yote yaligeuka—pamoja na Mipango Minne ya Kufanya kuwa ya Kisasa kabla ya Mwaka 2000—kuwa maongezi matupu, yakisababisha mandhari ya kufikirika katika filamu ya sayansi ya ubunifu. Hii ni ili kubadilishana mambo ya kukaa tu na yale ya utendaji kazi, kuwafanya watu, ndani ya kutojishughulisha kwao, kusimama mahali ambapo Mungu amewaweka. Jambo muhimu la pekee ni ukweli kwamba wanadamu wanaogopa sana kupoteza cheo hiki; hivyo basi wanakwamilia beji zao za ofisi kwa bidii yao yote, wakiwa na uoga mwingi kuwa mtu anaweza kujaribu kuzipokonya kutoka kwao. Wakati binadamu wako katika hali hii ya akili, Mungu hana wasiwasi kuwa watakuwa wenye kukaa tu, na kwa hiyo inavyostahili Yeye hubadili maneno Yake ya hukumu kuwa maneno ya kuhoji. Hawapi watu fursa ya kupunga hewa tu, lakini pia Anawapa fursa ya kuchukua matarajio waliyokuwa nao kabla ya sasa na kuyatayarisha kwa ajili ya kuyaangalia baadaye: Kile ambacho hakifai kinaweza kubadilishwa. Hii ni kwa sababu Mungu bado Hajaanza kazi Yake—hii ni bahati nzuri katikati ya bahati mbaya sana—na, zaidi ya hayo, Hawahukumu. Kwa hiyo acha niendelee kumpa ibada yangu yote!

Halafu, hupaswi kamwe kwa sababu ya hofu yako, kuweka kando maneno ya Mungu. Angalia uone kama Mungu ana mahitaji yoyote mapya. Kwa hakika, utagundua aina hii ya mahitaji: “Kuanzia wakati huu na kuendelea, katika mambo yote lazima uingie katika ukweli wa kutenda; kupiga domo tu, kama ulivyokuwa ukifanya, hakutakusaidia tena.” Ndani yake pia kunadhihirishwa hekima ya Mungu. Mungu daima Amewalinda shahidi Wake mwenyewe, na wakati ukweli wa maneno ya zamani umefikia hitimisho lake, hakuna mtu yeyote anayeweza kufahamu ujuzi wa “ukweli wa kutenda.” Hii inatosha kuthibitisha ukweli wa kile ambacho Mungu alisema “Ninaanza kufanya kazi hiyo Mwenyewe.” Inahusiana na maana halisi ya kazi katika uungu, na pia inahusiana na sababu kwa nini wanadamu, baada ya kufikia hatua mpya ya mwanzo, bado hawawezi kuelewa maana halisi ya maneno ya Mungu. Hii ni kwa sababu, zamani, idadi kubwa ya watu wangeshikilia ukweli katika maneno ya Mungu, ilhali leo hawana ufahamu juu ya ukweli wa kutenda, lakini wanaelewa tu vipengele vya juu juu vya maneno haya bila kuelewa asili yao. Hata muhimu zaidi, ni kwa sababu leo, katika ujenzi wa ufalme, hakuna mtu anayeruhusiwa kuingilia kati, lakini kutii tu amri ya Mungu kama roboti. Kumbuka hili vizuri! Kila wakati ambao Mungu huleta mambo ya zamani, Yeye huanza kusema kuhusu hali halisi ya leo; hii ni namna ya kuzungumza ambayo inafanya tofauti kubwa sana kati ya kile kinachokuja kabla na kile kinachokuja baadaye, na kwa sababu hii inaweza kufikia matunda bora hata zaidi, ikiwawezesha watu kuiweka hali ya sasa sambamba na ile ya wakati uliopita, na kwa njia hii kuepuka kuchanganya tofauti iliyopo kati ya hizi mbili. Huu ni upande mmoja wa hekima ya Mungu, na lengo lake ni kufikia matunda ya kazi. Baada ya hili, Mungu kwa mara nyingine Hufichua ubaya wa wanadamu, ili kwamba binadamu hawatasahau kamwe kula na kunywa maneno ya Mungu kila siku, na hata muhimu zaidi ili kwamba kila siku watajijua na kuchukua hili kama somo ambalo wanapaswa kujifunza kila siku.

Anapomaliza kuzungumza maneno hayo, Mungu amefanikisha matokeo ambayo Alinuia awali. Na kwa hiyo, bila kujali zaidi kama binadamu wamemwelewa au la, Yeye huipitia hili upesi sana kwa maneno machache, kwa sababu kazi ya Shetani haina uhusiano wowote na binadamu—kuhusu hili binadamu hawana ufahamu. Sasa, ukiacha ulimwengu wa roho, angalia zaidi jinsi Mungu anavyoweka mahitaji Yake kwa binadamu: “Ninapopumzika katika makaazi Yangu, Mimi huchunguza kwa karibu: Watu wote duniani wamo katika pilikapilika, ‘wakisafiri duniani kote’ na kukimbia huku na kule, yote kwa ajili ya hatima yao, maisha yao ya baadaye. Lakini hakuna hata mmoja ana nguvu ya kutosha kwa ajili ya kuujenga ufalme Wangu, hata nguvu kiasi ambayo mtu hutumia kuvuta pumzi.” Baada ya kubadilishana mambo haya ya kawaida na wanadamu, Mungu bado hajali kuwahusu, lakini Anaendelea kuzungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, na kwa njia ya maneno haya, Anafichua hali za jumla za maisha ya jamii ya wanadamu. Ni wazi kuona, kutokana na “kusafiri duniani kote” na “kukimbia huku na kule,” kwamba maisha ya binadamu hayana maudhui. Isingekuwa kwa ajili ya wokovu wenye nguvu wa Mungu, wale waliozaliwa katika familia ya chini na nje ya mstari wa kifalme wa China wangeishi maisha yote bure hata zaidi na ni heri waanguke Kuzimu na jahanamu kuliko kuja ulimwenguni. Chini ya utawala wa joka kuu jekundu, wao, bila kujua wenyewe, wamekosa dhidi ya Mungu na hivyo, kwa kawaida na tena bila kujua, wamekabiliwa na kuadibu kwa Mungu. Kwa sababu hii, Mungu amewachukua “waliookolewa kutokana na dhiki” na “wasio na shukrani” na kuwaweka pamoja kwa kuwalinganisha, kwamba wanadamu waweze kujitambua vizuri zaidi, na kuunda kutoka kwa hili foili kwa neema Yake ya kuokoa. Je! Hili halileti matokeo yanayofaa zaidi? Bila shaka, Sihitaji kusema kwa wazi sana, watu wanaweza, kutokana na yaliyomo katika mazungumzo ya Mungu, kuonyesha kipengele cha kukashifu, na tena, kipengele cha wokovu na rufaa, na hata tena, maonyesho mafupi ya huzuni. Wanaposoma maneno haya, watu bila kujua huanza kuhisi wenye mfadhaiko, na hawana budi ila kutoa machozi.... Lakini Mungu hatazuiliwa kwa sababu ya hisia chache za huzuni, wala Yeye, kwa sababu ya upotovu wa watu wote, Hataacha kazi Yake katika kuwafundisha watu Wake nidhamu na kuweka mahitaji kwao. Kwa sababu hii, mada Zake mara moja hugusia juu ya hali kama hizo za leo, na zaidi ya hayo Anatangaza kwa binadamu uadhama wa amri Zake za utawala, ili kwamba mpango Wake uendelee kwenda mbele. Hii ndiyo sababu, baada ya hili kwa kasi ya kutosha na kumkunja samaki angali mbichi, Mungu anatangaza wazi wakati huu muhimu katiba ya nyakati, katiba ambayo inapaswa kusomwa kwa uangalifu kwa karibu kwa kila kifungu kabla binadamu waweze kuelewa mapenzi ya Mungu. Hakuna haja ya kuingia zaidi katika hili sasa—lazima tu wasome kwa makini zaidi.

Leo, nyinyi—hili kundi la watu hapa—ndio pekee ambao mnaweza kuona kwa kweli maneno ya Mungu. Hata hivyo, katika kumjua Mungu, watu wa leo wamebaki nyuma sana ya mtu yeyote katika enzi zilizopita. Kutokana na hili ni wazi kabisa kiwango cha juhudi ambazo Shetani amewekeza kwa watu katika miaka hii elfu kadhaa, na kiwango ambacho zimewapotosha wanadamu, ambacho ni kikubwa sana kiasi kwamba, hata ingawa Mungu amesema maneno mengi sana, bado binadamu hawamwelewi wala hawamjui Mungu, lakini badala yake wanathubutu kusimama na kumpinga hadharani. Na hivyo Mungu mara nyingi huwafanya watu wa zamani kuwa kama ulinganishi kwa watu wa leo, ili kuwapa watu wa leo, licha ya wao kuwa wasiohisi na wapumbavu, nafasi ya uhakika ya marejeo. Kwa sababu wanadamu hawana maarifa ya Mungu, na kwa sababu hawana imani ya kweli ndani Yake, Mungu amewahukumu binadamu kuwa hawana sifa na mantiki, na hivyo, mara kwa mara, Amewaonyesha watu uvumilivu na kuwapa wokovu. Pigano linapiganwa kwa njia hii katika ulimwengu wa roho: Ni tumaini lisilofanikiwa la Shetani kuwapotosha wanadamu kwa kiwango fulani, kuufanya ulimwengu kuwa mbaya na mwovu, na hivyo kumvuta mwanadamu ndani ya matope na kuuharibu mpango wa Mungu. Lakini mpango wa Mungu sio kuwafanya binadamu wote kuwa watu wanaomjua, bali badala yake kuchagua sehemu ya kuwakilisha yote, na kuacha wengine kama bidhaa taka, kama bidhaa zilizoharibika, wanaofaa kutupwa kwenye rundo la takataka. Na hivyo, ingawa kutoka kwa mtazamo wa Shetani kuwamiliki watu wachache kunaonekana kuwa fursa nzuri kabisa ya kuuharibu mpango wa Mungu, je, zuzu kama yeye anawezaje kujua kuhusu nia ya Mungu? Hii ndiyo maana Mungu alisema, zamani, “Nimeufunika uso Wangu ili kuepuka kuangalia ulimwengu huu.” Tunajua kidogo kuhusu hili, na Mungu hahitaji kuwa wanadamu wawe na uwezo wa kufanya chochote, badala yake kwamba watambue kile Anachofanya kama cha muujiza na kisichoweza kueleweka na kumcha sana katika mioyo yao. Ikiwa, kama mtu anavyofikiria, Mungu angemwadibu bila kujali hali, basi dunia nzima ingekuwa imeangamia kitambo. Je, si huku kungemaanisha kuanguka ndani ya mtego wa Shetani? Na hivyo Mungu hutumia maneno Yake tu kufikia matunda Aliyo nayo mawazoni; mara chache sana kuna ujio wa ukweli. Je! Huu sio mfano wa kile Alichosema: “Kama Singeonea huruma ukosefu wenu wa sifa za kustahili, mantiki, na ufahamu, basi nyote mngeangamia katika kuadibu Kwangu, kutokuwepo tena. Lakini hadi wakati kazi Yangu hapa duniani itakapomalizika, Nitabaki mwenye huruma kwa wanadamu?”

Iliyotangulia: Sura ya 4

Inayofuata: Sura ya 6

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp