Sura ya 27

Leo, maneno ya Mungu yamefikia kilele chake, ambako ni kusema, sehemu ya pili ya enzi ya hukumu imefikia kilele chake. Lakini sio kilele cha juu kabisa. Wakati huu, sauti ya Mungu imebadilika, si ya kudhihaki wala ya ucheshi, na haigongi au kulaani; Mungu ametuliza sauti ya maneno Yake. Sasa, Mungu anaanza “kubadilishana maoni” na mwanadamu. Mungu anaendeleza kazi ya enzi ya hukumu na pia kufungua njia ya sehemu inayofuata ya kazi, ili sehemu zote za kazi Yake zipatane. Kwa upande mmoja, Anasema kuhusu “ukaidi na uhalifu sugu wa mwanadamu,” na kwa upande mwingine, Anasema “katika furaha na huzuni ya kutengana na kuunganika Kwangu na mwanadamu”—vyote viwili vinachochea mjibizo katika mioyo ya watu, vikiigusa hata mioyo iliyo baridi kabisa ya binadamu. Lengo la Mungu katika kusema maneno haya hasa ni kuwafanya watu wote waanguke chini mbele za Mungu, bila mnong’ono, mwisho kabisa, na baadaye tu “ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi.” Ufahamu kuhusu Mungu wa watu wa kipindi hiki unasalia wa juujuu kabisa, sio ufahamu wa kweli. Ingawa wanajikakamua kadri wawezavyo, hawawezi kufikia mapenzi ya Mungu; leo, maneno ya Mungu yamefikia upeo wake, lakini watu wanabakia katika hatua za mwanzo, na hivyo hawawezi kuingia katika matamko ya sasa hivi—ambalo linaonyesha kuwa Mungu na mtu ni tofauti kabisa. Kulingana na hili, wakati maneno ya Mungu yatamalizika watu wataweza tu kufikia viwango vya chini zaidi vya Mungu. Hii ndio njia ambayo Mungu hufanya kazi ndani ya watu hawa ambao wamepotoshwa kabisa na joka kubwa jekundu, na Mungu lazima afanye hivyo ili Atimize matokeo bora kabisa. Watu wa makanisa huzingatia maneno ya Mungu kiasi kidogo zaidi, lakini nia ya Mungu ni kwamba waweze kumjua Mungu katika maneno Yake—je, tofauti haipo? Hata hivyo, jinsi mambo yalivyo, Mungu hajali tena kuhusu udhaifu wa mwanadamu, na Anaendelea kusema bila kujali kama watu wanaweza kukubali maneno Yake au la. Kulingana na nia Yake, wakati maneno Yake yatamalizika utakuwa wakati ambapo kazi Yake duniani itakamilika. Lakini kazi hii ni tofauti na ya zamani. Wakati matamko ya Mungu yatamalizika, hakuna mtu atakayejua; wakati kazi ya Mungu itafika mwisho, hakuna mtu atakayejua; na wakati umbo la Mungu litabadilika, hakuna mtu atakayejua. Hivyo ndivyo hekima ya Mungu ilivyo. Ili kuepuka mashtaka yoyote kutoka kwa Shetani na kuingiliwa kokote na nguvu za uhasama, Mungu hufanya kazi bila mtu yeyote kujua, na wakati huu hakuna mjibizo miongoni mwa watu wa dunia. Ijapokuwa ishara za kugeuka sura kwa Mungu zilizungumziwa wakati mmoja, hakuna mtu anayeweza kulitambua hili, kwa kuwa mwanadamu amesahau jambo hili, naye halizingatii. Na kwa sababu ya mashambulizi kutoka ndani na nje—maafa ya ulimwengu wa nje na kuchomwa na kutakaswa na maneno ya Mungu—watu hawako radhi tena kumfanyia Mungu kazi, kwa sababu wanashughulika sana na shughuli zao wenyewe. Wakati watu wote wanakana ufahamu na ufukuziaji wa zamani, wakati watu wote wamejiona kwa dhahiri, watashindwa na nafsi zao wenyewe hazitakuwa na nafasi tena mioyoni mwao. Wakati huo tu ndio watu watatamani maneno ya Mungu kwa kweli, wakati huo tu ndio maneno ya Mungu yatakuwa na nafasi kweli katika mioyo yao, na wakati huo tu ndio maneno haya yatakuwa yamekuwa chanzo cha kuwepo kwao—na wakati huu, mapenzi ya Mungu yatakuwa yametimizwa. Lakini watu wa leo wako mbali sana na hilo. Baadhi yao wameweza kusonga kwa shida, na hivyo Mungu anasema huu ni “ukaidi sugu.”

Maneno yote ya Mungu yana maswali mengi. Kwa nini Mungu anaendelea kuuliza maswali kama hayo? “Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? …” Zamani, Mungu alifanya kazi kwa njia ya kuelezea mambo moja kwa moja au kuwa wazi moja kwa moja. Lakini baada ya watu kupitia maumivu mengi, hivyo Mungu hakuzungumza moja kwa moja. Kwa upande mmoja, watu wanaona kasoro zao wenyewe katika maswali haya, na kwa upande mwingine, wanafahamu njia ya kufanya mazoezi. Kwa sababu watu wote hupenda kula kile kinachopatikana kwa urahisi, Mungu ananena kama yanavyostahili mahitaji yao, Akiwapa mada za kutafakari, ili waweze kuzitafakari. Hii ni hali moja ya umuhimu wa maswali ya Mungu. Kwa kawaida, huu sio umuhimu wa baadhi ya maswali Yake, kwa mfano: “Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu?” Maswali kama haya huonyesha dhana zilizo katika vina vya mioyo ya watu. Ingawa midomo yao haisemi, kuna shaka ndani ya mioyo ya wengi wao, na wanaamini kwamba maneno ya Mungu yanawafafanua kama wasiokuwa na faida. Kwa kawaida, watu kama hao hawajijui, lakini hatimaye, watakubali kushindwa na maneno ya Mungu—hili haliepukiki. Kufuatia maswali haya, Mungu anasema pia “Nakusudia kusambaratisha mataifa yote yatawanyike, sembuse familia ya mwanadamu.” Watu wanapolikubali jina la Mungu, hivyo mataifa yote yatatetemeka, watu watabadili mawazo yao polepole, na katika familia mahusiano kati ya baba na mwana, mama na binti au mume na mke yatakoma kuwapo. Zaidi ya hayo, mahusiano kati ya watu katika familia yatakuwa ya kufarakana zaidi; watajiunga na familia kubwa, na ukawaida wa maisha ya takriban familia zote utatenganishwa. Na kwa sababu ya hili, dhana ya familia katika mioyo ya watu itazidi kuwa ya wasiwasi.

Kwa nini, katika maneno ya Mungu ya leo, mengi sana yametolewa kwa “kubadilishana hisia za moyoni” na watu? Kwa kawaida, hili pia ni kwa ajili ya kutimiza matokeo fulani, ambayo kutoka kwayo inaweza kuonekana kwamba moyo wa Mungu umejaa wasiwasi. Mungu anasema, “Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake?” Mungu anasema maneno haya kwa sababu moyo Wake umelemewa na huzuni. Kwa sababu watu hawawezi kuyajali kabisa mapenzi ya Mungu, na daima huwa ni wapotovu, na hawawezi kujizuia—wanafanya wapendavyo; kwa sababu wao ni duni sana, na daima wao hujisamehe, na hawajali kuhusu mapenzi ya Mungu. Lakini kwa sababu watu wamepotoshwa na Shetani hadi leo, na hawawezi kujikomboa, Mungu anasema: “Wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake?” Watu wanaishi katika mwili—katika kinywa cha mbwa mwitu mlafi. Kwa sababu ya hili, na kwa sababu watu hawajijui na daima wao hujiendeka na kujiingiza katika uzinzi, Mungu hana budi kuhisi wasiwasi. Kadri Mungu anavyowakumbusha watu hivyo, ndivyo wanavyohisi bora zaidi mioyoni mwao, na ndivyo wanavyokuwa radhi zaidi kushirikiana na Mungu. Wakati huo tu ndipo mwanadamu na Mungu watapatana, bila utengano wowote au umbali kati yao. Leo, wanadamu wote wanasubiri ujio wa siku ya Mungu, na kwa hiyo wanadamu hawajawahi kusonga mbele. Lakini Mungu anasema: “Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu.” Kwa maneno mengine, wakati Mungu atabadili umbo Lake, Mashariki itaangazwa kwanza na nchi ya Mashariki itakuwa ya kwanza kuchukua nafasi yake, baada ya hapo nchi zilizobaki zitafanywa upya kutoka kusini hadi kaskazini. Huu ndio utaratibu, na yote yatakuwa kwa mujibu wa maneno ya Mungu, na mara tu awamu hii itakapokuwa imekamilishwa watu wote wataona. Mungu hufanya kazi kulingana na utaratibu huu. Watakapoiona siku hii, watu watafurahi sana. Inaweza kuonekana kutoka kwa nia muhimu ya Mungu kwamba siku hii haiko mbali sana.

Katika maneno ya leo, sehemu ya pili na ya tatu zinachochea machozi ya uchungu kwa wote wanaompenda Mungu. Mioyo yao imegubikwa kivulini mara moja, na tangu wakati huu na kuendelea watu wote wamejaa huzuni kubwa mno kwa sababu ya moyo wa Mungu—baada tu ya Mungu kumaliza kazi Yake duniani, watahisi utulivu. Huu ni mwenendo wa kawaida. “Hasira inainuka ndani ya moyo Wangu, ikiandamana na hisia ya huzuni inayotapakaa. Wakati macho Yangu yanaangalia matendo ya watu na kila neno lao na kitendo kuwa vichafu, ghadhabu Yangu huzidi, na moyoni Mwangu kuna hali kubwa zaidi ya udhalimu wa ulimwengu wa mwanadamu, ambalo linanifanya kuwa na huzuni zaidi; Natamani kuumaliza mwili wa mwanadamu mara moja. Sijui kwa nini mwanadamu hawezi kujitakasa katika mwili, kwa nini mwanadamu hawezi kujipenda katika mwili. Yawezekana kwamba ‘kazi’ ya mwili ni kubwa sana?” Katika maneno ya Mungu leo, Mungu amemfichulia mwanadamu hadharani wasiwasi wote ulio ndani ya moyo Wake, bila kuficha chochote. Wakati malaika wa mbingu ya tatu wanamchezea muziki na kumpigia vibati, Mungu bado anawatamani sana watu walio duniani, na ni kwa ajili ya hili ndipo Anasema “Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Moyo wangu unajawa na huzuni ghafla, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha.” Ni kwa sababu hii ndio Mungu anasema maneno haya: “Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakomesha maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu.” Huzuni ya Mungu inaongeza chuki Yake kwa pepo, na hivyo Anafichua mwisho wao kwa umati mapema. Hii ni kazi ya Mungu. Daima Mungu ametaka kuunganishwa tena na watu wote na kuimaliza enzi ya kale. Watu wote kotekote duniani wanaanza kusonga—ambalo ni kusema, watu wote chini ya dunia wanaingia katika uongozi wa Mungu. Kwa hiyo, mawazo yao yanageuka na kuwachukia wafalme wao. Punde si punde, watu wa dunia wataingia katika machafuko na wakuu wa nchi zote watakimbia kwenda kila upande, hatimaye watu wao watawaingiza kwenye bamba la kukata kichwa. Huu ndio mwisho kabisa wa wafalme wa pepo; hatimaye, hakuna mtu atakayeweza kutoroka, wote lazima waupitie. Leo, wale ambao ni “wajanja” wameanza kujiuzulu. Wanapoona kwamba mambo hayaonekani kuwa mazuri, wanatumia fursa hii kusalimu amri na kutoroka shida ya msiba. Lakini Nasema wazi, kazi ambayo Mungu anafanya katika siku za mwisho ni hasa kumwadibu mwanadamu, kwa hiyo watu hawa wangewezaje kutoroka? Leo ni hatua ya kwanza. Siku moja, wote kotekote ulimwenguni wataingia katika ghasia ya vita, watu wa dunia hawatakuwa na viongozi tena, ulimwengu wote utakuwa kama rundo la mchanga uliochimbuliwa, usioongozwa na mtu yeyote, na watu watayajali tu maisha yao wenyewe, bila kumjali mtu mwingine yeyote, kwani kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu—ndiyo maana Mungu anasema, “binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine kulingana na mapenzi Yangu.” “Tarumbeta za malaika” ambazo Mungu anazungumzia sasa ni ishara, zinamwonya mwanadamu, na wakati tarumbeta zitalia mara nyingine, siku ya mwisho ya dunia itakuwa imefika. Wakati huo, kuadibu kote kwa Mungu kutaifika duniani kwa ukamilifu wake; hii itakuwa hukumu katili, na kuanza rasmi kwa nyakati za kuadibu. Miongoni mwa Waisraeli, mara nyingi kutakuwa na sauti ya Mungu ili kuwaongoza kupitia mazingira tofauti, na pia malaika wataonekana kwao. Waisraeli watakamilishwa katika miezi michache tu, kwa sababu hawatastahili kupitia hatua ya kuondoa sumu ya joka kubwa jekundu, itakuwa rahisi kwao kuingia kwenye njia sahihi chini ya aina mbalimbali ya uongozi. Kutokana na maendeleo yaliyo Israeli inaweza kuonekana hali ya ulimwengu wote, na hii inaonyesha jinsi hatua za kazi ya Mungu zilivyo za haraka. “Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu!” Zamani, Mungu alitawala tu mbinguni. Leo, Anatawala duniani; Mungu amechukua mamlaka Yake yote, na hivyo inatabiriwa kuwa wanadamu wote hawatakuwa tena na maisha ya kawaida ya binadamu, kwa kuwa Mungu atapanga upya mbingu na dunia, na hakuna mtu anaruhusiwa kuingilia. Hivyo, mara nyingi Mungu humkumbusha mwanadamu kuwa “wakati umewadia.” Wakati Waisraeli wamekwisharudi katika nchi yao—siku ambayo nchi ya Israeli itakuwa imepatwa tena—kazi kubwa ya Mungu itakuwa imekamilika. Bila mtu yeyote kutambua, watu duniani kote wataasi, na nchi kotekote ulimwenguni zitaanguka kama nyota zilizo mbinguni; kufumba na kufumbua, zitakuwa magofu. Na baada ya kuwashughulikia, Mungu atajenga ufalme unaopendwa naye.

Iliyotangulia: Sura ya 26

Inayofuata: Sura ya 28

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp