194 Mungu Kupata Mwili ni Kitu Rahisi?

1 Miongoni mwa binadamu, Nilikuwa roho ambaye hawakuweza kuona, Roho ambayo hawangeweza kuigusa. Kwa sababu ya hatua Zangu tatu za kazi duniani (kuumba ulimwengu, ukombozi, na kuiharibu), Naonekana miongoni mwao katika nyakati tofauti ili kutenda kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Mara ya kwanza Nilipokuja miongoni mwa binadamu ilikuwa katika Enzi ya Ukombozi. Bila shaka Nilikuja miongoni mwa jamii ya Wayahudi. Sababu Yangu ya kufanya kazi hii mwenyewe ilikuwa kwa sababu Nilitaka kutumia kupata mwili Kwangu kama sadaka ya dhambi katika kazi Yangu ya ukombozi. Kwa hivyo watu wa kwanza kuniona Mimi walikuwa Wayahudi wa Enzi ya Neema. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza Mimi kufanya kazi Nikiwa katika mwili.

2 Katika Enzi ya Ufalme, kazi Yangu ni kushinda na kutakasa, kwa hivyo kwa mara nyingine Nafanya kazi ya uchungaji katika mwili. Hii ni mara Yangu ya pili kufanya kazi katika mwili. Katika hatua mbili za mwisho za kazi, wanachokutana nacho watu si tena Roho asiyeonekana, asiyeshikika, bali ni mwanadamu ambaye ni Roho Aliyefanyika mwili. Hivyo machoni pa binadamu, Nilikuwa tena mtu asiye na sura wala hisia za Mungu. Zaidi ya hayo, Mungu ambaye watu huona, si wa kiume pekee, bali pia ni wa kike, kitu ambacho ni cha kushtua na kushangaza kwao. Muda baada ya muda, kazi Yangu ya ajabu huziondoa imani za kale ambazo zimekuwa kwa miaka mingi sana. Watu hushangazwa!

3 Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyeongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa na binadamu, na tofauti kwamba mmoja alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki.

Umetoholewa kutoka katika “Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 193 Kile Mungu Aonyesha kwa Wote ni Tabia Yake ya Haki

Inayofuata: 195 Mungu ni wa Kawaida Jinsi Usemavyo?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp