227 Biblia Nzima Imetolewa kwa Msukumo wa Mungu?
1 Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Huu ni ufahamu wenye makosa wa mwanadamu, na hauafikiani kabisa na kweli. Kwa kweli, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu.
2 Nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, sembuse kuona maono ambayo Yohana aliona. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, n.k wakati huo. Yote aliyoyasema ambayo yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hayakuweza kumwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na kufuru kukubwa sana kwa watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa!
Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili