572 Hii ni Imani ya Kweli Katika Mungu?

1 Watu huona tu kupata neema na furaha ya amani kama ishara ya imani katika Mungu, na kutafuta baraka kama msingi wa imani katika Mungu. Watu wachache sana wanatafuta kumjua Mungu au kutafuta mabadiliko katika tabia zao. Imani ya watu katika Mungu hutafuta kumfanya Mungu kuwapa hatima inayofaa, kuwapa neema yote chini ya jua, kumfanya Mungu mtumishi wao, kumfanya Mungu adumishe uhusiano wa amani, wa kirafiki pamoja nao, na ili kusiwe na mgogoro wowote kati yao. Yaani, imani yao kwa Mungu inahitaji Mungu kutoa ahadi ya kutimiza mahitaji yao yote, kuwapa chochote wanachoomba. Wanahitaji Mungu kutomhukumu mtu yeyote au kushughulika na mtu yeyote, kwa kuwa Mungu daima ni Mwokozi Yesu mkarimu, ambaye huwa na uhusiano mzuri na watu wakati wote na mahali pote.

2 Wanavyoamini ni hivi: Watu daima humwomba Mungu vitu bila haya, na Mungu huwapa kila kitu kwa upofu, kama wao ni waasi au watiifu. Wao daima wanataka “malipo ya deni” kutoka kwa Mungu, na Mungu, lazima Alipe “deni Lake” bila upinzani wowote, na “kulipa” mara dufu, kama Mungu amepata chochote kutoka kwao au la. Anaweza tu kuwa chini yao; Hawezi kuwapanga watu kiholela, sembuse Hawezi kuwafunulia watu hekima Yake ya kale ya siri na tabia ya haki kama Anavyotaka, bila ruhusa yao. Wao huungama tu dhambi zao kwa Mungu na Mungu huwasamehe tu, na Hawezi kuchoshwa na hilo, na hii inaendelea milele. Wanamwamuru Mungu tu na Yeye anatii tu. Je, si siku zote mmeamini kwa njia hii?

Umetoholewa kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 571 Watu Hawamtendei Mungu kama Mungu

Inayofuata: 573 Yako Wapi Maonyesho Yako ya Uaminifu kwa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki