751 Ayubu Alitumia Maisha Yake Yote Kutafuta Kumjua Mungu

1 Ayubu alimiliki na kufuatilia mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawa alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo kwazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawa alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuza binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawa miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu kutokuwa wa ajabu kwa maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

2 Katika macho ya Ayubu, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Hakuwa amemwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa ajabu duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu havikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala havikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote.

3 Maisha ya Ayubu, yalikuwa utambuzi, katika maisha yake ya kila siku, wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye Amejificha miongoni mwa mambo yote. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti ya moyo wa Mungu na maneno ya Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote lakini anaonyesha sauti ya moyo Wake na maneno kwa kutawala sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule ufahamu na maarifa sawa kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 750 Sababu ya Ayubu Kupata Sifa ya Mungu

Inayofuata: 752 Thamani ya Maisha ya Ayubu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp