192 Hukumu ya Mungu Huniokoa Kutokana na Dhambi

1 Niliapa mara nyingi kuacha kila kitu na kumfuata Bwana, lakini sikuweza kuondokana na majaribu ya utajiri na umaarufu. Nilihisi kwa kweli kuwa ilikuwa heshima kuteseka ili kueneza injili na kumshuhudia Bwana, lakini nilihisi mwenye kukerwa na mwenye aibu nilipokabiliwa na mateso na taabu. Niliamua mara nyingi kufuata amri za Bwana na kuwapenda wengine kama ninavyojipenda, lakini nilipanga njama na kushindania hadhi na wafanyikazi wenzangu, nikiishi dhambini. Nilifunga na kuomba mbele za Bwana mara nyingi, nikisema kwa sauti: Ee Bwana! Utarudi lini na kuniokoa kutoka katika lindi kuu la dhambi? Nitatakaswa lini na kuingia katika ufalme wa mbinguni pamoja na Wewe?

2 Katika mshangao wangu nasikia sauti ya Mwenyezi Mungu ikigonga mlangoni mwa moyo wangu. Maneno Yake yote yanauchoma moyo wangu kama upanga mkali, yakifunua ukweli wa upotovu wangu. Nilimwamini Bwana ili nipate tu baraka na kuingia katika ufalme wa mbinguni, nilikuwa nikifanya tu mapatano na Bwana. Nilifurahia neema Yake lakini sikufikiria kulipa mapenzi yake. Dhamiri yangu au mantiki yangu ipo wapi? Nilizungumza juu ya kushuhudia kwa Bwana lakini badala yake nilifanya kazi kwa ajili ya hadhi; nilimdanganya Bwana. Nilidhani nilibadilika kwa kweli kwa sababu nilifanya matendo kadhaa mema. Nilipokabiliwa na majaribio nililalamika moyoni mwangu huku nikiamini kuwa nilikuwa shahidi. Niliishi katika dhambi, nikitenda dhambi na kutubu kila siku, lakini bado nilitamani kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ninapoona haki ya Mungu na utakatifu Wake, sina mahali pa kuficha aibu yangu, na nasujudu.

3 Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu ni kama kupitia usafishaji wa ziwa la moto. Nimekuwa mwenye kiburi na mwasi mara nyingi sana, Mungu ameniadibu na kinfundisha nidhamu kwa ukali. Ninaposisitiza njia yangu, Roho Mtakatifu ananiacha na ninaishi gizani. Nimekuwa mkaidi na mwasi mara nyingi, kila wakati nikitaka kutoroka hukumu ya Mungu. Maneno ya Mungu yananipa nuru na huniongoza nielewe kazi Yake. Hukumu yote ambayo Mungu humfichulia mwanadamu ni ukweli na haki. Kumwamini Mungu pasipo kutii hukumu Yake, ningewezaje kumjua Mungu au kupata ukweli? Bila kufuatilia ukweli, ningewezaje kuepa ushawishi wa Shetani? Kupitia majaribio nimeona kwamba hukumu na kuadibu kweli ni upendo wa Mungu. Hukumu ya Mungu imeniokoa na ninaishi kwa kudhibitisha mfano wa binadamu.

Iliyotangulia: 191 Maneno ya Mungu Yaliuzindua Moyo Wangu

Inayofuata: 193 Rehema ya Mungu Ilinihuisha Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp