783 Kumjua Mungu ni Heshima ya Juu Zaidi kwa Viumbe

1 Kutia ukweli kwenye vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kuu hata zaidi. Na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama kiasi kipi kinahesabiwa kama kumjua Mungu. Hili ndilo linalomshangaza mwanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na mwanadamu—na hakuna awezaye kujibu swali hili, kwa sababu, hadi leo, hamna katika wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii.

2 Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapotambulishwa kwa mwanadamu, kutakuwepo katika mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati ya kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, hapo awali hakujawahi kuwa na kazi kama hii katika historia ya ukuaji wa mwanadamu.

3 Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe wote? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itapokea malipo. Bila kujali jinsia yao ama uraia wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni ya mwisho na ya juu zaidi kuwahi kutekelezwa katika miaka 6000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi inayodhihirisha kila kundi la mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 782 Kumjua Mungu Lazima Ujue Hatua Tatu za Kazi Yake

Inayofuata: 784 Ni kwa Kumjua Mungu tu Ndiyo Unaweza Kufuata Hadi Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp