785 Kumjua Mungu, Lazima Ujue Maneno Yake

1 Kumjua Mungu kunapaswa kutimizwa kupitia kwa kusoma na kuyaelewa maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake. Kutoka kwa maneno ya Mungu unaweza kuuona upendo Wake na wokovu kwa wanadamu, na vile vile mbinu Yake ya kuwaokoa…. Hii ni kwa sababu maneno ya Mungu yanaonyeshwa na Mungu Mwenyewe bali hayajaandikwa na mwanadamu. Yameonyeshwa na Mungu binafsi- Yeye; Mungu mwenyeweAnaeleza maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. Kwa nini yanaitwa maneno kutoka moyoni? Ni kwa sababu hayo hutolewa kutoka ndani kabisa, na yanaonyesha tabia Yake, mapenzi Yake, mawazo Yake, upendo Wake kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na matarajio Yake ya wanadamu….

2 Matamshi ya Mungu yanajumuisha maneno makali, na maneno ya upole na yenye kuzingatia, na vile vile maneno mengine ya ufunuo ambayo hayalingani na matakwa ya binadamu. Ikiwa unayaangalia tu maneno ya ufunuo, unaweza kuhisi kwamba Mungu ni mkali. Ikiwa unaangalia maneno ya upole tu, utaweza kuhisi kuwa Mungu sio mweneye mamlaka sana. Hivyo basi hupaswi kuyachukua nje ya muktadha; badala yake yaangalie kutoka kila pembe. Wakati mwingine Mungu huzungumza kwa mtazamo mpole na wenye huruma, na hivyo basi watu wanauona upendo Wake kwa wanadamu; wakati mwingine Yeye huzungumza kwa mtazamo mkali sana, na hivyo basi watu wanaona tabia Yake ambayo haitavumilia kosa lolote. Mwanadamu ni mchafu kwa njia ya kusikitisha, na hastahili kuuona uso wa Mungu au kuja mbele Zake. Kuwa watu sasa wanaweza kukubaliwa kuja mbele Zake ni kwa neema Yake tu.

3 Hekima ya Mungu inaweza kuonekana kutokana na jinsi Yeye anavyofanya kazi na kwa umuhimu wa kazi Yake. Watu bado wanaweza kuona mambo haya katika maneno ya Mungu hata bila mwingiliano wa moja kwa moja kutoka Kwake. Wakati mtu ambaye kwa kweli ana ufahamu wa wa Mungu anapowasiliana na Kristo, kuwasiliana kwake na Kristo kunaweza kulingana na ufahamu wake wa Mungu; hata hivyo, wakati mtu ambaye ana ufahamu tu wa kinadharia anakutana na Mungu, hawezi kuona uhusiano. Kipengele hiki cha ukweli ni siri kubwa zaidi; ni ngumu kuelewa. Jumlisha maneno ya Mungu ya siri ya kupata mwili, yaangalie kutoka pande zote, na kisha Sali pamoja, tafakari, na shiriki zaidi kuhusu kipengele hiki cha ukweli. Kwa kufanya hili utaweza kupata nuru ya Roho mtakatifu na uje kuelewa. Kwa sababu wanadamu hawana nafasi ya kuwasiliana na Mungu moja kwa moja, lazima wategemee uzoefu wa aina hii kupata njia zao na kuingia kidogo kwa wakati ili kupata maarifa ya kweli ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 784 Ni kwa Kumjua Mungu tu Ndiyo Unaweza Kufuata Hadi Mwisho

Inayofuata: 786 Mwanadamu Amjua Mungu Kupitia Uzoefu wa Neno Lake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp