965 Kweli Unaijua Tabia ya Mungu ya Haki?

1 Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia. Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki?

2 Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini. Je, hili si la kujiadhibu? Kwa kweli, unaelewa kweli, na una uhakika wa nia za Mungu? Daima umetumia “Majaaliwa ya Mungu” kusawiri na kukana maneno ya Mungu. Huku ni kumuelewa Mungu visivyo kukuu! Huelewi kazi ya Mungu na huyaelewi mapenzi ya Mungu katu; hata zaidi, huelewi nia nzuri ambazo Mungu ameweka katika miaka Yake 6,000 za kazi ya usimamizi. Unayaelewa visivyo madhumuni ya Mungu, huyaamini maneno ya Mungu, huuweki ukweli kwenye vitendo wala kujitolea unapotimiza wajibu wako. Je, unawezaje kuyaridhisha mapenzi ya Mungu?

3 Watu wengi hawajawahi kulenga kuweka ukweli katika vitendo ama kubadili tabia zao. Wao tu hutilia maanani kuuliza ikiwa watapata hatima nzuri ya mwisho, jinsi Mungu atakavyowashughulikia, ikiwa Ana majaaliwa yao kuwa watu Wake na mambo mengine ya uvumi. Je, watu hawa ambao hawajashughulika na kazi ya kweli wanawezaje kupata uzima wa milele? Sasa Ninawaambia kwa dhati: Watu waliojaaliwa wasiouweka ukweli katika vitendo wataondolewa mwishowe, na ni wale tu wanaojitumia kwa kweli kwa ajili ya Mungu na kufanya kadri wawezavyo kuuweka ukweli katika vitendo wataweza kusalia na kuingia katika ufalme wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 964 Kila Kitu Afanyacho Mungu ni cha Haki

Inayofuata: 966 Mungu ni Mwenye Haki kwa Kila Mtu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp