823 Ni Kwa Kujua Matendo ya Mungu Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kumshuhudia Kweli

1 Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, basi Mungu hataisifu imani yako. Ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha.

2 Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaelekeza wanadamu, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 822 Jinsi ya Kushuhudia kwa Mungu ili Upate Matokeo ya Vitendo

Inayofuata: 824 Akili Anayopaswa Kuwa Nayo Mwanadamu Baada ya Kushindwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp