784 Ni kwa Kumjua Mungu tu Ndiyo Unaweza Kufuata Hadi Mwisho

1 Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho.

2 Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi.

3 Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 783 Kumjua Mungu ni Heshima ya Juu Zaidi kwa Viumbe

Inayofuata: 785 Kumjua Mungu, Lazima Ujue Maneno Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp